Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

sidhani kama mtu yeyote anaweza akasoma ulichoandika na kushindwa kuona maana iliyofichika; mara kadhaa umefanya hivvyo kumdunisha Nyerere mbele ya hadhara na matokeo yake wanafunzi wako hapa wamefuata cue yako...

MM,

Tusigande hapa.

Nimeweka mengi tu humu toka jana usiku.

Hujaona?
 
Ooh pole sana mzee mwenzangu; ninafahamu nina kawaida ya kuwachosha watu kwa udadisi wangu. Vumilia tu ninajua ulizoea mawazo rahisi rahisi yasiyochosha.



Ala! Sasa mbona wewe huachi kusema "wazee wangu, wazee wangu, wazee wangu"? Ukiacha nami nitaacha... vinginevyo tuendelee kubanana humo humo.



Hujaichambua lolote; nilitaka kusema na kukuuliza maswali lakini najua ungepeperuka tena kama kipepeo anayetafuta maua... Ungekuwa unaujasiri wa kujibu maswali basi santuri hii isingekwama.

''Wazee wangu'' lakini silulizi swali.
 
Najua una frustuations and homa kali kwa kuhofia bakora za ndalicchako juma tatu,nakushauri ukalale na uache kuuharibu huu mjadala,utakua umefanya jambo la maana sana
Mbona nimesha kwambia mtihani huo niliufanya siku nyingi sana, yaani kabla wazazi wako hawajabarehe! mie nilifanya mitihani ikiitwa Cambrige exams, kwanini hutaki kuelewa?Muulize mzee Mohamed akusaidie maana kwa umri wake anaifahamu sana.
 
Mohamed Said,

Germano Pacha alikuwa na cheo gani TAA?

Ritz,

Hebu soma hapo chini jibu lako lipo hapo labda kama utataka ziada:

When the Tanganyika African Association (TAA), TANU's predecessor, held a secret meeting to collect donations to send Germano Pacha to Dar es Salaam to attend the TANU founding conference in 1954, the highest contribution, which was twenty shillings, came from my grandfather, Salum Abdallah.

Germano Pacha was then TAA's Provincial Secretary Western Province.

That meeting was attended by the notables of Tabora including school teachers, Abubakar Mwilima, Harub Said and George Magembe.

These men came to play very important roles during the struggle.

However, my grandfather fell out with President Julius Nyerere, as many were to do, and was detained by the government soon after independence under the 1962 Preventive Detention Act.
 
Sasa kama unataka mtu amuelewe huyo mtu unayetumia kwenye kupasha habari zako ni kwanini usimtaje ili wanaomjua watuthibitishie. Lazima utakuwa una la zaidi ya hili unalolisema angalizo la kutotaja jina. Umeamua kufunguka unemaliza tusiojua tujue

Hapana hizi habari kanipasha mkewe Abdu Sykes.
Jina nililohifadhi ni jina la mumewe marehemu Bi. Sophia.
 
Udini, ugonjwa mkubwa unaolitafuna Taifa kwa sasa, japo hatupendi kulizungumzia tatizo hili!
 
Wakuu Gwalihenzi na DULLAH MSAVIVOR imetosha turejee kwenye mjadala,

Nyerere alikuwa na dada yake anaitwa Sophia.
Bi. Sophia na mumewe walikuwa wakimpenda sana Bwana Abdu.

Abdu akiwafanyia party hadi watoto wao.
Huyu mama ni marehemu sasa.

Yericko atamjua maana ni shangazi lake.

Unajua the ''Tanu spirit ...'' wazee wanasema mpaka uwe umieshi
zama zile ndiyo utaijua.

Mtu anatoa chumba cha mbele nyumbani kwake kuwa ofisi ya TANU.
Hadai kodi.

Chamwenyewe anapanda baiskeli kutoka Dar es Salaam hadi Rufiji
njia nzima anawakatisha watu kadi za TANU.

Akifika Dar es Salaam anamtafuta Idd Faiz kumkabidhi hela za kadi
na yeye wala hachukui hata masurufu kwa ajili ya kujikimu.

Hawa ndugu zetu wanakejeli haya kwa kuwa hawayajui.

Hapana haja ya kuwalaumu sie tuwafahamishe tu wajue kuwa watu hawa walikuwepo
katika historia ya Tanganyika.

Rashidi Ali Meli alikuwa mhasibu wa Dar es Salaam Municipal Council.
kachukua fedha za ofisi kampa Idd Faiz kutunisha mfuko wa safari ya Nyerere UNO.

Rashid Ali Meli alihudhuria ule mkutano wa kwanza wa TANU pale Arnautoglo.
Baada ya kutoa zile fedha asubuhi wakaguzi wamemvamia kufanya ukaguzi...

Pazuri hapa....

Inaelekea makachero walinusa wakapeleka taarifa kwa Waingereza kuwa TANU
wamechota katika hazina ya serikali na Rashid Ali Meli ndiyo mbaya wao.

Huyu kachero katika TANU Wazungu watu kama hawa wanawaita ''mole.''

Huyu ''mole'' mzee wangu mmoja kanitajia alikuwa ndani kabisa katika uongozi
wa juu wa TANU.

Mbona nilitaka kuzimia?

Rashid Ali Meli akikaa Ilala.
Wazee walikesha wakimlilia Allah amnusuru Rashid Ali Meli...

Siku nilipompelekea kitabu cha Abdu Sykes (English Version) Mama Daisy (Mke
wa Abdu Sykes)alinambia, ''Nilikuwa nikimwambia baba yako Bwana Abdu taratibu
na mambo haya. Maana alikuwa na kabati lake la fedha. Yeye akiletewa taarifa kuwa
TANU ofisi kuna tatizo hili haulizi zaidi anaingia ndani anatoka na fedha anakabidhi
basi ilikwenda vile hadi ile biashara yake ya Petrol Station pale Ilala Boma ikafilisika.
Nazerali ndiyo akamkopesha fedha na dhamana akaweka ile nyumba yake ya Stanley.
Uhuru umepatikana baba yako anaambiwa si yeye aliyeasisi TANU...''

Kwa muda mama yangu akajiinamia...

''Ahsante mwanangu Mohamed leo watu watamsoma baba yako na watamjua Abdu
kafanya nini. Nilikutana na Maria baada ya miaka mingi sana pale Diamond Jubilee siku
Nyerere anaaga tulikukaanae wanawake wa Dar es Salaam. Maria akasimama akasema,
''Mimi nafika Dar es Salaam kanipokea Mama Daisy na mumewe marehemu Abdu Sykes...''

Sishangai kama anatoka mtu akasema yeye wazee wangu hakupata kuwasikia.
Atawasikiaje?

Na sisi yeye peke yake wengi humu hawayajui haya ndiyo maana wanasema ''hadithi''
na ''ngano'' za Mohamed Said.

Laiti Nyerere angeliwaadhimisha wazee wangu dunia nzima ingewajua na kuwathamini.

Panatosha.
 
Congo, Rwanda, Haiti, Burundi, Uganda, Sierra Leone, hizi zote nchi za Kiislam.

Mbona umesahau na vita vilivyotokea Angola, Msumbiji, Eritrea, Norhern Ireland, Spain, Srilanka, Vita vikuu ya Kwanza na vya pili, Vietnam, nk! bila shaka hizi pia ni nchi za Kiislam!!!!!
Na hata Mgalatia Hitler alipowaua Mamilioni ya Wayahudi bila shaka hao nao walikuwa..........!
 
Mtu anatoa chumba cha mbele nyumbani kwake kuwa ofisi ya TANU.
Hadai kodi.
mkuu Mohamed Said hiyo spirit hata sasa ipo, tunavipenda vyama vyetu tukiamini ndivyo vitakavyotukomboa,
 
Last edited by a moderator:
Ritz,
nawe una hoja gani! hadi ujibiwe hapa..

Kweli kauzu zaidi ya dagaa hivi hujajiuliza tu kwa nini watu wanakupuuza? Kujibishana na wewe nikujidhalilisha tu wewe ni kukusoma na kukupuuza ni futuhi wetu humu JF michango yako inatuliwaza.
 
Back
Top Bottom