Mtini
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 1,493
- 2,366
Nadhani mtakubaliana na mimi kuwa unapozungumza juu ya mafanikio ya CHADEMA huwezi kukwepa kuwataja watu wafuatao: Mbowe, Prof. Safari, Salum Mwalimu, Tundu Lissu, Zito Kabwe, Dr. Slaa, John Mnyika, Halima Mdee, Mch. Msigwa n.k
“UCHU” huu ulianzia mbali, kutoka kwa Zitto Kabwe na genge lake, Zitto hakujali madhara yanayoweza kukikumba Chama bali alielekeza macho kwenye kiti cha yule dikt… wa pale chamani ambaye hajawahi ruhusu uchaguzi huru na wa haki wa hiyo nafasi kwa kisingizio cha wazee wa chama wananitaka mimi. Hii ikapelekea Zito na genge lake kutimuliwa chamani na kukiacha chama kikipita katika wakati mgumu.
Kabla maumivu ya Zito hayajaisha, Mbowe akampokea Lowasa bila maridhiano na wenzake. Mbowe alikuwa tayari kufanya lolote kumpokea Lowasa hata kama ni kwa gharama ya kuwapoteza watu maarufu waliokisaidia Chama kufika mahali kimefika.
Leo “IKULU” imekosekana na “KESHO” ya chama imekosekana, maana morali ya baadhi ya watu waliokifikisha Chama kwenye KEKI YA MAFANIKIO imeanza kushuka.
MBOWE bado hujachelewa ni wakati muafaka sasa wa wewe kumchinjia Lowasa Baharini na Kuwaangukia wenzako na kuuomba radhi UMMA WA CHADEMA na kujiuzuru ili kuruhusu waliondoka kurudi na waliokufa mioyo kufufuka upya ili kurudisha imani kwa watanzania.
I STAND TO BE CORRECT TIME WILL TELL