Uchawa wa Viongozi unatisha

Uchawa wa Viongozi unatisha

Hakika leo nimeamini kuwa Taifa hili tumefika hapa tulipo Kwa ajili ya unafiki na uchawa wa Viongozi ambao ndiyo washauri wa Rais kuwa waongo na watu wakujipendekeza tu kwenye mamlaka ya uteuzi.

Haiingii akilini eti kadogosa DG wa TRC anasema Rais SAMIA kawashinda Wajerumani katika ujenzi wa reli, wakati ukweli haupo hivyo.

Hata angekuwa anamsifu kwa kuanza Kwa SGR Watanzania tunajua kuwa wazo hili ni Hayati Magufuli na pia kuna uchakachuaji mkubwa wa mradi ule kwa Sasa mbali na kucheleweshwa kukamilika kwake kutokana na wizi unaoendelea.

Kadogosa acha kumdanganya Rais Samia, fanya kazi.

Action speaks louder than words
Na huyo Sa100 ambaye anafanywa kama ana akili kisoda unamchukuliaje? Kuacha kumpa lawama Sa100 inakufanye uwe mnafiki kama huyo mhuni wa TRC.
 
Jiwe ndo alianzisha huu ujinga kuwapendelea zaidi wanaomsifia sasa saivi imekuwa kama ugojwa bila mama kukemea kwa hakika ipo siku watasema Sa100 ndo ametuletea uhuru kutoka kwa mkoloni
Bora ata jiwe tuliona mabadiliko kidogo japo hii tamaduni ni ya kijinga na Jiwe alikosea na lawama apewe pia.
 
Hakika leo nimeamini kuwa Taifa hili tumefika hapa tulipo Kwa ajili ya unafiki na uchawa wa Viongozi ambao ndiyo washauri wa Rais kuwa waongo na watu wakujipendekeza tu kwenye mamlaka ya uteuzi.

Haiingii akilini eti kadogosa DG wa TRC anasema Rais SAMIA kawashinda Wajerumani katika ujenzi wa reli, wakati ukweli haupo hivyo.

Hata angekuwa anamsifu kwa kuanza Kwa SGR Watanzania tunajua kuwa wazo hili ni Hayati Magufuli na pia kuna uchakachuaji mkubwa wa mradi ule kwa Sasa mbali na kucheleweshwa kukamilika kwake kutokana na wizi unaoendelea.

Kadogosa acha kumdanganya Rais Samia, fanya kazi.

Action speaks louder than words
Kwa maoni yangu Rais Samia amewashinda Wajerumani kutokana na kutumia fursa ya ukuaji wa Technologia ambayo imewezesha Nchi sasa kujenga Reli ya Kisasa Standard Gauge Railways kwa kutumia mapato yetu ya ndani (Hata kama tumekopa)
 
Back
Top Bottom