Uchawi wa macho ukoje na nini tiba yake?

Undava King

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2017
Posts
3,422
Reaction score
5,675
Uchawi wa macho a.k.a Evil eye ni aina ya uchawi unaotupiwa muhusika ukuue au kukutaabisha kupitia jicho la mchawi.

Mara nyingi uchawi huu ufanyika katika maeneo yenye umati mkubwa wa watu mfano magengeni, mikahawani, minadani, n.k

Uchawi huu ni Kijicho kwa maana ya wivu wa kichawi na roho mbaya kwa mtu asiye na hatia.

Unapokuwa ukila chakula na mchawi akakubaini kuwa unakula mbele yake ni kana kwamba unamtambia najua wewe uwezi nunua ndiyo maana wanitolea macho ebu angalia ninavyofaidi.

Sasa kukukomesha mchawi unuia kimoyomoyo kwa kunung'unika na ukukazia macho yake "ambayo ukiyatizama nikama yanakwambia nakuchukia kama kifo au kufa tu" papo hapo uchawi huu utoka ndani yake na kumdhuru yule aliyekusudiwa.

Zongo hili umkumba mchawi aliyeununua au mwenye kuumiliki kama vile arosto ya madawa ya kulevya mara anapoona mazingira ya uchawi wake hawezi jizuia kukuroga hata kama ni mwanaye wa kumzaa.

Pindi unaporogwa na haina hii ya uchawi uwezi chukua round ni dakika chache tu baada ya kumaliza kula, kunywa au kumeza funda la mate tiyari utaanza kuhisi hauko sawa, tumbo litakuuma mno au kuvurugika hapo hapo utahisi homa, kichefuchefu na ukiwa na bahati nzuri utatapika.

Kinachofuata hapo kama utakimbizwa hospitalini hakuna watakachobaini na badala yake itatuchukua masaa kadhaa tu ya siku au siku chache kukusahau kama uliwahi kuwepo.

UNAJILINDA VIPI

1. Kama wewe si mshirikina chukua tahadhari acha mazoea ya kula ovyo ovyo mbele za watu usiowafahamu au kwenye umati mkubwa.

2. Dadisi au tafuta taarifa toka kwa wenyeji wa maeneo husika ulipofikia juu ya tabia za kishirikina katika maeneo yao hasa ukiwa maeneo ya vijijini ambapo kwa asilimia kubwa uchawi huu umeenea.

3. Tembea na kijiwe kidogo mfukoni au ukiweke katika sikio lako la upande mmoja kama wanavyoegeshea penseli mafundi seremala, hii ni kinga dhidi ya uchawi huu.

4. Chomeka njiti moja au mbili za kuchokonolea meno (toothpick) katika nywele zako za kichwani kwa wale wenye nywele ndefu hakikisha haionekani, hii pia itakusaidia ukirushiwa uchawi huu wakati unafakamia msosi au kinywaji usidhurike.

5. Hakikisha kila unapokula hasa mgahawani tafuta sehemu inayokupa faragha kiasi cha kutoangaliwa sana na wapita njia.

6. Ukishajua unakula katika mazingira ambayo ni hatarishi, usikwepeshe macho au kuona aibu kuwasoma watu unaokula nao au wanaokutazama, mara kwa mara wakazie macho na wao wakikutazama hili hata kama ipo nia atapotezea atajua mlengwa ana machale au kishashtukia mchezo na nikimroga hapa atanijazia nzi.

7. Usimpe nafasi uliyebaini au kumuhisi ndiye kakuroga nafasi atoroke, muumbue na hamasisha watu walio karibu wamdhibiti asitoroke hata kama huna uwakika kumbuka wapo watakaokuja kumtetea watatoa na nondo za muhusika kuwa innocent na wengine wataenda mbali kiasi cha kukutajia muhusika (kumbuka wenyeji wanawajua fika wahusika isipokuwa wewe hapo uliyefika katika mazingira yao)

Ikitokea ukamfumbia macho mwanga utakufa wewe na kesho ataendelea kuua wengine, ila ukimtaitisha papo hapo, basi utapata msaada kwa wenyeji kumlazimisha akukorogee uji wa mahindi wa moto kwa kutumia mkono wake kama mwiko (hapo ndipo utajua kuwa uchawi upo)

Akishamaliza kuukoroga uji huo hapo hapo katika eneo la tukio utapewa unywe na baada ya sekunde tu utatapika vyote ulivyokula na ndiyo pona pona yako hiyo.

Kitakachokushangaza ni kuwa kile ulichokula pengine ni ugali na samaki, ulimtafuna minofu kabla ya kummeza ila hapa utamtapika mzima kabisa na ameoza ananuka balaa na ana funza wakutosha, itoshe kusema uchawi haufai na unatesa watu.

Uchawi huu umeenea sana maeneo ya kanda ya ziwa kule ukerewe na rorya na kaskazini huko uchagani, tanga na maeneo mengi tu hapa nchini, kikubwa nimekusanua tu hili uchukue tahadhari haijalishi unaamini au hauamini kama uchawi upo.
 
Umeeongea mengi sana ila yote uliyoyaongea utawasaidia wale wenye uwezo mdogo wa kufikiri, tukiweza mshida adui UMASIKINI haya yote uliyoyasema yatabaki kuwa hadithi.
Unaposema UMASIKINI ni sawa na kusema maisha duni au yasiyofaa.

Je, ushirikina si moja ya vitu vinavyopelekea maisha hayo duni kuwepo?

Unajua ni kaya ngapi kwa sababu ya uchawi kama huu ninaouzungumzia wamepoteza nguvu kazi za familia zao ambazo zingewatoa huko kwenye lindi la umasikini?

Je, ukijifanya hujui au umeelimika hiyo itafanya jamii yako iache uchawi?

Bila shaka ninachokifanya hapa nikusaidia jamii nzima igundue hizi mbinu na kuutokomeza uchawi maana nguvu ya uchawi ni siri zake, na jamii iliyoacha uchawi ni jamii yenye maendeleo.
 
Uchawi wa macho a.k.a Evil eye ni aina ya uchawi unaotupiwa muhusika ukuue au kukutaabisha kupitia jicho la mchawi.

Mara nyingi uchawi huu ufanyika katika maeneo yenye umati mkubwa wa watu mfano magengeni, mikahawani, minadani, n.k

Uchawi huu ni Kijicho kwa maana ya wivu wa kichawi na roho mbaya kwa mtu asiye na hatia.

Unapokuwa ukila chakula na mchawi akakubaini kuwa unakula mbele yake ni kana kwamba unamtambia najua wewe uwezi nunua ndiyo maana wanitolea macho ebu angalia ninavyofaidi.

Sasa kukukomesha mchawi unuia kimoyomoyo kwa kunung'unika na ukukazia macho yake "ambayo ukiyatizama nikama yanakwambia nakuchukia kama kifo au kufa tu" papo hapo uchawi huu utoka ndani yake na kumdhuru yule aliyekusudiwa.

Zongo hili umkumba mchawi aliyeununua au mwenye kuumiliki kama vile arosto ya madawa ya kulevya mara anapoona mazingira ya uchawi wake hawezi jizuia kukuroga hata kama ni mwanaye wa kumzaa.

Pindi unaporogwa na haina hii ya uchawi uwezi chukua round ni dakika chache tu baada ya kumaliza kula, kunywa au kumeza funda la mate tiyari utaanza kuhisi hauko sawa, tumbo litakuuma mno au kuvurugika hapo hapo utahisi homa, kichefuchefu na ukiwa na bahati nzuri utatapika.

Kinachofuata hapo kama utakimbizwa hospitalini hakuna watakachobaini na badala yake itatuchukua masaa kadhaa tu ya siku au siku chache kukusahau kama uliwahi kuwepo.

UNAJILINDA VIPI

1. Kama wewe si mshirikina chukua tahadhari acha mazoea ya kula ovyo ovyo mbele za watu usiowafahamu au kwenye umati mkubwa.

2. Dadisi au tafuta taarifa toka kwa wenyeji wa maeneo husika ulipofikia juu ya tabia za kishirikina katika maeneo yao hasa ukiwa maeneo ya vijijini ambapo kwa asilimia kubwa uchawi huu umeenea.

3. Tembea na kijiwe kidogo mfukoni au ukiweke katika sikio lako la upande mmoja kama wanavyoegeshea penseli mafundi seremala, hii ni kinga dhidi ya uchawi huu.

4. Chomeka njiti moja au mbili za kuchokonolea meno (toothpick) katika nywele zako za kichwani kwa wale wenye nywele ndefu hakikisha haionekani, hii pia itakusaidia ukirushiwa uchawi huu wakati unafakamia msosi au kinywaji usidhurike.

5. Hakikisha kila unapokula hasa mgahawani tafuta sehemu inayokupa faragha kiasi cha kutoangaliwa sana na wapita njia.

6. Ukishajua unakula katika mazingira ambayo ni hatarishi, usikwepeshe macho au kuona aibu kuwasoma watu unaokula nao au wanaokutazama, mara kwa mara wakazie macho na wao wakikutazama hili hata kama ipo nia atapotezea atajua mlengwa ana machale au kishashtukia mchezo na nikimroga hapa atanijazia nzi.

7. Usimpe nafasi uliyebaini au kumuhisi ndiye kakuroga nafasi atoroke, muumbue na hamasisha watu walio karibu wamdhibiti asitoroke hata kama huna uwakika kumbuka wapo watakaokuja kumtetea watatoa na nondo za muhusika kuwa innocent na wengine wataenda mbali kiasi cha kukutajia muhusika (kumbuka wenyeji wanawajua fika wahusika isipokuwa wewe hapo uliyefika katika mazingira yao)

Ikitokea ukamfumbia macho mwanga utakufa wewe na kesho ataendelea kuua wengine, ila ukimtaitisha papo hapo, basi utapata msaada kwa wenyeji kumlazimisha akukorogee uji wa mahindi wa moto kwa kutumia mkono wake kama mwiko (hapo ndipo utajua kuwa uchawi upo)

Akishamaliza kuukoroga uji huo hapo hapo katika eneo la tukio utapewa unywe na baada ya sekunde tu utatapika vyote ulivyokula na ndiyo pona pona yako hiyo.

Kitakachokushangaza ni kuwa kile ulichokula pengine ni ugali na samaki, ulimtafuna minofu kabla ya kummeza ila hapa utamtapika mzima kabisa na ameoza ananuka balaa na ana funza wakutosha, itoshe kusema uchawi haufai na unatesa watu.

Uchawi huu umeenea sana maeneo ya kanda ya ziwa kule ukerewe na rorya na kaskazini huko uchagani, tanga na maeneo mengi tu hapa nchini, kikubwa nimekusanua tu hili uchukue tahadhari haijalishi unaamini au hauamini kama uchawi upo.
Upo Sana arusha pia.
Ila mambo mengn acha alinde mungu tu huwezi fika eneo ukaanza kuuliza habari za uchawi😀😀
 
Back
Top Bottom