Uchangiaji kwa ajili uzoaji taka

Wakulonga

JF-Expert Member
Oct 29, 2012
659
1,000
Habari wana JF
Naomba niende moja kwa moja kweny mada. Suala la usafi ni jambo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu kwani humuepusha na magonjwa mbali mbali. Kama ilivyo katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dsm watu huchangia kwa ajili ya uzoaji taka. Watu huchangia kwa gharama tofauti kulingana na sehemu husika. Kwa mfano kwetu tunatoa Tsh 5,000/- kwa mwezi kwa ajili uzoaji taka. Hilo mimi sina shaka nalo nimeridhika kabisa, wasiwasi wangu ni hii risiti niliopewa mbona haionyeshi hiyo shilingi elfu tano je ninaamini vp kweli fedha yangu inafika mahala husika au midomoni mwa watu? Wahusika kama mpo humu hebu rekebisheni ili mtuondoe shaka.
 

Attachments

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom