Uchifu ni ushirikina, ukabila na kafara

sambulugu

JF-Expert Member
Jun 1, 2021
3,944
7,436
Jamii ya watanzania ilishatoka huko kwenye uchifu!

Na huu upuuzi ukiendekezwa utaturudisha nyuma sana hasa kwenye baadhi ya jamii kwa kuongeza ushirikina na uchawi hivyo kupelekea mauaji kila kona ya nchi!

Ukitizama nchi ya Nigeria ina matatizo mengi sana kwa kuwa inaruhusu uchifu kitu ambacho kinahamasisha matumiazi ya nguvu za giza!

Uchifu pia kwa sehemu kubwa utahamasisha ukabila na umaeneo kwa kuwa Chifu atataka awe mtawala wa jadi hata kama hatambuliki kisheria!

Uchifu pia huendana na matendo ya kafara na mazindiko ya kimila! Kitu kama hiki kitahamashisha mambo kama ya mauaji ya wenzetu wenye ualbino,uuzwaji wa viungo vya binadamu n.k

Nchi itakuwa chini ya shetani haswa kwa kuwa kama unavyoona sasa serkali haizungumzii hata watu kufanya ibada badala yake inasisitiza mambo ya uchifu!

Mauaji ya sasa ni kutokana na roho za kichwawi zinazodai kafara ya damu! Japo kwa macho ya kawaida wanasaikolojia wanadai ni ugumu wa maisha na mahusiano! Kitu amabacho sio kweli kwa kuwa maisha magumu watanzania hawa hawa wanayo miaka yote!! Kwa jicho la kiimani hii ni kwa kuwa mkuu wa nchi kajitwika uchifu na wachawi wanatumia hilo jina la uchifu kuomba damu za kafara na matokeo yake ndo haya ya kuuana ovyo!

Uchifu umeeneza sana uchawi kitu amabacho kiliwafanya watu wa kijijini miaka ya nyuma kutodiriki hata kujenga nyumba nzuri za bati kwa kuhifia kurogwa! Pia vijana wengi wamekufa kwa kurogwa na kutolewa kafara!

Moja ya sababu hata za wenzetu kwenye ualbino ilikuwa ni waganga wa kienyeji kuwadanganya watu kuwa ukipata kiungo cha mwenye ualbino utapata utajiri! Waganga wa kienyeji hawana tofauti na machifu! Maana uchifu ndo mkuu wa waganga wa kienyeji hivyo kuachiwa machifu kujimwayamwaya wanaweza kuleta zahama nchini!

Asanteni sana wadau!
 
Mama hakubaliki kabisa Magu. Leo atakuwepo Magu ila ameandaliwa mvua tangu juzi kitu kinapiga nonstop.

Screenshot_20220204-062301_Weather.jpg


picha ya chini ni siku ya mwisho kuwepo jua.

20220202_180644.jpg
 
Sasa hao wanigeria unaowasema na uchifu wao na huo uchawi uliousema na wewe ambae hauna machifu wala uchawi nani ameendelea, nani raia wake wana exposure, nani raia wake ni wajanja na matajiri...?...
 
Inawezekana Mama ameliona hili anataka kuturudisha kwenye utamaduni wetu wa KiAfrica aka back to our roots....labda anataka kuwarudisha kwenye dini na taratibu za babu zenu ambazo imezitelekeza na kulaanika mpaka leo tumekuwa masikini...
 
inawezekana Mama ameliona hili anataka kuturudisha kwenye utamaduni wetu wa KiAfrica aka back to our roots....labda anataka kuwarudisha kwenye dini na taratibu za babu zenu ambazo imezitelekeza na kulaanika mpaka leo tumekuwa masikini...
Nakuambia sisi tunaotoka jamii za kifugaji tunajua kuwa uchifu ni ndumba hakuna la maana hapo mzee! Saizi haya mambo yameshapungua sana kwenye jamii zetu saizi tunapeleka watoto kusalimia nyumbani halafu wanataka kuturudisha huko haiwezekani tukatae!
 
inawezekana Mama ameliona hili anataka kuturudisha kwenye utamaduni wetu wa KiAfrica aka back to our roots....labda anataka kuwarudisha kwenye dini na taratibu za babu zenu ambazo imezitelekeza na kulaanika mpaka leo tumekuwa masikini...
Uchief na maendeleo wapi wapi uchief ni uchawi na uchawi ni against maendeleo.
 
Ili upewe uchief ni lazima uwe gwiji yaani wachawi wote wa eneo husika wewe ndiwe mwamba wao yaani masta mwenyewe na Ili uwe masta ni lzm shetani akukubali yaani umemtolea Sana kafara ya damu za watu umeua watu wengi sana. Sasa mama anaturudisha kwenye ushirikina na uchawi zama hizi ambao miaka nenda umeshindwa kumsaidia mwafrika ikiwemo hata kuzuia asichukuliwe utumwani au kutawaliwa na mkoloni.
 
Mama anataka kurudisha kwenye ujima, zama za kuogopa kujenga nyumba utarogwa, usipeleke watoto kijijini watarogwa, usiage mtu kijijini utakula mzinga njiani, nk.
Watz walishatoka huko
 
M
Hakuna upotoshaji hapo.chief,mzee,wazee ni vyeo vikubwa sana kwenye giza upande wa pili.
Hao machief wanalipi la kutushauri kizazi cha sasa.
Museveni alirudisha Uchifu Nchini Uganda wapi ulisikia Uganda imegubikwa na Uchawi kuliko Tanzania?

Sijui umri wako lakini Uchifu hauna ubaya wowote.

Tupige Siasa safi tuache Fake news.
 
M
Museveni alirudisha Uchifu Nchini Uganda wapi ulisikia Uganda imegubikwa na Uchawi kuliko Tanzania?

Sijui umri wako lakini Uchifu hauna ubaya wowote.

Tupige Siasa safi tuache Fake news.
Una faida gani kwenye Jamii ya sasa
 
Back
Top Bottom