Uchambuzi wangu juu ya Mabadiliko ya Baraza la Mawaziri

Nawasalimu kwa Jina la JMT

Leo napenda kutoa uchambuzi wangu kidogo juu ya Mabadiliko ya Baraza la Mawaziri

Kwa Mawaziri
Kwanza napenda kusema Mama hajafanya vibaya! Mawaziri ni wasimamizi wa Sera ana haki ya kuweka yeyote amtakaye.

Malalamiko kadhaa yamesikika juu ya watu hawa
1. Mchengerwa kutolewa utumishi

Hapa inaonekana watumishi wengi walimpenda na kumkubali sana mchengerwa. Mimi sio mtumishi wa umma ila kiukweli hata mimi niliona jamaa ametosha pale. Sijui nini kimemfanya Rais amtoe Ila naamini kama Samia ameona reaction ya watumishi atafikiri upya Kama hakukuwa na ulazima wa kumtoa pale

2. Kuondolewa Lukuvi
Kusema kweli Mimi sijawai kuwa mfuasi wa Lukuvi na ukiniuliza Kwa nini nitakwambia kwa miaka yote aliyokaa Lukuvi ardhi nilichokuwa nakuona ni ongezeko la makazi holela kila siku. Bora uholela ungekuwepo kwenye makazi ya zamani na sio maeneo mapya ila mfano kwa Dar tu, Hadi maeneo mapya ya chanika, goba, madale, kibamba uholela unazidi kukua kila siku wakati Wizara ipo na wanaweza kutumia hata wanafunzi wa vyuo vya ardhi katika kupima na kupanga makazi ila kwake huo ubunifu sikuwai uona. Mikoa yote Tanzania ni uholela tu wa makazi! Nilimuona kwenye vyombo vya Habari tu akitoa matamko na si lolote lingine. Kwenye hili nasema Mama yuko sahihi.

3. Jaffo kuendelea kuwa Waziri
kama ilivyo Kwa Lukuvi, nimeona Jaffo nae bado yupo kwenye baraza. Kwangu Mimi Jaffo alifeli kwenye mazingira. Mwaka 2019 tulipitisha Sheria kuzuia mifuko ya plastiki ila kwenye hili Jaffo amefeli big time. Kuna uzi niliandika humu kumshauri Makamu wa Rais kuzunguka kwenye vibanda vya chips Dar na Dodoma aone kwa Jinsi gani mifuko ya plastiki imerudi kwenye hadi kufungia chips. Jaffo alifeli kwenye Mazingira hivyo hakustahili kurudi. Naamini Mama Samia ataendelea kuliangalia hili

4. Kabudi na Kitila
Najua Rais ana utashi wake Ila Kwa kumuondoa Prof Kitila naweza kusema kuwa hajakosea! Sikuona ubunifu wowote kwa kitila kwa alivyokuwa Biashara na hata Uwekezaji. Ni mtu wa maneno mengi tu

Kwa Kabudi nikiri huyu mzee uwezo anao Ila naona kama alikata tamaa kufanya kazi baada ya kifo cha JPM. Naona pia mama yuko sahihi. Naamini anaweza kunfikiria badae

5. Ridhiwani na Nape
Kwa hawa wote maneno yamesemwa kumgusa JK kuwa ndo sababu ya wao kuteuliwa. Kwa hawa naweza kusema sioni Tatizo kwao. Nape ni mtendaji mzuri sana. Alionekana alivyokuwa Wizara ya habari Mara ya mwisho. Ridhiwani watu wanakosea kumjudge mapema. Ni mpya kabisa kwenye Baraza. Sioni Tatizo kwake zaidi ya maneno ya kutunga ya watanzania yanayoongozwa na chuki tu. Huyu awe judged Kwa utendaji wake atakaouonesha pale Ardhi.

Mwisho kwenye Baraza la Mawaziri napenda kukiri kusikitika kutokuwepo kwa Charles Kimei- Sijui Mama anamuwazia nini Ila Kwa mafanikio ya huyu mtu akiwa crdb ninaona ni mtu muhimu sana kuwepo kwenye wa shauri wa Mama Samia kwenye cabinet

Dr Charles Kimei namfanisha na watu wenye weredi na u smart wa kupekee kama Prof Luoga, Nehemia Mchechu, Prof Chamuliro, Prof Mchome, Kanali Simbakalia ambao wana uwezo mkubwa sana wa kiakili hivyo hawana budi kuwa washauri wa Karibu wa Mamlaka.

Nataka na napenda sana Mama Samia afanikiwe. Ameanza vizuri na anakwenda vizuri. Napenda sana azidi kufanikiwa zaidi. Natumai Kwa sehemu chache nilizoshauri atazingatia humu.
Hamna lolote hatuwezi kum rate SSH kwa MIEZI michache hii. Tayari VIASHIRIA vya UDINI, na NEPOTISM vinaonekana WAZI unless otherwise wewe ni MFAIDIKA!
 
Baraza la mawaziri limejaa waislamu utadhani kamati ya msikiti wa ijumaa.
Huyo maza mdini sana
 
Kimei hapana. Ni mkabila wa saaana
Crdb ndo Bank pekee ya kitanzania na Tanzania iliyofungua tawi nje ya Tanzania na haya yalifanyika chini ya Kimei.

Kama alikuwa na uwezo mpaka wa kufanya makubwa kiasi kile ni vizuri tukaendelea kumtumia sasa Kwa manufaa ya Nchi
 
Hamna lolote hatuwezi kum rate SSH kwa MIEZI michache hii. Tayari VIASHIRIA vya UDINI, na NEPOTISM vinaonekana WAZI unless otherwise wewe ni MFAIDIKA!
Samia hana u dini. Hapo umekosea sana! Kati wa viongozi hapa Tanzania ambao sio wadini Samia anaweza akawepo top 3
 
Baraza la mawaziri limejaa waislamu utadhani kamati ya msikiti wa ijumaa.
Huyo maza mdini sana
Mbona teuzi anazoteua wakristo wenzetu hamusemi? Kwani Baraza lina Waislamu wangapi na wakristo wangapi?

Acha udini!
 
5. Ridhiwani na Nape
Kwa hawa wote maneno yamesemwa kumgusa JK kuwa ndo sababu ya wao kuteuliwa. Kwa hawa naweza kusema sioni Tatizo kwao. Nape ni mtendaji mzuri sana. Alionekana alivyokuwa Wizara ya habari Mara ya mwisho. Ridhiwani watu wanakosea kumjudge mapema. Ni mpya kabisa kwenye Baraza. Sioni Tatizo kwake zaidi ya maneno ya kutunga ya watanzania yanayoongozwa na chuki tu. Huyu awe judged Kwa utendaji wake atakaouonesha pale Ardhi.
Suala la uadilifu kwenye mali ya umma sio kigezo kwenye hiz teuzi?
Mbona umeongelea upande mmoja tu wa utendaji la maadili umeweka kando?
 
Samia hana u dini. Hapo umekosea sana! Kati wa viongozi hapa Tanzania ambao sio wadini Samia anaweza akawepo top 3
Alupoingia unajua alifanya nini ktk walinzi wake?
Akatuletea wamama wenye vishungi. Sina tarizo na vishungi vya Dini zai kama wangekuwa Zanzibar. Ikaleta manung'uniko kuwa Rais akiienda nje ya nchi hasa Marekani nk. Tanzania itaonwkana kwamba Waislamu ni 100% wakati wao ni aslimia 30% Na ushee. Akaambiwa vaa wewe lakini hawa walinzi wako Waislam wafunge vitambaa. Ndo hapo huzioni tena shungi.
 
Suala la uadilifu kwenye mali ya umma sio kigezo kwenye hiz teuzi?
Mbona umeongelea upande mmoja tu wa utendaji la maadili umeweka kando?
Ridhiwani ana shida gani kwenye uadilifu? Tupe hoja na ushahidi pia hapa
 
Alupoingia unajua alifanya nini ktk walinzi wake?
Akatuletea wamama wenye vishungi. Sina tarizo na vishungi vya Dini zai kama wangekuwa Zanzibar. Ikaleta manung'uniko kuwa Rais akiienda nje ya nchi hasa Marekani nk. Tanzania itaonwkana kwamba Waislamu ni 100% wakati wao ni aslimia 30% Na ushee. Akaambiwa vaa wewe lakini hawa walinzi wako Waislam wafunge vitambaa. Ndo hapo huzioni tena shungi.
Wewe mtu akivaa ushungi kipi kinakukera?

Mbona wanawake wa kiyahudi Nao wanafunika nywele zao? Shida yako nini?
 
Kuna kipi nimeongea juu ya Lukuvi cha uongo?
tumsubiri huyo msoga wako tuone kama makazi holela hayataendelea ili tuje kukusuta humu ndani.hiyo wizara ina changamoto nyingi na si wizara ya kufantiwa majaribio kwa akina ridhiwani.inahitaji uthubutu na watu jasiri na wenye ukomavu wa kiakili na busara.
 
Back
Top Bottom