Uchoyo mbaya jamani

Uchoyo mbaya jamani

Dejane

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
51,002
Reaction score
72,284
Habari gani mabibi na mabwanaa,

Dinazarde nakuja tena kuchanaa natokeaa jiji la Mwanza na thamani ya juu kama Samaki wa Mwanza "SATO"
heheeheeehee! watu8 usione wivu njoo Mwanza ule Samaki banaa au ntakutumiaa kwa watsapp au sio men!

Hayaa jamaniii leo nimekumbukaa kisa cha zamani kidogo japo kidogo kinitoee roho mie Mungu mkubwaa Alihamdulillah pia bwana asifiweee kwa uwezo wake:.

Zamani nilivyokua mdogo nilikua mji fulani hivi yaani Samaki ni adimu kwelii kuwapataa sasa nilikua naishi kwa bibi yangu pia alikuwepo shangazi yangu kipenzii alinipenda sana tokea nikiwa mdogo.

Sasa pale home kulikua na Hotel kwa hiyo mara moja moja shangazi yangu alikua akiagiza Samaki toka Mwanza zinaletwa hapo home zinatengenezwa na kukaangwaa halaf zinauzwa mle hotelini.

Sasa zikiletwa Samaki mimi ndio mdogo lazima nipewe mkia wa samaki nile siku hiyo kwangu ni bonge la shangwee aisee!

Sasa ikatokea kuna binti mmoja jirani yetu tulikua tunasoma nae akachukuliwaa na Shangazi yangu tukawa tunaishi nae pale home kwa hiyo wadogo tukawa mimi na yeye!

kasheshe likaanzaa yaani kila ntakacholetewaa lazima tugawane au tunagawanishwaa basi mimi naona sifaidi natamani arudishwe kwao aisee!

Tukipakuliwa msosii tunakula naee nikawa sipendi napenda kula mwenyewe peke yangu,basi nikawa nasingiziaa kwa bibi na shangazi kua flani anakula sana pia anakula haraka haraka mi nakua sishibiii YAANI HUO WOTE NI UCHOYO WANGU MIE HAHHAHA
basi kila mtu akawa anakula msosi wake peke yakee.

Nakumbuka siku moja zililetwaa Samakii kama kawaida zikatengenezwaa nikabakishiwaa mkia wangu miee sasa yule binti alikua ametoka sijui aliendaa wapi kwa muda ule weeee nikaenda nikajificha chumbani kwa Babu yangu maana mle chumbani hakuna aliekua anaingia ovyo ovyo hata bibi yangu pia alikua haingii mara kwa mara maana kabila langu upande wa baba yaan watu wakioana wakafikiaa kuzeekaa basi wanatengana vyumba babu analala chumba chake na bibi pia chumba chake piaa.

Basi nikamtafuna haraka haraka ili yule binti akija anikute nishamla samaki ile namaliziaa tu kula samaki nikanigwa mfupaa ukakwamaa koonii weee niliona kama nakufa mpaka machozi yakanitoka bila hata kupendaa pakawa hapakalikii chumbani nikatoka njeee kabisaa nikafanya kila namna ule mwiba hautoki tu halafu pia unanipa maumivu basi nikapata wazo nichukue mswaki nijichokonoe maana kidole hakitoshi LAHAULAA WALA QUWATA ILA BILLAH LIAZIM si nikatapika mkia wotee ule na mwiba wa samaki ukatokaa kooni nikajisikiaa shwari basi nikapotezeaa maana ilikua kidogo tu nikasalimiane na Israel baada ya hapo sikumwambia mtu yeyote pale nyumbani ikabaki siri yangu basi nafsi ikawa inanisutaa na kuniambiaaa Unaona uchoyo ulivyo mbayaaa yaani kula tu Samaki mpaka ukajificheee!

Tokea siku hiyo nikaacha uchoyo wa vyakula hata kikiwa kidogo tunakula wote tuliopo nyumbanii aiseeee hua siisahau hii,
Sasa kuna watu ni wakubwa lakini uchoyo ni asili yao jamani kama una tabia ya uchoyo iachee hasa kwenye chakula kama kipo acha watu wale kama hakipo basi.
Ni hayo tu jamani japo inachangamsha lakini inafurahishaa pia inafundishaaaaa Dinazarde a.k.a MUKE YA MUSUKUMA
 
Unanikumbusha na mimi, kuna siku Daddy aliniletea Ice cream, kukawa kuna Rafiki yangu amekuja kucheza na mimi... nikaanza kumfukuza, kacheze kwenu...!
 
[/COLOR][/SIZE]
Unatuambia ili iweje?

Hahhhhahhha wivu tu muonee kwa hiyo we umepaona hapo tu kwenye MUKE YA MUSUKUMAA basi umenunaa najua unataka pichaaa subiri Tyta ajee wala usikondee
 
Last edited by a moderator:
Sasa zikiletwa Samaki mimi ndio mdogo lazima nipewe mkia wa samaki nile siku hiyo kwangu ni bonge la shangwee aisee!!!!!!!

Hii point yako hapo juu nimeipenda!
 
Sasa zikiletwa Samaki mimi ndio mdogo lazima nipewe mkia wa samaki nile siku hiyo kwangu ni bonge la shangwee aisee!!!!!!!

Hii point yako hapo juu nimeipenda!

Na wewe ulikua mdogo peke yako kwenu eeeeeeehee
 
Back
Top Bottom