Uchimbaji mafuta na nchi ya 'MAJUHA' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchimbaji mafuta na nchi ya 'MAJUHA'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Speaker, Oct 26, 2012.

 1. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Inasemekana kwamba Mafuta yamegundulika ndani ya Tanzania.

  Kama hii ni kweli, basi naomba nianze kwa kusema kwamba Mungu ashukuriwe maana ame tubariki kuliko tunavyostahili, na ame tubaliki kuliko viwango vya akili zetu.

  Mwaka 1965, serikali ya Tanzania iliamua kuanzisha kampuni ya TIPER (Tanzanian and Italian Petroleum Refining Company Ltd).

  Kazi ya hii kampuni ilikua ni kupokea mafuta machafu, Crude Oil, kuyasafisha, na kisha kuhifadhi kwa muda kabla ya kuya peleka kwa wauzaji kama vile BP, Shell nk.

  Katika kusafishia mafuta hapa hapa nchini, tulikuwa tunaweza kunufaika kwa mambo yafuatayo:

  1. Tulipata Bitumen, ambayo ni residue ambazo zina tengezea lami, kwa ajili ya ujenzi wa barabara, na vifaa vya kuezekea nyumba kama mabati, vigae etc

  2. Fuel Oil, ambayo ni mafuta mazito, hutumika kwenye meli, na hata kwenye furnace kwa ajili ya joto kali sana hasa kuyeyushia vyuma nk.

  3. Mafuta ya kulainishia vyuma, kama vile grease ambazo unapaka kwenye minyororo, geti, nk.

  4. Diesel, kwa ajili ya magari makubwa.

  5. Gasoline, kwa ajili ya magari madogo, piki piki etc.

  6. LPG,...ambayo ni gesi tunayotumia kwa kupikia majumbani, wengine wanatumia kwenye gari siku hizi badala ya gasoline.

  7. Na mengineyo mengi.

  Hizi zote ni faida kubwa sana, ambazo tulikua tuna zipata kwa kununua mafuta machafu na kuyasafishia hapa hapa nchini.

  Lakini mwaka 1999, kwa akili za ajabu kabisa, serikali ikasimamisha kampuni hii. Naomba niuite uhujumu uchumi labda mkubwa kuliko maelezo ulio wahi kutokea Tanzania kwa sababu kufungia TIPER kuliua viwanda vingine vingi vidogo vidogo.

  Mwaka 2001, wakaamua waifufue TIPER (Tanzania Internationa Petroleum Reserve),...lakini sasa hivi, kama jina lilivo, ikiwa sio kwa ajili ya kwa ajili ya refining, ila kwa ajili ya kutunza mafuta yaliyoagizwa toka nje.


  Sasa najiuliza:

  1. Hivi kweli tumewahi ongozwa na rais mzalendo? Ni nani aliyeua TIPER ya zamani na kuleta TIPER ambayo sasa ni kama "godauni" tu?

  2. Kulikuwa na ulazima wa kuagiza lami nje ya nchi wakati tulikuwa tunaweza wenyewe kutengeneza hapa hapa nchini? Hizi gharama za kuagiza lami kama product ya crude oil peke yake ni kubwa kuliko zile za kutengeneza mitambo ya refining inayooza pale tuanze kurekebisha makosa yetu?

  3. Crude oil ndani yake unapata materials kwa ajili ya kutengeneza matairi ya magari (refer to General Tyres Tanzania),...serikali inawaza nini kukifufua kiwanda hiki?

  Uganda wamegundua mafuta kwao, Museveni amekataa kuchimba hadi wasomeshe vijana wao kwanza watakaosimamia shughuli hiyo wenyewe, wakati huohuo wakijenga mitambo madhubuti kwa ajili ya kazi hiyo.

  Huku kwetu tunaendelea kulialia mafuta yawe ya muungano au sio, sasa tukianza kuchimba tutasafirisha crude oil kwenda Uganda kusafisha au?

  Hizo gharama zitakuwa ndogo kuliko kufufua TIPER ambayo pia ni itachukua watu wengi sana kwa kuwaajili?

  Mungu sasa inatosha, ILAANI kidogo Tanzania.

  Kwanini kutupa mafuta ilihali tu MAJUHA?
   
 2. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Mkuu nashukuru umeleta hii mada hapa.

  Mimi ninafanya kazi na kampuni hizi za oil na gesi lakini kila nchi ninayoenda biashara hii inashikiliwa na serikali kuu aidha katika kuuza au kuanzia utafiti hadi mauzo.

  Mfano UAE wana kampuni yao inaitwa AGNOC hii inacontrol biashara yote kuanzia utafiti, mikataba hadi kuuza na iko chini ya seriKali. Ukienda Saudia hali ndio ile ile wana kampuni yao inaitwa SAUDI ARAMCO hii ndiyo main Client wa Kazi zote zinazohusiana na mafuta au gesi lakini kwetu tumeuza karibu vitalu vyoote sasa unafikiri tutakuwa matajiri lini?

  Wenzetu nchi zao ni majangwa lakini hadi maji safi wameyapata na kujenga miji mizuri plus kuwalipa wananchi wao pesa sisi hata tupewe vyote sijui kama tutafanikiwa kuutupilia mbali umaskini.
   
 3. M

  Magurudumu JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,751
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Hao wenzetu ni waaminifu na wana uzalendo na nchi zao. Hawaibi wala kufanyia nchi zao ufisadi. Hapa kwetu ni tofauti kabisa. Viongozi wetu unawajua. Ukiwakabidhi miradi nyeti kama hiyo pesa zote zitaishia kwenye mifuko yao, wato wao, mahawara zao n.k.
   
 4. M

  Magurudumu JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,751
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Tanzania mafuta yamegunduliwa Pemba tu na sio kwingineko. Na kama ujuavyo wazanzibar wanataka kujitoa kwenye muungano. Moja ya sababu kubwa ni hayo mafuta ili yawafaidishe wenyewe. Uamsho wanafanya fujo, tatizo ni hayo mafuta ya pemba. Kwa hiyo bora usiseme Tanzania imegundua mafuta. Kama hao wazenji wakifanikiwa kujitoa, hakutakuwa na Tanzania yenye mafuta.
   
 5. Tigga Mumba

  Tigga Mumba JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 747
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Usidanganye watu. Nijibu yafuatayo na usiwe mshabiki:

  1. Yamegundulika block gani
  2. Operator gani ameyagundua?
  3. TVD(total vertical depth) na MD(measured depth) ni ngapi?
  4. Nipe size ya reservoir

  Msiwe washabiki maandazi....

  Process za exploration/drilling na discovery kwa bahati gas au mafuta yakiwepo tena offshore sio kama kukuna ngozi yako.....

  Ni process nzito zinazohitaji resources kibao.

  Acheni maneno ya vijiweni
   
 6. Tigga Mumba

  Tigga Mumba JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 747
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Speaker

  Hakuna mafuta yaliyogundulika block yoyote offshore Tanzania (ocean side).
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Tigga Mumba

  Tigga Mumba JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 747
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Mu-sir

  Sisi tuna matatizo makubwa ya kiutawala. Siasa nyingi mno
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. J

  John W. Mlacha Verified User

  #8
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  Hizo blokc azijue wapi? Kwanza hajui dvd ninini ..yeye kaslikiliza hotuba ya imam anavyowadanganya ili kuwapandisha munkari ya Muungano tu basi anakuja hapa anajua na hapa ni sehem ya mihadhara
   
 9. MWANAWAVITTO

  MWANAWAVITTO Senior Member

  #9
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Speaker

  hili Taifa limeliwa na wenye meno
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mkuu Speaker umenikumbusha hiyo kitu TIPER..... Dah kweli hii nchi ya MAJUHA na UJUHA.....

  Tumejazwa upuuzi na wababaishaji wanaojiita wanasiasa wasio na maono wala ndoto achilia mbali kujiamini kuwa wanaweza kulisogeza Taifa! Sasa kama TIPER ilitushinda, je tutaweza kusimamia kuchimba wenyewe?

  Sisi tumekuwa taifa la kutia uchungu sana sababu maeneo yote sensitive na uchumi wa taifa tunafanya mzaha na hatueleweki mbele ya dunia ukilinganisha na wenzetu:

  Kilimo chetu hoi...
  MIFUGO yetu hoi...
  Nishati ndio usiseme....
  Madini ndio kabisaa...

  Na sasa ndio tunajibebesha balaa jingine la Mafuta na Gesi... Tayari watu wapo busy na masemina, watu mawizarani na ofisi zote za Ikulu ziko busy masafari ya kuzunguka nchi mbalimbali ukiuliza nini, unaambiwa Mafuta na Gesi...

  Ndugu yangu Speaker tufungue tu NGO yetu ya "kuwaelimisha wananchi juu ya changamoto zitakazotokana na uchumi wa gesi na mafuta" lol....

  Utapeli, upigaji nk nk kwa kifupi ni UJUHA tu kama ulivyosema!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  TIPER haikuwahi kufilisika wala kushindwa kazi zake.
  Ila ni uhujumu uchumi tu ulio fanywa na wakubwa,(lawama zote kwa mkapa)
  ili waweze kuingiza mafuta wao,waingize rami,waingize kila product separately kwa
  manufaa yao wenyewe.

  Inatia kichefu chefu kuona jinsi mitambo ya kusafishia mafuta inavo oza
  kwa kutofanya kazi afu tunalia umaskini.

  Hawa wahujumu hawaja tajirika tu kwa dili zao hizo?
   
 12. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Ha ha,hizo NGO ni njia nyingine ya wizi tu.
  Hakuna NGO inayo fanya kazi kwa makusudi iliyo anzishiwa,
  waki jitahidi ni 10% watafanya ila 90% ni matumbo yao tu.

  Naogopa sana kuwa tapeli.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Speaker na Tigga Mumba mna akili sana, Prof. Sos Muhongo naamini atahitaji michango yenu.
   
 14. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  kwa nini walikuwa wanayahifadhi kabla ya kuyapeleka kwa wauzaji?
   
 15. M

  Mea2 Member

  #15
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  tanzania kweli ni taifa la majuha tumebarikiwa rasilimali nyingi sana lakini ujuha wetu ndo unatufanya tunaendelea kuwa maskini,kwa mfano swala la madini kila siku najiuliza ni kwanini wasipeleke watu nje ya nchi kujifunza mambo ya madini na baada ya miaka kadhaa tukaweza kuendesha wenyewe migodi yetu,ukienda kwenye makampuni ya madini mbalimbali utakuta wanaleta watu wa kada zingine kama vile watu wa mazingira,ugavi,uhasibu wakati kuna watanzania ambao wanaweza kufanya kazi hizo kweli taifa letu hili ni ujuha tu kuanzia kwa wananchi mmojamoja hadi kwa viongozi wetu,kwanini nasema hivi kwa sababu sisi kama wananchi wa kawaida kabisa tunaweza kufanya mahamuzi ambayo baadaye yatabaki kuwa historia kwa vizazi vijavyo tuondokane na UJUHAAAAAAAAAAAA
   
 16. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa ufupi, ni kweli mafuta yamegunduliwa na kabla hayajatangazwa rasmi, Prof Tibaijuka aliomba mipaka ya tanzania iongezwe baharini na viwanja vyote huko baharini vimeisha gawiwa kwa vigogo [majina yanahifadhiwa kwa sasa] mkuu wa nchi akiwemo. Kwa hiyo ujue kuwa mafuta yakichimbwa, mikataba itakuwa kati ya wachimbaji na "owners" ambao siyo serikali.

  Lakini mafuta hata yakisafirishwa kwenda sudani, Uganda au Lybia kusafishwa kisha yarudishwe nchini kwa bei kubwa wao si tatizo maana watakuwa wamepata chao. Mungu atusaidie tupate uongozi wa watu wenye hofu na Mungu ambao ni wazalendo pia ili kuanza upya... maana nchi iko pabaya.

  Na ujue kuwa kuua TIPER ya kwanza na kuleta TIPER ya pili, ilikuwa ni fursa ya kuhalalisha wizi maana katika mabadiliko hayo ndipo wizi mkubwa unatokea. Ni kitu gani kimebadilika katika miaka miwili. Unafunga shirika na unalifungua baada ya miaka miwili?

  Mungu atusaidie
   
 17. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Chukua mfano huu "usio hai"
  Nina safisha mafuta lita 500,000 kwa siku.
  BP,Shell,Engen,Oilcom,etc wanaweza kuuza lita 300,000 kwa siku.
  Hizo lita 200,000 zina pelekwa wapi?

  Kumbuka hizo marketing companies hawana uwezo wa kutunza mafuta mengi
  kwa wakati mmoja.
   
 18. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwa kifupi hatujawahi kuwa na kiongozi Mzalendo.
   
 19. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,569
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Tigga mumba na speaker! Suala la mafuta siku zoote ni nyeti saana, rais wa nchi husika ndio anakuwa na mandate kutangaza
   
 20. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  soma hapa: Mafuta, gesi mkombozi mpya kiuchumi Tanzania
   
Loading...