Uchambuzi wa sakata la Mohammed Damaro Camara

Uchambuzi wa sakata la Mohammed Damaro Camara

Lazima mchezaji apate uthibitisho wa maandishi kutoka FIFA kuhamishwa kutoka shirikisho moja kwenda lingine. Ni LAZIMA, otherwise mchakato unakuwa batili.
Sasa kwa Damaro uhamiaji ndiyo wamembadili uraia tangu akiwa Singida black stars, hivyo wenye makosa ni nani kwa kesi hiyo?
 
Sasa kwa Damaro uhamiaji ndiyo wamembadili uraia tangu akiwa Singida black stars, hivyo wenye makosa ni nani kwa kesi hiyo?
Mchezaji anatakiwa
1. Kuwa raia na kutokana na taarifa za uhamiaji ni raia wa Tanzania
2. Mchezaji anatakiwa kulihama shilika la mpira la awali yaani GFF na kuwa chini ya mamlaka ya TFF

Kigezo Cha kwanza Yanga hakiwahusu:
Kigezo Cha pili Yanga kinawahusu walitakiwa wahakikishe ACT yake inahamishiwa TFF:

Kibu Denis
Kibu hakuwahi kucheza mpira Kongo hivyo Shirika la mpira la Kongo halikumtambua:

Kibu alianza kucheza mpira Tanzania akimilikiwa na TFF ila hakuwa raia:
Hivyo alihitaji uraia wa Tanzania tu:
 
FIFA inatoa uraia?
Fifa inatengeneza sheria za mpira, kwa kifupi mmezoea kujificha chini ya kivuli cha serikali na ccm ila swala likifika fifa hawaangalii serikali wala ccm ndio maana kuna swali simba wameuliza kuhusu uadilifu wa TFF
 
Nigeria walitaka waende Kombe la Dunia kwa maandiko uliyoaandika faili lao limetupwa nje...
Mkuu umezungumzia uzawa ingawaje raia anaweza kuwa sio wa kuzaliwa na pia passport sasa hivi unaweza kutoa bila namba ya NIDA sio?
Swala la Nigeria na hili ni tofauti, pamoja na kupata uraia kuna taratibu zinatakiwa kufatwa ikiwemo kuhamishwa shirikisho la mpira.
Wanachozungumzia Simba ni kama taratibu zilifatwa na sio kuhoji serikali walimpaje uraia kama ingekuwa swala la uraia wangeulizwa Uhamiaji na serikali.
 
Lazima mchezaji apate uthibitisho wa maandishi kutoka FIFA kuhamishwa kutoka shirikisho moja kwenda lingine. Ni LAZIMA, otherwise mchakato unakuwa batili.
Achana nao kanuni na sheria za FIFA zinasema passport pekee sio kigezo bado mtu anabisha na kuendelea kuropoka
 
andiko hili limedadavuliwa kutoka kwenye andiko cha mchambuzi nguli wa michezo Tanzania ORUMA
Simba SC wanaandaa barua rasmi kwa TFF (Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania) kupinga uhalali wa mchezaji Mohammed Damaro Camara kutumiwa kama mchezaji mzawa badala ya mchezaji wa kigeni.

HOJA KUU ZA SIMBA SC

1. Suala la Passport
Simba wanadai taratibu za nchi zimekiukwa wakati Camara alipopewa Passport ya Tanzania
Kumiliki passport peke yake hakutoshi kumfanya mchezaji awe mzawa kwa mujibu wa kanuni za FIFA
2. Kanuni za FIFA Kuhusu Kubadilisha Shirikisho (Change of Association)
Kwa mujibu wa FIFA Regulations on the Status and Transfer of Players, mchezaji anapaswa:
✅
Kupeleka maombi rasmi FIFA ya kubadilisha Member Association
✅
Kusubiri uthibitisho wa maandishi kutoka FIFA
✅
Kupata kibali kabla ya kucheza
❌
Simba wanadai hatua hizi hazikufuatwa

USHAHIDI WA ZIADA - KESI YA JOSEPHAT ARTHUR BADA
Hii ndiyo hoja yenye nguvu sana:
Mchezaji Josephat Arthur Bada (ambaye pia alipewa Passport ya Tanzania kama Camara) alitumia Passport yake ya Ivory Coast (si ya Tanzania) wakati alipokuja Tanzania kwa mechi ya JS Kabylie vs Yanga katika mashindano ya Afrika.
Hii inamaanisha:
Kama Bada kweli angekuwa raia wa Tanzania, angetumia passport ya Tanzania
Kutumia passport ya Ivory Coast kunaonyesha uraia wa Tanzania unaweza kuwa wa mashaka
Inatoa mfano wa moja kwa moja kuhusu jinsi passport za Tanzania zinavyoweza kutolewa kwa njia zisizo halali

ATHARI ZINAZOWEZEKANA
Kama madai ya Simba yatathibitishwa:
Kwa Klabu inayomiliki Camara (inawezekana Yanga SC au klabu nyingine):
Kupoteza pointi za mechi zote alizocheza
Faini kubwa kutoka TFF na huenda FIFA
Kupunguziwa pointi au adhabu nyingine
Kwa TFF:
Uchunguzi wa FIFA kuhusu uadilifu
Vikwazo vinavyowezekana kutoka FIFA
Aibu ya kimataifa
Kwa Mpira wa Tanzania:
Uadilifu wa ligi utakuwa mashakani
FIFA inaweza kuingilia kati

MTAZAMO WA KISHERIA (FIFA Regulations)
Kifungu muhimu ni Annexe 1 ya FIFA RSTP kinachosema:
Mchezaji ambaye ana uraia wa nchi zaidi ya moja na ameshacheza kwa timu ya taifa ya nchi moja, anaweza kubadilisha tu kwa masharti maalum ya FIFA - si kwa kupata passport tu.
Pia Article 5 ya FIFA RSTP inasisitiza kwamba:
Mchezaji anapaswa kusajiliwa na Member Association moja tu kwa wakati mmoja, na uhamisho kati ya associations lazima ufuate taratibu rasmi.

HITIMISHO
Sakata hili ni kubwa na linaweza kuwa na athari za muda mrefu kwa mpira wa Tanzania. Kama FIFA itafungua uchunguzi, matokeo yanaweza kuwa makubwa sana kwa wadau wote waliohusika. Suala la msingi ni kwamba passport si sawa na eligibility ya kucheza mpira - hizi ni taratibu mbili tofauti kabisa.
5 - 0
 
Fifa inatengeneza sheria za mpira, kwa kifupi mmezoea kujificha chini ya kivuli cha serikali na ccm ila swala likifika fifa hawaangalii serikali wala ccm ndio maana kuna swali simba wameuliza kuhusu uadilifu wa TFF
Una uhakika wale wachezaji wanaotoka England wanaochezea Taifa stars wana passport ya Tanzania?
 
Achana nao kanuni na sheria za FIFA zinasema passport pekee sio kigezo bado mtu anabisha na kuendelea kuropoka
Ikifika mechi na Yanga ndio mambo ya uraia yana anza hiki ni kichaka kina andaliwa baada kipigo cha Saba, Damaro kacheza Singida na walikutana na Simba akiwa na huo uraia mbona haikua kesi?
 
Lazima mchezaji apate uthibitisho wa maandishi kutoka FIFA kuhamishwa kutoka shirikisho moja kwenda lingine. Ni LAZIMA, otherwise mchakato unakuwa batili.
FIFA anatoa wapi uthimbitisho kama sio mamulaka za serikali na hao ndio waliwapa uraia?
 
Subiri kwanza tarehe 1 march unyooshwe vizuri na damaro ili upate ushahidi wa kushtaki vzr
 
Mchezaji anatakiwa
1. Kuwa raia na kutokana na taarifa za uhamiaji ni raia wa Tanzania
2. Mchezaji anatakiwa kulihama shilika la mpira la awali yaani GFF na kuwa chini ya mamlaka ya TFF

Kigezo Cha kwanza Yanga hakiwahusu:
Kigezo Cha pili Yanga kinawahusu walitakiwa wahakikishe ACT yake inahamishiwa TFF:

Kibu Denis
Kibu hakuwahi kucheza mpira Kongo hivyo Shirika la mpira la Kongo halikumtambua:

Kibu alianza kucheza mpira Tanzania akimilikiwa na TFF ila hakuwa raia:
Hivyo alihitaji uraia wa Tanzania tu:

Yanga wamemsajili Damaro kutoka Singida black stars ( usajili wa ndani) hivyo haja ya ACT inatokea wapi? Sheria ipi hiyo inayosema kuwa mchezaji akiwa wa kigeni hata kama anachezea ndani anatakiwa kuwa ACT?

Yanga hakuna wanapowajibika katika hili kwasababu
1) mchezaji kapewa uraia akiwa yupo Singida
2) ni usajili wa ndani ambao uraia wa mchezaji ulishabarikiwa na mamlaka kabla hata ya kusajiliwa Yanga ( hakuitaji ACT)
 
Kitu ambacho nmegundua viongozi wa Simba ikifika mechi na Yanga wana anzisha vijisababu vya kijinga jinga kuwa andaa mashabiki kiakili endapo watapoteza mechi visingizio viwe kuonewa, tangu lini vilabu vikahusika na utoaji wa uraia na kwanini Damaro tu wakati uraia ulitolewa kwa wachezaji zaidi ya watatu na bado wapo Tanzania wanacheza?
kitu kingine Simba wanawahujumu Yanga mapato kwa kuanzisha hizo drama ili mashabiki wasijae uwanjani,
Fuatilia vizuri mkuu mmoja wa hao unaosema ni bada hayuko Tanzania na uko anakocheza hakutumia passport ya Tanzania
 
Sasa kwa Damaro uhamiaji ndiyo wamembadili uraia tangu akiwa Singida black stars, hivyo wenye makosa ni nani kwa kesi hiyo?
Kiongozi unatakiwa kuelewa hapa anazungumziwa mchezaji ambae kabadili uraia FIFA je wametoa uthibitisho kuwa huyo mchezaji ni raia wetu kimichezo?
 
Yanga wamemsajili Damaro kutoka Singida black stars ( usajili wa ndani) hivyo haja ya ACT inatokea wapi? Sheria ipi hiyo inayosema kuwa mchezaji akiwa wa kigeni hata kama anachezea ndani anatakiwa kuwa ACT?

Yanga hakuna wanapowajibika katika hili kwasababu
1) mchezaji kapewa uraia akiwa yupo Singida
2) ni usajili wa ndani ambao uraia wa mchezaji ulishabarikiwa na mamlaka kabla hata ya kusajiliwa Yanga ( hakuitaji ACT)
Gentleman, moja ya jukumu la Yanga ilikuwa ni kuthibitisha uraia wake kupitia taarifa za FIFA ili aruhusiwe kusajiliwa kama mchezaji mzawa jambo ambalo halikufanyika.

Ishu kubwa ni kwamba mchezaji alishawahi kuitumikia timu ya vijana ya Guinea hivyo anatambulika chini ya shirikisho la Guinea.

Ili kumhamishia TFF ni lazima FIFA wahusishwe na watoe 'Release letter' baada ya wao kujiridhisha, mfano Brahim Diaz kutoka Spain kwenda Morocco.

Kosa lipo, na sio kama Yanga hawajui. Ni vile mpira wetu unaongozwa na busara
 
Kiongozi unatakiwa kuelewa hapa anazungumziwa mchezaji ambae kabadili uraia FIFA je wametoa uthibitisho kuwa huyo mchezaji ni raia wetu kimichezo?
Tatizo kuna vitu mnachanganya, kuna uraia wa nchi na uraia wa kimpira.

Damaro kapewa uraia wa Tanzania tokea akiwa Singida, Anatumia "Uraia wa Nchi". TFF inamruhusu acheze kama mzawa kwa sababu ana pasipoti ya Tanzania, Hapa hakuna pingamizi FIFA kwa sababu ni mambo ya ndani ya nchi.
Ila hawezi kuchezea timu ya taifa ya Tanzania kwasababu haijabadilisha uraia kimpira na ili abadili uraia kimpira hapi ndipo taratibu za FIFA zinapokuja.

chilonge pitia hapa na mleta uzi rodrick alexander
 
Fuatilia vizuri mkuu mmoja wa hao unaosema ni bada hayuko Tanzania na uko anakocheza hakutumia passport ya Tanzania
Keyekhe yupo Singida hata leo yupo kwenye line up Vs Mtibwa, by the way huu uraia ulitoewa mwaka jana kabla ligi haija anza mbona hakukua na Kelele
 
Lazima aombewe/aombe na FIFA watafanya mawasiliano na mashirikisho yote mawili.
FIFA kazi yao ni kuthibitisha kama document zipo sawa pia kama mchezaji amekidhi vigezo habari za uraia ni swala la serikali
 
Back
Top Bottom