uchumba

Mising

Member
Joined
Aug 3, 2018
Posts
11
Reaction score
3
Naomba ushauri jamani ndugu zangu nilipendana na binti mmoja kwa kipindi cha muda wa miaka minne hadi sasa lakini ikafikia muda yeye baada ya kumaliza chuo tukaamua kuwajulisha wazazi ili taratibu zingine zifuate barua, washenga na nyinginezo lakini sasa mahari iliyotajwa milioni tano mimi sina hata baiskeli na binti tunapendana hatari sasa anaujauzito wangu na wazazi hawajajua hili sasa nifanyeje ili nipeleke mahali kwao maana binti anataka nimuoe na wazazi washasema kumtoa pale kwao mpaka pesa yote itimie mil.5 sasa nipo njia panda nifanyeje hapa wadau maana nataka nimuoe huyu.
 
Una Miaka mingapi?

Ukiishampa mimba binti atakufuata mwenyewe tena utaoa kwa laki 2.5 (jifanye huna tena mpango wa kuoa na nyumbani kwao wajue binti yao ni mjamzito)
 
nina miaka 25 pia najitegemea kwa sasa nina maisha yangu
 
Hivi wazazi wengne wanaakili kweli? Sijaona bint wa milion 5 kwa dunia ya sa hivi.
 
Ndo kama hivo mkuu mimi maisha yangu ya kawaida tu lakini wameniwekea uo ugumu
 
Isije kuwa ulienda ukweni kwa kujikweza , kuwa muwazi kwa kuwapa ukweli juu ya kile ulichonacho kitakachosalia unawaomba utamalizia kidogo kidogo sidhani kama watakataa
 
Washirikishe wazazi wako ,atumwe mtu kwao ,waelezwe hiyo Pesa hamna kwa sasa na mtaitoa kidogo kidogo,mtoe kiasi mchukue jiko
 
Wazazi wengine wana tamaa sana aisee mil 5 usawa huu?.alafu ukute alitumika.mkuu waeleze mkwanja ambao wewe umejipanga na kama wakikataa kabisa utalea mtoto huyo vinginevo mke atakuja tu mwenyewe kwako.
 
Washirikishe wazazi wako ,atumwe mtu kwao ,waelezwe hiyo Pesa hamna kwa sasa na mtaitoa kidogo kidogo,mtoe kiasi mchukue jiko
nshafanya hivo Muda mrefu buthadi ndugu wakawapigia magoti ila wakakataa kuwa hata kuruhusu ndoa mpaka hicho kiasi kikamilike
 
Isije kuwa ulienda ukweni kwa kujikweza , kuwa muwazi kwa kuwapa ukweli juu ya kile ulichonacho kitakachosalia unawaomba utamalizia kidogo kidogo sidhani kama watakataa
wanajua nilipokuwa naishi na maisha yangu ya kawaida tu mimi ni fundi ila hicho kiasi niliwaambia kuwa sina but wakakataa wakidai ndugu wanichangie hili itimie nimuoe binti yao
 
wanajua nilipokuwa naishi na maisha yangu ya kawaida tu mimi ni fundi ila hicho kiasi niliwaambia kuwa sina but wakakataa wakidai ndugu wanichangie hili itimie nimuoe binti yao
Bas kuwa mpole tu huna namna
 
Milion 5?
Aisee watu mnapunwa pesa, kiasi hicho siwezì nikatoa hata kama nimependa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…