Inasemekana kwamba Mafuta yamegundulika ndani ya Tanzania.
Mungu sasa inatosha, ILAANI kidogo Tanzania.
Kwanini kutupa mafuta ilihali tu MAJUHA?
..
Mkuu, napenda sana watu wanaopost vitu vyenye AKILI humu jamvini, sio kushupalia huyu kasemaje kisiwa Cha Zimbabwe Sijui huyu kaloanisha nanii, lakini Mustakabali wa watanzania ambao uko ndani ya weledi wa uwezo wetu hatujaugusa hasa hasa..
Katika Orodha ya Mabilionea Wa Duniani moja Kati ya biashara zao kiongozi ni Mafuta Na pili Madini, tukatae tukubali mafuta Na Madini ni Nguzo Za uchumi wa serikali yoyote katika DUNIA ya Leo, kuongelea mafuta ni kuongelea vitu vyenye akili .. I support you..
Nirekebishe kauli kwamba Kwamba Mungu ailaani Tanzania kidogo, no Tanzania tumeshajilaani,kujichukia Na kujikataa tena sana tu si kidogo, Mwenyezi Mungu katupa kila kitu jamani, lakini sisi ndio tumejikataa Kwa kukubali kuongozwa Na watu Wenye fikra mfu.. Unajua ukiongizwa Na watu Wenye fikra mfu hata Jamii inakuwa ya kimisukule tu..
Sisemi Kwa Ubaya wala simwonei Mtu ila Kwa Sasa CCM iko madarakani, Na kuna watu maelfu tu wanajiita wakereketwa au washabiki Wa chama hiki, LAKINI count my words, CCM ikiondoka madarakani, chama kingine kikaingia Na kuwafungua wananchi macho Kwa kile chama hiki Na serikali yake vimewatendea wananchi wake, nakwambia hata wale wanaojiita wakereketwa Kama sio wakeketwa Wa chama hiki watajutia Na kulilia wakati wao walioupoteza kuunga mkono wasichokijua..I mean it
NCHI zilizoendelea zilishaapa kujiimarishia ichumi wake Kwa kuzifanya NCHI zinazoendelea kuwa soko Na mashinary zao. Na hii ikienda sambamba Na kuhakikisha zinanyimwa Elimu AMA ya darasani au ya kazini, hii ni pamoja Na kuwahadaa Vijana wao Wenye AKILI kutoka vyuoni Na kuwapatia dhihadi Za elimu (scholarship) Na kuhakikisha wanasomea Kada ambazo sio vumbuzi Na sizizo Na mguso filirishi. Na baada ya hayo huajiriwa Na serikali
Zao ka kukamatwa Na pepo Jamhuri..
Mpango huu ulikuwa wazi hata Mwalimu aliueleza sana sana, lakini kusema bila matendo hakusaidii mbele ya macho yake viwanda vikaanza kuuliwa ivi ivi akiona, vya nguo,vya nyama, vya zana Za kilimo Na hatimaye Leo tunashuhudia NCHI imeshageuzwa gulio la bidhaa Za nje, hadi vijiko..
Fikiria tu kwamba ili Mtu astawi Kwenye chama anahitaji fedha kutoka kwa wale wale wanaotuuzia vitu vyao, NCHI haina bajeti ya uchaguzi hadi viongozi wenu mletewe fedha Za kiwachagua unadhani hii sio LAANA ??!
Tanzania inahitaji Mtu anayejua Nini kiwe Nini na lini..
CCA