Uchovu wa mwanaume kipindi mkewe mjamzito

Wakuu,eti hii ina ukweli?mwanaume anakuwa mchovu naye anapenda kulala lala wakati mkewe mjamzito..eti wanasaidiana uchovu?hebu ambao mna wake ambaowashakuwa wajawazito fungukeni kuhusu hilo..kuna ukweli?

Ni kweli mkuu na hu ila si kwa kila mimba ,kwani kila mimba huja na staili tofauti.hii ya kulala na uchovu ilishanikumba.kuna wengine huumwa kabisa
 
Naunga mkono hoja
Mke wangu wakati ni mjamzito miezi mitatu ya kwanza nilitapika sana kichefuchefu sana kula udongo na ndimu kwa sana na nilikuwa wakati mwingine mchovu hata kazini kuna wakati nilikuwa siwezi kwenda wakati yeye wala hajisikii kichefuchefu wala kutapika mpaka alikuwa ananionea huruma ila kuanzia mwezi wanne na kuendelea ile hali sikuwa nayo tena kwakweli niliteseka sana kipindi hicho ijapokuwa sijui kulikuwa na connection gani kwani hospitali nilipoenda hawakuona tatizo lolote lile ila nakumbuka muuguzi mmoja mama mtu mzima aliniuliza mkeo anaujauzito nilipomuambia ndio akanisikitia tu na kuniambia hiyo hali itaacha yenyewe

Mi niligonga ugali mlenda mpaka nikashika adabu,hadi wafanyakazi wenzangu wakanishtukia,hakuna msosi uliokuwa unapanda kama ugali na mlenda au bamia.hata samaki niliokuwa napenda sana waligoma
 
sio mke tu hata ndugu, nakumbuka sister angu alipokuwa mja mzito miez ya mwanzoni niligonga mihogo mibichh plus chumvi plus pilipili, mh kuja kujua nilimaind
 
inawezekana tusibishe kwani kuna mambo mengi bado kujulikana katika tasnia ya maumbile na sayansi kwa ujumla. mfano kuna kitu kinaitwa 'intuition' ambapo mtu aweza kujua jambo bila kuona. nadhani katika maisha yako uliwahi kumuwazia mtu mara ukaona akitokea. ukiunganisha na hilo alilosema gfsonwin kuhusu emotions waweza pia pia kuunganisha na suala la kisaikolojia kwamba feelings na matarajio ya mwanaume vinaweza kuzifanya homoni katika mwili wake uzalishe vichocheo ambavyo vitasababisha hali tofautitofauti kama uchovu, furaha hasira, kichefuchefu n.k. Hakuna anayeweza kutoa jibu sahihi labda kama amefanya utafiti au kusoma tafiti kuhusu jambo hili.
 
Wakuu,eti hii ina ukweli?mwanaume anakuwa mchovu naye anapenda kulala lala wakati mkewe mjamzito..eti wanasaidiana uchovu?hebu ambao mna wake ambaowashakuwa wajawazito fungukeni kuhusu hilo..kuna ukweli?

Labda kama hiyo mimba mliiendea wote kwa mganga
 
Back
Top Bottom