Uchambuzi wa tatizo katika mradi (Project Analysis)

Jul 3, 2016
19
13
Ni matumaini yetu kwamba nyote mu-wazima jukwaani hapa, na mnaendelea vyema na majukumu ya kitaifa.
Leo tungelipenda ku-share nanyi juu ya uchambuzi wa tatizo katika mradi wa maendeleo ya kijamii (Problem analysis)

Uchambuzi wa tatizo ni moja miongoni mwa vipengele katika uchambuzi wa hali/mazingira katika mradi (situational analysis). Vipengele vingine katika uchambuzi wa hali/mazingira hujumuisha utathmini wa hitajio (need assesment) na uchambuzi wa wadau ((stakeholders' analysis)

Hatua hii hufuata baada ya shughuli ya tathmini ya hitajio (need assessment) kuwa imefanyika, taarifa zipatikanazo baada ya kufanyika kwa tathmini ya hitajio hutumika katika kung'amua mzizi halisi wa tatizo linaloikabili jamii husika. Ifahamike kwamba, asili ya tatizo inapojulikana basi hurahisisha mchakato mzima wa uibuaji wa mradi. Hatua hii ni muhimu sana na huzingatiwa kama kigezo katika uibuaji wa miradi inayofadhiliwa na mashirika mfano Umoja wa Mataifa (UN), UNDP na wadau wengine wa maendeleo.

Uchambuzi wa tatizo katika uibuaji wa mradi hujumuisha vipengele vikuu vitatu, navyo ni:

  1. Tatizo lenyewe, hii ni hali hasi (negative situation) yenye kuathiri ustawi mzima wa jamii na mtu mmoja mmoja pia katika nyanja za kiuchumi, kijamii, kimazingira n.k. Mfano kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI, uchafuzi wa mazingira n.k, hizi ni hali ambazo hukwamisha ustawi wa jamii hivyo huchukuliwa kama ni matatizo ambayo miradi hupaswa kuja na majibu.
  2. Chanzo cha tatizo, hii hujumuisha mambo (factors) ambayo hutokea katika jamii, taasisi na hata nchi pia, ambayo huchochea uwepo wa tatizo husika. Mambo haya huweza kuwa katika hali za kitabia (behaviour), mitazamo (attitudes) n.k. Vyanzo vya tatizo hugawanyika katika sehemu mbili nazo ni:
    1. Chanzo cha juu juu (underlying cause), hichi ni chanzo ambacho huonekana mapema wakati wa uchambuzi wa matatizo, japo kiasili si chanzo haswa cha tatizo. Na hapa ndipo wabunifu wengi wa miradi hukosea, huchulia vyanzo hivi kama ndio vyanzo haswa vya tatizo na hatimaye kuja na mradi ambao baada ya utekelezaji wake, tatizo bado huendelea kuonekana. Mfano tatizo la kuongezeka kwa idadi ya watu wanaougua ugonjwa wa malaria, kutopatikana kwa vyandarua na madawa ya kutosha huweza kuonekana kama ndio chanzo halisi cha tatizo, japo kiuhalisia hichi si chanzo. (root cause)
    2. Chanzo halisi (root cause), hichi ni chanzo ambacho mara nyingi hakionekani kwa urahisi, kuonekana kwake yabidi ufanyike uchambuzi makini. Mfano kwa tatizo la ongezeko la idadi ya watu wauguao ugonjwa wa malaria, kiuhalisia chanzo chake ni uwepo wa mbu waenezao ugonjwa huo. Hivyo ili kutatua tatizo yapaswa kuja na mradi ambao utatokomeza mazalia ya mbu, na si kuja na mradi wa kugawa vyandarua na dawa.
  3. Madhara (consequence), hii hujumuisha hali ya kiuchumi, kijamii, kisiasa, kimazingira na hata kitamaduni ambayo husababishwa na uwepo wa tatizo. Mfano kwa tatizo la ongezeko la watu wauguao ugonjwa wa malaria, madhara huweza kuwa vifo, kuongeza utegemezi katika familia n.k

NAMNA YA KUCHAMBUA TATIZO (HOW TO ANALYSE PROBLEM)

Kuna njia mbalimbali ambazo hutumika katika kuchambua tatizo, njia hizo hujumuisha mti wa mfupa wa samaki (fish bone tree) na mti wa matatizo (problem tree). Mti wa matatizo ni njia maarufu ya uchambuazi wa tatizo,msingi mkubwa katika uchambuzi wa tatizo ni uulizwaji wa swali "Kwanini?" baada ya tatizo halisi kujulikana, wadau watapaswa kuliainisha tatizo halisi kisha kujiuliza ni kwanini linatokea. Utaratibu wa kuuliza "Kwanini?" kuwapo kwa tatizo unapaswa kuwa wa kimantiki (logical sequence), mbali na hivyo hirakia (hierarchy) inapaswa kuzingatiwa pia.

Mchakato wa uchambuzi wa tatizo unapaswa ushirikishe wadau wa mradi hasa wale wenye kuathirika kwa kiwango kikubwa kutokana na uwepo wa tatizo husika, hii ni kwa sababu, watu hawa wana ufahamu sahihi juu ya tatizo na madhara yake pia.Pindi tatizo halisi linapokuwa limeainishwa kiustadi, ndipo mradi huibuliwa ili kuleta hali chanya ambayo itaondoa tatizo husika. Kimsingi mchakato huu utaweza kuainisha vyanzo vingi vya tatizo (root causes), uamuzi juu ya tatizo lipi lichukuliwe na lipi liachwe katika uibuaji wa mradi itategemea na kiasi cha rasilimali za taasisi husika pia makubaliano ya wadau washiriki wa mchakato (stakeholders)

Ni imani yetu kwamba tulichokusudia kukifikisha l kimeeleweka.

Ahsanteni

Kwa huduma za:
-Maandiko ya miradi ya maendeleo (project proposals)
-Maandiko ya mipango ya biashara (business plans)
-Semina katika maeneo ya Uibuaji na usimamiaji wa miradi (Project Planning and Management)
-Semina katika uendelezaji na mbinu za kibiashara (Business development and strategies)


Usisite kututafuta kwa namba 0719 518367, 0783 695639, 0657 935110
E-mail platinumconsultancy74@gmail.com

MUHIMU: KUTOKANA NA MAKOSA YA UCHAPAJI KICHWA CHA HABARI KWA LUGHA YA KIGENI KISOMEKE "PROBLEM ANALYSIS" NA SI PROJECT ANALYSIS KAMA ILIVYOANDIKWA.

Samahani kwa usumbufu.
 
Kumbe project analysis kiswahili chake ni uchambuzi wa tatizo katika mradi?
 
Certainly applicable.....just go guys; huduma hizi zinahitajika sana...Watanzania tutumie huduma hizi kwa miradi yenye mafanikio hata kabla ya haijaanza.
 
Back
Top Bottom