Uchokozi wa Edo: Roho mbaya ya kushangaa mishahara mikubwa ipo

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Thursday June 20 2019
uckozipic.jpg

Juzi rafiki yangu alinitafuta akiwa likizo Dar es Salaam. Alikuwa ametokea kazini kwake katika mgodi mmoja ulioko mikoani. Akanidokeza jinsi vijana wa Namba Moja wanavyochapa kazi kwa sasa. Wakaguzi wa mara kwa mara wanakwenda migodini kukagua hili na lile.

Moyoni nikashangilia. Tumeibiwa sana katika eneo hilo. Namba Moja anarekebisha mambo. Baadaye akanitia huzuni kidogo. Wakaguzi huwa wanashangaa mishahara yao.

Wanashangaa mishahara ya Watanzania wanaopiga kazi migodini. Wanadai ipo juu sana. Hawana shida na mabosi wa kizungu. Bosi mmoja anachukua dola 30,000 kwa mwezi, mwingine anachukua dola 20,000 kwa mwezi. Haina tatizo na hawaoni tatizo.


Wanashangaa wanapoona kijana wa Kitanzania anachukua Sh8 milioni kwa mwezi baada ya makato ya kodi. Wengine wanachukua hadi Sh12 milioni kwa mwezi.

Roho zinawauma na kama migodi ingekuwa chini ya Serikali hapo hapo wangemshauri mheshimiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa mishahara hiyo. Ni vile tu hawana mamlaka wala nguvu ya kufanya hivyo kwa sababu wazungu wanaipanga hii mishahara kutokea kwao.

Kwa nini wakaguzi huwa wanashangaa mishahara mizuri? Mshangao unatoka wapi? Roho mbaya tu. Mshangao hautoki kokote zaidi ya roho mbaya. Hatuna mazoea ya kulipana vizuri.


Kampuni ya nje inapomlipa kijana wa Kitanzania fedha nzuri kuna watu inawakera. Wanaposikia mgeni analipwa hizo fedha hawana tatizo sana.

Tumeathirika kisaikolojia kwamba Mtanzania hastahili kulipwa Sh20 milioni kwa mwezi. Haiwezekani. Mioyo ya Watanzania wengine imegoma kushangilia. Ni dalili ya roho mbaya au kutojiamini ambayo wengi tunazaliwa nayo.


Unaposikia wanasiasa wanatuambia kuna nafasi za kazi za wageni ambazo zinastahili kufanywa na Watanzania, usiamini kwamba wanataka kazi hizo zifanywe na Watanzania kwa mshahara uleule wa mgeni. Nafasi hiyo akichukua Mtanzania majadiliano ya mshahara yataanza upya. Kama katika nafasi hiyo mgeni alikuwa analipwa Sh20 milioni, basi watataka Mtanzania alipwe Sh5 milioni.

Kauli zetu za roho mbaya ni kama vile “atatusumbua sana mtaani”. Mwingine atanong’ona “huyu mshahara wake si unaweza kulipa watu wawili na kazi zikaenda?”. Ni kauli za roho mbaya ambazo Watanzania inabidi tuanze kuzitafakari
 
hahahahaahaahaha mnisaidie kumtag mkuu BAMS.. najua vijana watafikiwa tu huko watu hampendi kuwaona msiowajua ambao hawana Sir names mnazozijua wakisukuma. maLexus Cruiser, Porche Cayene, X5, X3. nk.

Akifanikwa Mtanzania mmoja mmakonde, mnyaki, mzaramo, msukuma, myamwezi nk basi ujue watanzania wengi huko nyuma watakuwa wamepata nafuu..Hawa Wahindi na Waarabu sio watanzania jamani, akili yao iko Oman, Dubai, India, Canada nk usiwaone wajifanya watanzania lengo ni kuchuma..
 
Huyu mshahara wake ni $192,000 sawa na zaidi ya milioni 400 kwa mwaka. Kila kitu chake kuanzia chakula, umeme, maji, usafiri, wafanyakazi analipiwa na walipa kodi kwa mwaka mzima. Sijawahi kumsikia akidai mshahara wake ni mkubwa hivyo aupunguze.
Kabisa, mwaka mmoja zamani kidogo nilipangiwa mshahara wa USD 500, wakubwa fulani walisema ni zaidi ya mshahara wa DC, waliamua mashirika yapunguze mishahara mpaka ikafikia 220,000/=(1998)
 
Kuna jamaa mmoja miaka kama 4 iliopita hivi aliwahi itwa interview NMB kulikua kuna nafasi ya mtaalamu wa IT, sio nafasi ya IT officer ni zaidi ya hapo hio nafasi aliyekuwepo hapo alikua mzungu akawa anataka kurudi kwao huyo mzungu alikua analipwa milioni 8 na extra zingine kama nyumba, fuel allowance, vocha sijui na makorokocho mengine jamaa ni mswahili alifuatilia akapata taarifa jamaa analipwa kiasi hicho cha fedha interview jamaa alifaulu akawaambia mimi nilipeni 5,000,000 hahaha aiseee wabongo wakaona jamaa mbona anataka alipwe hela nyingi hivyo jamaa akawauliza mbona huyu anaeondoka hapa analipwa 8,000,000 mimi nimetaja ya chini ya hapo tatizo liko wapi kama 5,000,000 ni nyingi nipeni 3,500,000 wabongo walipatwa na kigugumizi ila mwisho wa siku walikua wanataka wamlipe jamaa milioni 2 jamaa akawaambia kama ni hivyo tafuteni mtu mwingine..moral of the story wabongo hatupendani miksa wivu
 
Kwa mgodi wa dhahabu na mishahara ya kimataifa, hiyo mishahara ya wabongo kawaida tu, tena inaweza kuwa midogo.

Watu washalipwa mishahara hiyo na zaidi bila kufanya kazi mgodi wa dhahabu (well, banks ni migodi ya fedha).

Tatizo Tanzania hatuendi na mishahara ya kimataifa.

Roho mbaya inachangia sana kutufanya tuzidi kuwa masikini.
 
Kuna Waziri mmoja awamu ya Mkapa wakati makampuni ya wawekezaji kwenye dhahabu yalipoanza kuja kuwekeza. Baada ya kuona mishahara waliyopanga wawekezaji ikiwa minono hata ule wa msafishaji ofisi kuzidi mshahara wake akatoa comment kwa mwekezaji kwamba mishahara ile kwa Watanzania ni mikubwa sana wataishia kuoa wake wengi na kunywa pombe. Sikumbuki ni waziri yupi wa awamu ya Mkapa.

Kwa mgodi wa dhahabu na mishahara ya kimataifa, hiyo mishahara ya wabongo kawaida tu, tena inaweza kuwa midogo.

Watu washalipwa mishahara hiyo na zaidi bila kufanya kazi mgodi wa dhahabu (well, banks ni migodi ya fedha).

Tatizo Tanzania hatuendi na mishahara ya kimataifa.

Roho mbaya inachangia sana kutufanya tuzidi kuwa masikini.
 
Kuna Waziri mmoja awamu ya Mkapa wakati makampuni ya wawekezaji kwenye dhahabu yalipoanza kuja kuwekeza. Baada ya kuona mishahara waliyopanga wawekezaji ikiwa minono hata ule wa msafishaji ofisi kuzidi mshahara wake akatoa comment kwa mwekezaji kwamba mishahara ile kwa Watanzania ni mikubwa sana wataishia kuoa wake wengi na kunywa pombe. Sikumbuki ni waziri yupi wa awamu ya Mkapa.
Ni mambo ya aibu. Watu wanatoka kwao wanataka kulipa mishahara inayoeleweka kimataifa ili wafanyakazi wapige kazi kwa moyo wote, serikali inaleta choyo.
 
Back
Top Bottom