Tyta
JF-Expert Member
- May 21, 2011
- 12,767
- 10,539
rafiki yangu sr yamemkuta yakumkuta. alianza kuwasiliana kwa pm na mwanadada 'mmoja' humu jf. Mawasiliano yakanoga na kukolea kwelikweli. Sr na mwanadada wa jf wakapanga kukutana mahali fulani kwa pm.wakatajiana muda na sehemu ya kukutana hapo.wakati huo kwa pm hizo hizo walishatongozana na kukubaliana. Kila mmoja alisita kumpa nambari ya simu mwingine.
Lakini walikubaliana kukutana sehemu 'maalum' kwa muda 'maalum'. Sr alikuwa wa kwanza kufika na akaweka 'mazingira' tayari. Mara ngo! Ngo! Ngo! Kufungua anaingia mdada. Ni mchumba wa sr. Kila mmoja akaanza kumwagia mwenzake maswali mfululizo kama mvua. Nusura zipigwe na ngumi humo humo. Kila mmoja anamwona mwenzake si mwaminifu. Na uchumba wao uko mashakani. sr anaomba ushauri wenu waungwana. Karibuni!
tutam ''pm'' si ni member wa jf?