As for me, uchumba si kitu chepesi kama wanvyochukulia hawa vijana wa dot com, uchumba ni zao la urafiki mzuri kati ya wapendao, urafiki ambao kila moja amemridhia mwenzake baada ya kuchunguzana na hatimaye kupeana ahadi ya kuoana na hapo ndio uchumba unakuja na pete ya uchumba inavikwa kw wale wenye utaratibu huo, ktk uchumba ndio stage ambayo wazazi wapande zote wanajulishwa na maandalizi ya ndoa yanafuatia, safari ya uchumba kwenda kwenye ndoa inategemea na wahusika wenyewe jinsi walivyojipanga na wanavyopenda ndoa yao iweje iweje. Kwa makubaliano ya pande zote mwanamke na mwanamme kwa pamoja watapanga lini wameremete. Bainafsi nilikaa ktk urafiki na mwenza wangu for about 8 years,mwaka wa tisa nikamvika pete na mahali yake kabisa nikatoa then after months tukameremeta, ,,, yupo pia rafiki yangu ambaye alipata rafiki na wadumu kwa miezi saba, mwezi wa nane kamvika pete ya uchumba na mwezi wa kumi walimeremeta. Hivyo basi kwa mifano hiyo michache unaweza kuona ni jinsi gani wahusika wenyewe wanavyoweza determine lini mwisho wa urafiki, lini mwisho wa uchumba na lini wafunga ndoa, sidhani kama kuna kanuni , sheria wala principle inayoguide lini mwisho wa urafiki,uchumba. Kwa kumalizia tu, vijana wa sasa hivi wao wanaruka stage ya urafiki ambayo ndio nafasi ya kuchunguzana kabla ya kuahidiana kuoana(uchumba), wao wanaanza na ahadi ya kuoana( uchumba) moja kwa moja matokeo yake baada ya mda mapungufu wanayoona kati yao wanashindwa kuvumilia na kuumizana mioyo yao. KWA HIYO, NWASHAURI VIJANA WAPITIE STAGE ZOTE WASIKURUPUKE OTHERWISE MAJERAHA YA MAPENZI YATAZIDI KADRI SIKU ZIENDAVYO