Uchambuzi: Wimbo wa WAAH! Diamond Ft Koffi Olomide..Toa maoni

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,622
2,835
Habari wana JF.
Tukiwa tunaelekea mwisho wa mwaka wasanii mbalimbali wameachia nyimbo zao.Wao wenyewe wanaziita za kufungia mwaka.

Mmoja kati ya wasanii walio achia wimbo ni Diamond Platnumz aliomshirikisha Koffi Olomide unaitwa WAAH!
Hadi sasa video ya wimbo huo imeachiwa ikiwa na wiki moja katika mtandao wa YOUTUBE imevuna watazamaji Milioni 9.8 na bado wanaendelea.

Wimbo huu umetokea kupendwa kwasababu kwanza ni ukubwa wa wasanii walioshirikiana yaani Diamond na Koffi Olomide.

Lakini pia aina ya muziki ni rhumba/sebene ni aina ya muziki unaopendwa sana Afrika. Hasa ukizingatia ukubwa wa lugha mbili ya Kilingala na Kiswahili.

Cha tatu ni mashairi yaliyotumika.Mashairi yaliyotumika ni ya yanayoeleweka haitampa MTU anayesikiliza wakati mgumu kuyaelewa. Ni tofauti na nyimbo za zenye mashairi mazito yenye kutafakari hizi husikilizwa na wachache walengwa.

Cha nne wimbo huu ni wa kuchezeka yaani kuanzia mwanzo hadi mwisho vionjo vilivyotumika ni vya kucheza hivyo umepokelewa kwa kasi kwasababu nyimbo zinazopendeka ni za kucheza kwa mfano Yope,Inama na nyinginezo.

Nimechambua tu kwanini wimbo huu umepata kuwa mkubwa na kuhit headlines hata kuvunja rekodi ya kuwa Wimbo wa Kwanza katika Youtube in Sub-Saharan Africa kufikisha views million 2 ndani ya muda mchache...

Sijatumia u timu wala ushabiki katika kuchambua nawasilisha .
 
Hamna kitu kinaitwa "mashairi" mle

Halafu hii sijui ipo kwenye genre gani haieleweki ni zuku, bolingo, bongo fleva, taarabu nk.
 
Bonge la wimbo, hii ni nyimbo yangu bora ya mwaka, ki ukweli Diamond, anapambana sana.
 
Rhumba mkuu..I feel like will,I feel am a prince and I feel my self.
Hamna kitu kinaitwa "mashairi" mle

Halafu hii sijui ipo kwenye genre gani haieleweki ni zuku, bolingo, bongo fleva, taarabu nk.
 
Binafsi ni shabiki wa Diamond....Ila huu wimbo ukiniambia ni wimbo wa Koffi nitakuelewa zaidi..alichofanya Diamond ni kununua wimbo wa Koffi na kuufanyia remix..

Wimbo mzima ni Koff tu.
Wimbo mzima ni koffi? acha uchawi dada, koffi kaimba kibwagizo tu halaf unasema wimbo mzima ni koffi? unatumia kiungo gani kusikiliza?
 
Back
Top Bottom