Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,601
- 729,485
Unaweza ukabisha kabisa na usiamini hata chembe lakini hili jambo lipo tena enzi na enzi
na haliishii kwa wanaume tu bali hata kwa wanawake na huku ni kuwafanya wanawake kuwa wagumba au kukosa watoto hata kama mimba ikitunga.
Baadhi ya waganga wa jadi ni watu hatari sana unaenda kwake kwa nia njema ya kupata tiba ya mwandani wako asirukeruke atulie kwako yeye anakutamani na kukupa dawa ya kwenda kuua nguvu za mwenzio (Kuweni makini sana mnaoenda kutafuta tiba za namna hii, si wote ni watu wema)
Lakini vile vile kuna hili la chuki ndani ya ndoa -kusema tukose wote, chuki mitaani, kijicho na rohombaya vyote hivi huweza kumfanya mtu akakufanyia kitu kibaya kama hicho.
Kingine cha kutisha zaidi ni hawahawa waganga wenyewe wanaotaka kujihakikishia ulaji wa kila siku na hata utajiri, mara nyingi watu wa jinsi hii huwapa wateja wao dawa za ziada nje ya matibabu ili zikamuumize mwenza wako na mwisho wa siku urudi kwake.
Katika hili hata wanawake kwa wanawake, mashoga mawifi majirani mama wakwe na hata ndugu hufanyiana sana haya mambo kwa sababu za kijinga mno.
Vyovyote vile iwavyo mwisho wa siku anayefaidi ni mganga na nyie kubaki mnaumizana kukomoana na kujengeana Chuki zisizoisha.