ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
Apps huwa zinatangulia kwenye iOS na nyingi za hali ya juu hubaki kwenye platfomu hii kwa muda mrefu na nyingine huishia kutopatikana kabisa katika platfomu ya Android, wachilia mbali kampuni zenye ushindani mdogo kwa sasa kwenye uwanja huu yaani Amazon, Blackberry OS na Windows Phone. Hapa tunazungumzia zaidi ubora wa apps kuliko idadi ya Apps. Kiidadi kuna taswira kwamba karibuni Android wataipita iOS kwa kuwa na idadi kubwa ya Apps.
Apple ni Kampuni ya Vifaa: Sababu ya kwanza inayopelekea Apple kupata apps nzuri ni kwamba Apple ni kampuni ya vifaa (hardware) kuliko software, Apple hutengeneza software kwa lengo la kuipa iOS ukamilifu lakini hailengi kupata faida kwenye Apps hizo kwa kiasi kikubwa, na hii ndio tofauti ya msingi kwani Microsoft na Google zote ni kampuni za programu (software) hivyo ni matarajio yao kupata faida kutoka kwenye biashara hii, ingawa kampuni mbili hizi zina mbinu tofauti katika kuingiza fedha.
Kwa hiyo wakati Apple wanauza simu na tablet ghali, wao ndio walioanzisha mtindo wa app kwa dola moja na unaweza kuweka kwenye gajeti zako hata kumi. Hivyo wao ndio waanzilishi wa mfumo wa kibiashara wa apps kuwa bei rahisi mno.
Kinyume na hali hii, watengeneza apps katika platfomu ya Windows Phone (wakati huo ikiwa Windows Mobile) walitengeneza na kuuza apps kwa gharama kubwa sana kwa mfano kampuni ya SPB iliuza apps za kawaida kabisa katika platfomu hii kwa dola 20 kwa leseni ya kutumia kwenye simu moja tu. hii ilipelekea biashara ya apps kutoshamiri kama ilivyo sasa.
Usimamizi wa hali ya Juu: Wakati Android imepanda mno kwa idadi ya programu (apps), nyingi kati ya programu zake ni zile zisizo na maana au zenye ubora wa hali ya chini. Hii inatokana na kutokuwa na usimamizi na uwekaji wa viwango mzuri.
Apple ina usimamizi na masharti ya hali ya juu kwa watengeneza programu, hivyo kunapatika ubora (quality) wa hali ya juu katika apps zao. Sera ya Android kwamba utaweza kuuza kwa ubora utakaouweka kwenye programu yako bila ya kuweka masharti na usimamizi umeifanya platfomu hiyo kuwa na "programu matakataka" nyingi mno.
App za Skrini ya Pili: Kuna apps ambazo zimezipatia simu na tableti jina la "second screen", hizi ni programu za chaneli na vipindi vya televisheni. Programu hizi kwa sasa ni kivutio kikubwa na nyingi zinapatikana kwenye iOS kuliko platfomu nyingine zote. Hii imetokea kuwa mkondo kwa vile wengi wameanzia na kuishia kwenye jukwa hili hili la iOS. Bila ya shaka Android na wapinzani wengine wameliona hili, huenda watalifanyia kazi. Ukitaka kufahamu uzuri wa programu za aina hii; chukulia mfano wa Skysports App ambayo inaonyesha Premier League, Bundesliga, La Liga, Serie A, Formula 1 na vipindi vingine muhimu vinavyovutia kwenye michezo, app hii inapatikana kwenye iOS na gajeti chache tu za Android, utendaji wake kazi (implementation) kwenye iOS ni wa hali ya juu, hasa kule kujumuishwa kwa opta stats kunakufanya uone kuna umuhimu wa kuwa na programu hii kwani kuna cha ziada ambacho hakipatikani kwenye televisheni moja kwa moja.
Kufunguliwa kwa Gajeti (Root): Huku ni kufunguliwa kwa bidhaa za Android na hivyo mtumiaji kuwa huru kufanya mambo mengine mwenyewe, athari kubwa ambayo inawakimbiza wenye apps za biashara kubwa ni kuwa gajeti zinapofanyiwa rooting watumiaji wanaweza kuweka programu za kulipia bila ya kulipa. Wakati root limeruhusiwa rasmi kwenye Android, Apple wako kwenye vita dhidi ya jailbreakers, huduma inayofanana na root ya Android. Kila baada ya muda mfupi Apple hutoa kizibo (patch) cha kuhakikisha kuwa jailbreak inapoteza uwezo. Ingawa hizi zimegeuka kuwa mbio za paka na panya wengi wamechoshwa na wanaendelea kuchoshwa na jailbreaking kwa sababu wakati mwengine inakuwacha uwe nyuma kwa matoleo ya iOS ili kusubiri jailbreak. Hivyo root na jailbreak ni furaha kwa baadhi watumiaji lakini ni msiba kwa watengenezaji wa programu wote (isipokuwa apps za bure)
Gajeti Kukosa Umoja (Windows Phone): Hili ni kosa jengine ambalo limefanywa na Microsoft. Tablet wamezipeleka kwenye Windows 8 OS na simu zimebaki peke yake kwenye Windows Phone OS. Ukizingatia idadi ndogo ya simu za Windows Phone (6% tu ya simu zote Duniani kwa mujibu wa ripoti ya Mintel Disemba 2012), hii inafanya watengeneza apps waone kuwa hakuna mauzo makubwa katika platfomu hii na hivyo haivutii sana. Laiti Microsoft wangepeleka tablet kwenye OS Windows Phone, soko lake lingevutia zaidi wateja na hivyo kulipa ukuaji na unyakuaji wa hisa mzuri zaidi.
Android imechelewa kutulia: Matoleo ya nyuma ya Android mpaka ufikia 2.3 Gingerbread ilikuwa si kwa ajili ya tableti. Toleo la Android Honeycomb likawa la tableti peke yake, kuanzia toleo la Icecream Sandwich ndio Android imeanza kujumuisha tableti na simu kama platfomu moja. Hii imewachukua muda mrefu sana kuifikia, kosa hili halikufanywa na Apple walipoanza tu kutoa tableti basi moja kwa moja iOS ilianza kufanya kazi kwenye simu na tableti kama OS moja na kutoa maelekezo makini kabisa juu ya nini watengeneza apps wafanye ili kuwezesha apps zao kufanya kazi kwenye iPad ya kwanza mwaka 2010.
Windows Phone imechelewa Kutoka: Yaani ni vigumu kuamini kwamba Windows Phone imewachukua muda mrefu sana kuweza kutulia kwenye utaratibu wa kisasa baada ya kuachana na Windows Mobile iliyofeli baada ya kutoka kwa iOS na Android. Microsoft walikuwa mchezoni kwa muda mrefu sana lakini walizembea kuuona ukweli mwaka 2007 wakati iPhone inaingia sokoni. Sasa hivi wana mlima mrefu sana wa kupanda kuzifikia Android na iOS. Pia mkakati wa kuipeleka tableti kwenye OS kamili huenda ukaiangusha Microsoft au huenda ukaipa faida, kwa kifupi hapa Microsoft wamecheza kamari na hawajui matokeo yatakuwa je.
Utulivu (Stability): Hii ndio sifa ya iOS tangu toleo la kwanza, Apple wanaonekana wanajua nini wanafanya na wapinzani wamo kurekebisha makosa, moja baada ya jengine, badala ya tu kulenga kwenye uboreshwaji kama wanavyofanya Apple. Matokeo yake iOS imejichukulia sifa ya kuwa platfomu ya uhakika na ya kitaalamu (professional), kwa hiyo wenye apps ambazo za maana hutanguliza apps zao kwenye iOS kisha baada ya kuuza na kupata faida ndio huangalia uwezekano wa kwenda kwengine.
Gajeti kukosa umoja (Android):
Ukitengeneza apps za iOS kwa ajili ya simu na tableti basi una hakika itafanya kazi kwenye kila kifaa cha iOS iwe ni iPhone iPad Mini au iPod Touch. Hii si hali katika Android, inabidi programu yako uijaribu na uifanyie marekebisho ili ifanye kazi kwa ufanisi na bidhaa zenye ukubwa wa 3", 3.5", 4", 4.2", 4.5", 4.8", 5" 5.5" 6" 7", 8' na kadhalika na msururu ni mrefu. Ndio utaona app ipo kwenye Play Store lakini haikubali kuinstall kwenye baadhi ya simu au tableti kwa vile haikutengezwa kuwa na ufanisi katika gajeti yenye ukubwa huo. Hii huwapa kazi ngumu na ya ziada watengeneza apps wa Android.
Wakati umefika wa Google kuifanyia marekebisho Android katika suala la Apps ili waweze kutoa ushindani wa ubora (quality) katika apps na sio idadi tu.
Chanzo: gajetek habari: Uchambuzi: Sababu za Apple Kutamba Kwa Apps