Leo nimefurahishwa Lissu kaongea huku ametulia tena kawa mpole, naona keshasoma upepo.
Katika hotuba yake naomba nichambue kidogo maelezo yake, kimsingi hayo aliyoyaelezea yaliwahi kutekelezwa na awamu zilizopita na yakashindikana, ni maneno yakuombea kura tu sio yakiutekelezaji.
1. Kuhusu fao la kujitoa, zipo changamoto za kiutendaji hasa uwezo wa mifuko yenyewe hivyo anaposema mtu ukipugwa tu ukachukue fedha zako. Labda angetueleza kiwango cha labour turnover kikoje, kama wanao acha kazi ni wengi kuliko wanao ajiriwa basi itakuwa pyramid financing, itafika sehemu ita collapse yenyewe. Kwanza tuangalie kwanini kijana afanyekazi miaka kumi halafu apoteze ajira yake na iwe mwisho wa tumaini lake kimaisha, tatizo ni nini? Kinacho mfanya asifanye kazi hadi uzeeni ni nini tunapaswa kuangalia "job security" ya watumishi wetu na sio kukimbilia kuwapa fedha ili wakafie mbele. Kabda ya kufikia huo uamuzi tunapaswa kuwa na labour data base kwanza tujue uwezo wa nguvukazi ya taifa.
2. Vitambulisho vya machinga, kule mbeya alisema atavifuta leo kasemea dosari zake hivyo naamini wazo lake la kuvifuta kaliondoa hivyo siwezi kuzungumzia kwani hajasema atafanya nini juu ya hilo
3. Kuhusu upunguzaji kodi, naona kaongea kienyeji sana labda mikutano ijayo atalitolea ufafanuzi, kasema importers wana kodi 15 yeye atazifuta ibaki moja, kwa kuwa kazitaja kwa idadi basi anazijua vizuri ni vyema akatuambia atafuta kodi zipi? Kwa uchache kuna import duty, exercise duty, vat, income tax etc. Hizi kodi zingine ni mfumo wa kimataifa chini ya WTO hiyo mifumo inafanana duniani sasa sijui anamaanisha Tanzania itajiondoa WTO, ipo mifumo ya SADC na EAC common customs kauli yake ni too skeleton na haijitoshelezi. Mfumo huu aliutumia Rais Mwinyi na ndio chanzo cha kuua viwanda vyetu vya ndani sasa anataka kuturudisha kulekule kwenye ruksa sio?
4. Kulipa fidia kwa maana ya kutibu vidonda, akumbuke kuna wahindi walinyanganywa nyumba zao wakati wa azimio la arusha nao watafidiwa? kuna makampuni ya Rockefeller na Mackenzie yalitaifishwa mashamba ya chai kahawa pareto je nayo yatafidiwa? vipi kuhusu bank ya Barclays UK ambayo ilitaifishishwa na kuanzishwa BOT nayo itafidiwa? Mgodi wa Geita Mine nao ataurudisha kwa Wajerumani? Ni vyema Chadema wakatafakari upana wa tatizo wanalotaka kulitengeneza.
5. Kuvutia wawekezaji, huu mfumo ndio alioutumia mzee wetu marehemu Mkapa, sote tunajua yaliyotupata na hatujasahau naomba usiturudishe huko, hakuna mazingira rafiki ya uwekezaji tusidanganyane. Kwanza ukilegeza mfumo wa kodi hakuna mwekezaji atakuja wekeza labda wachimba mafuta gesi na dhahabu. Mambo amabayo yeye Lissu amekuwa akiyapiga vita tangu zamani huko ubelgiji wamempa nini? Kiujumla mawazo ya Lissu ni yakienyeji sana na yaliyopitwa na wakati.