Uchumaji wa Mboga

Uchumaji wa Mboga

Sooth

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2009
Posts
3,922
Reaction score
5,628
1. Mboga za aina nyingi, zipo tayari kuchumwa
Za maboga ndizo nyingi, nazi sharti kukunwa
Kuna za bila shilingi, hazihitaji kupondwa
Majani yaliyonyooka, magumu kuchumwa mboga
2.Sokoni zinapatikana, kila mtu kujipatia
Bei zinajulikana, rahisi hutaumia
Muhimu ni kupatana, ili usijejutia

3.Zipo za kutengeneza, madawa yanatumika
Zimekaa kama meza, jiandae kuchunika
Janile gumu kucheza,gonjwa mepata kichaka

4.Jani lililopigwa pasi, gumu kweli kulichuma
Hunyooka ka patasi, haliwezi kunjamana
Pepo hupungua kasi, pa kupita pamebana

5.Napenda lililopinda, urahisi kulikata
Utaona na marinda, wakati linakatika
Nyuma yake utashinda, roho ikisuuzika

6.Jani lililojikunja, lazima lichumwe mboga
Ruhusa kupiga mbinja, hata za mahaba soga
Shika shinani na chinja, anza kwanza na kuoga

Samahani rudia tena
 
Nilimkuta anaanika Nguo Jioni akiwa Nyumbani kwake name nikitoka matembezi ya saa kumi na Mbili ni hapo juzi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom