UCHAMBUZI: Tulimsoma vibaya Rais Samia

IslamTZ

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
309
182
Abuu Islam

_ 1.jpeg

Utangulizi:

Baraza jipya la mawaziri alilolitangaza Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi, Januari 8, 2022 limeshtua wengi. Vigogo, wakiwemo walioibuka katika awamu ya awamu ya tano, Maprofesa Kitila Mkumbo na Palamagamba Kabudi wametupwa, sura mpya, kama Ridhwani Kikwete, zimeingia, wengine, kama Nape Nnauye wamerejea baada ya kuwekwa pembeni awamu iliyopita.

Mshtuko uliowakumba watu ni matokeo ya kumsoma vibaya Rais Samia. Tulivyomdhania sivyo alivyo, kama ambavyo nataka kuonesha katika makala hii.

Usuli:

Katika mkutano mmoja na wanawake, akiwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anaonekana akieleza mambo yalivyokuwa siku Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ilipomteua kuwa mgombea mwenza wa Rais John Magufuli.

Anasewa baada ya mgombea urais kupatikana, walienda kukaa Kamati Kuu, ambapo yeye naye alikuwa ni mjumbe. Kamati ndogo ya vingunge wa kamati kuu ikakaa kujadiliana na mgombea waliporudi wakaja na jina.

Samia anasema: “Rais Kikwete ambaye alikuwa mwenyekiti wakati ule, akaja. Kavuta tu kiti, pap. (akawatangazia) ‘Mgombea anasema atafanya kazi na Samia.’ Mie ‘Mama yangu, siwezi siwezi siwezi.’ Wakanambia, ‘Utaweza.’”

Kwa mujibu wa Samia, makamu wa Rais aliyekuwepo wakati ule Dkt Mohammad Gharib Bilal, alimfuata akamshika mkono, akamwambia: “Sister utaweza. Ntakusaidia. Utaweza.” Kwa kauli yake Samia anasema: “Ehh haya. Ujasiri ukanishinda nikaanza kupiga kilio.”

Kwa kauli yake hii, ni wazi kuwa Rais Samia hakutarajia wala hakutamani kushika wadhifa ule wa umakamu wa rais bali aling’ang’anizwa. Watu walimuamini kuliko alivyojiamini yeye mwenyewe. Kwa sababu aliukataa umakamu wa rais mwanzo kabla ya kupewa moyo na kubadili mawazo, wengi tuliamini hata nafasi ya urais haitaki.

Labda ni kwa sababu ya mawazo hayo ndio maana baada ya kubainika kuwa Rais Magufuli alifariki, inasemekana kulikuwa na jitihada kubwa ya kufanya mapinduzi ya kikatiba kwa kutafuta namna ya kumuweka mtu mwingine. Bahati mbaya, watu wazito walisimama kidete kuhakikisha hilo halitokei.

Kwa dhana hiyo waliyokuwa nayo watu wengi, haistaajabishi kuona kuwa baada ya kuapishwa, wengi walimchukulia Rais Samia kirahisi, kama mtu aliyejikuta katika sehemu mbaya na katika muda mbaya na kulazimika kubeba mzigo usio wake. Baadhi wakamuita raisi wa bahati mbaya (accidental president), wengine wakasema ni wa mpito na hivyo wengi tukaanza kufikiria 2025 atakapopatikana mwenyewe.

Lakini kwa ushahidi wa matukio ya hivi karibuni, yaliyopelekea kujiuzulu kwa Spika Job Ndugai, ni wazi kuwa Samia si rais kishikizo bali bado yupo yupo sana tu na ana ajenda zake. Nani angedhani kuwa mwisho wa Ndugai ungekuwa wa aibu kiasi cha kulazimika kujiuzulu uspika Januari 6, katika uamuzi aliouita ni wa hiari uliozingatia maslahi ya taifa, Serikali na chama chake, CCM.

Licha ya kutaka tuamine hivyo, kila ishara zinaonesha kuwa haukuwa uamuzi wa hiari hata kidogo. Maji yalishazidi unga na alikosa mtetezi ndani ya CCM.

Kauli za Ndugai alizozitoa Desemba 26, 2021 kuhusu kiwango cha mikopo ya nchi na kutaja uwezekano wa serikali iliyopo madarakani kung’olewa katika uchaguzi mkuu wa 2025 ndiyo mambo mawili yanayotajwa kumuondoa katika nafasi yake. Kauli zake ambazo ni wazi zililenga kumkosa Rais Samia ziliudhi watu wengi na kusababisha akabiliwe na shinikizo la kujiuzulu.

Ndugai katika hotuba yake alizungumza kwa uchungu akikosoa mkopo wa shilingi trilioni 1.3 kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) wa kuwezesha mapambano dhidi ya Uviko-19, akidai kuwa mrundikano wa mikopo utapalekea nchi itapigwa mnada na kutaka fedha za tozo za miamala ya simu zitumike kugharamia miradi ya maendeleo.

Ndugai alinukuliwa akisema: “Juzi mama amekwenda kukopa Sh1.3 trilioni, deni na tuna majengo hivi sasa ya madarasa ya vituo vya afya ambayo yanajengwa kwa tozo. Hivi ipi bora, sisi Watanzania wa miaka 60 ya uhuru tuzidi kukopa hayo madeni au tubanane banane hapahapa tujenge wenyewe bila madeni haya makubwa makubwa?”

Kauli yake ilijibiwa haraka na Rais Samia, akisisitiza kwamba Serikali itaendelea kukopa ili kujenga miradi ya maendeleo. Ndugai akajiongeza na kuamua kuomba radhi, ingawa kimagumashi, maana hakukubali kosa bali alidai alinukuliwa vibaya.

Katika hatua ambayo haikutarajiwa, na hapa ndio inadhihirika kuwa watu hatukumsoma vizuri na kumuelewa mama, Rais Samia aliukataa msamaha alioombwa, badala yake akamkosoa vibaya Ndugai. Akihutubia viongozi katika hafla ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa matumizi ya fedha tajwa Shilingi trilioni 1.3 alimtaja Ndugai kuwa kuwa ana ‘stress ya 2025’.

“...Kwa sababu huwezi kuamini kiongozi mliyemwamini, mshika mhimili aende akaseme yale aliyoyasema.” alitupa kijembe Rais Samia hatua iliyoonesha kuwa Samia huyu sio yule wa 2015 aliyelia akiukataa umakamu wa rais.

Samia wa sasa:

Samia wa sasa sio tu anautaka urais, lakini ana ajenda yake. Nini kimebadilika? Majibu yanaweza kuwa katika maeneo kadhaa.

Kwanza, baada ya kupitia kipindi kigumu cha miaka mitano, akiwa makamu, Rais Samia ameona na anajua mengi. Huenda Rais Samia sasa anahisi anao wajibu wa kurekebisha mengi ambayo hayakwenda sawa katika kipindi kile cha mtangulizi wake (2015 – 2021) ndio maana alipoingia tu madarakani alianza kuleta mabadiliko hapohapo ya kisiasa, kiuchumi, kidiplomasia na kadhalika.

Pili, Rais Samia bila shaka amegundua kuwa kushikilia nafasi hiyo ya urais si suala lake binafsi tu linagusa makundi ya watu anaoyawakilisha. Iwapo akiruhusu kushindwa, itajenga taswira mbaya juu ya uwezo wa makundi hayo kupewa nchi huko baadae. Rais Samia ni Mzanzibari, Mswahili na zaidii ni mwanamke. Kushindwa kwake kutakuwa ni kizuizi kwa mtu wa aina hiyo huko baadae.

Pia, ikumbukwe kuwa makundi yote hayo matatu yana mategemeo makubwa kwake katika kusuluhisha mikwamo yao. Wazanzibari kwa miaka wanalalamika kuwa hawajatendewa haki na serikali ya Muungano, Waswahili (zaidi Waislamu) wamepitia mengi magumu awamu iliyopita na wanawake ndio usiseme - wana malalamiko kibao.

Sio siri kuwa makundi hayo yote yamefaidika kutokana na urais wake. Tukiaanza na kundi la Wazanzibari, sio siri kuwa mgao wa Zanzibar kwenye mikopo na misaada kutoka nje imepanda umeongezeka, ushahidi ukiwa ni mgao ilioupata kutoka katika fedha za mkopo wa Shirika Fedha Duniani (IMF) wa shilingi bilioni 230 kati ya shilingi trilioni 1.3 zilizopatikana kwa ajili ya nchi nzima kwa ajili ya kukabiliana na janga la corona. Fedha hizo ni sawa na zaidi kidogo ya asilimia 17.

Mwanzoni tu mwa utawala wake, Rais Samia akawatoa jela Masheikh wa Jumuiya ya Uamsho zaidi ya 30, wengi wao wakina na asili ya Zanzibar. Kutoka kwao hakuna maana kuwa hakukuwa na wengine waliokuwa na mashtaka kama hayo na ambao wamekaa ndani muda mrefu, lakini wale walikuwa ni Wazanzibari. Kisu kimegusa mfupa. Damu nzito kuliko maji.

Kundi jingine ni la wanawake, ambao sio siri kuwa nao wamefaidika mno katika ngazi zote. Kwa mara ya kwanza, Rais kateua mawaziri wanawake katika wizara ambazo hawakuwahi kuzishikilia huko nyuma, zikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Ulinzi.

Tayari Rais Samia pia kashaamua kutenganisha Wizara ya Afya mbali na Jinsia, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto, uamuzi ambao aliutangaza Desemba 16 mwaka jana. Bila shaka uamuzi huo utanyanyua hadhi ajenda ya mwanamke. Katika hatua nyingine, Rais Samia alifuta amri ya mtangulizi wake ya kuzuia wasichana waliopata mimba kurejea shule!

Katika baraza lake jipya alilolitangaza Januari 8, 2022 Samia amemteua Dkt Ashatu Kijaji kuwa Waziri wa wizara nyingine nyeti ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara. Pia, amempa Ummy Mwalimu nafasi katika Wizara ya Afya, huku akiendelea pia na Profesa Joyce Ndalichako katika wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu huku Dorothy Gwajima akipewa Wizara mpya ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Watoto na Makundi Maalum bila kumsahau Jenista Mhagama alipelekwa Utumishi.

Rais alinukuliwa akisema: “Maamuzi yangu ni kuitenga Wizara itakayoshughulikia Jinsia Maendeleo ya Wanawake kutoka kwenye kuchanganywa na Wizara ya Afya kwa sababu tukiweka Wizara ya Afya na mambo mengine na hali tuliyonayo sasa hivi duniani Sekta ya Afya peke yake inachukua sura kubwa."

Waswahili (Waislamu) nao ni kundi jingine ambalo Rais Samia analisimamia maslahi yake baada ya kupitia kipindi kigumu katika utawala wa awamu ya tano, hasa katika masuala ya uteuzi. Ilikuwa ni kawaida kwa Rais kuteua kundi la watu kwenye nyadhifa mbalimbali, bila kuwepo mswahili hata mmoja.

Katika baraza jipya alilolitangaza tunaona mawaziri pamoja na manaibu watano kutoka mkoa wa Pwani pekee wakiwemo Dkt Suleiman Jaffo, Mohammed Mchengerwa, Abdallah Ulega, Ridhwani Kikwete na Omar Kipanga. Bado kuna mkoa kama wa Tanga ambapo kwa uchache kuna mawaziri kama watatu. Zanzibar nayo haijasahauliwa, husausan kwenye wizara za muungano.

Kwa haya yanayoendelea, ni wazi kuwa tulimsoma vibaya mama. Kule kuangusha kilio baada ya kuteuliwa Umakamu Rais, hakukumaanisha udhaifu, kukosa ajenda, kukosa kujiamini au vyovyote bali ulikuwa ni mshtuko tu. Lakini huenda pia miaka mitano aliyohudumu kama Makamu Rais imemfundisha kuwa imara na kumempatia ajenda.

Kasema sahihi mwenyewe katika hotuba ambayo aliitumia kukataa msamaha alioombwa na aliyekuwa Spika, Ndugai na ‘kumchamba’. Rais Samia alisema: “Don't judge the book kwa 'cover' yake. Wamenitazama nilivyo wakasema wanijaribu. Wamekosea, hapa sipo."
 
Mungu ibariki Tanzania

Sidhani kuna asiyejua nguvu ya kiti cha urais/ufalme/umalkia/amiri jeshi mkuu.
Sidhani kama wanayoyafanya hawajui matokeo yake.
Sidhani kama walikua na ushauri na wakakosa au kushindwa kumshauri nje ya hadhara.

Tuendelee kuliombea taifa letu amani tukijua katika kila nchi kuna muwakilishi wa Mungu ambaye ni mtawala mkuu/ Mfalme/Rais wa nchi hiyo.

Kwakuwa taratibu za kumpata zilikua sahihi, na kwakuwa tumeamriwa na Mungu kuwa watii. Hatuna budi kuwa watii huku tukimuomba Mungu usiku na mchana kwaajili ya ustawi, amani na mafanikio ya Rais na taifa letu; huku tukipeleka haja zetu nyingine zisizokuwa na hila kwa Mungu tukiwa safi.

Kwa tunaamini chochote Rais anachokifanya kipo anachokijua na kukiamini; basi na sisi tuendelee kuomba ili Mungu amuongoze kwa maono na ndoto atufikishe pale tunapohitaji

Katika hili sakata wapo wanaotoa ushauri mzuri au pongezi nyingi kwa Rais lakini ni wenye hila ndani yao na muda utasema. Maadui unaowajua ni bora zaidi ya marafiki usiowajua na ukadhani ni marafiki kumbe wana jambo lao.

Wapo wanaoongea lugha mbovu/dharau/chuki/dhihaka dhidi ya Rais sababu wanaumia kwa yeye kuwa kwenye hicho kiti na wanaona hastahili. Hawana mpango kabisa wa kumsaidia Rais wanatamani watumie nguvu zao binafsi kuonyesha misimamo yao kwamba wako bora zaidi. Ila tuu wanajisahau kwamba hawana hiyo mamlaka.

Wapo wanaoongea na kukosoa kwa nguvu bila mipaka sababu wanaamini kwamba mambo yanayofanyika sio sahihi na hayawapendezi ila wanahisi hawana nafasi ya kusikilizwa. Lakini wanasahau SSH ndio Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Busara ni bora kuliko nguvu, wangeangalia njia bora yenye maslahi ya taifa ingekua bora zaidi.

Watanzania tumuombee Rais. Tumuombee apate watu sahihi wa kutafsiri kile anachotaka kufanya, na apate wasaidizi wa kukifanya kwa usahihi uleule uliotafsiriwa. Mungu ni mwema sana kwetu na ataendelea kututendea mema kadri tunavyomuomba kadri ya nia zetu njema ukamilifu wetu mbele zake.

Yohana 16:23-24
"Katika siku hiyo hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin nawaambia, kama mkimwomba Baba jambo lolote kwa jina langu, yeye atawapa. Mpaka sasa hamjaomba jambo lolote kwa Jina langu. Ombeni nanyi mtapewa, ili furaha yenu ipate kuwa kamili."
 
Sikupingi mama D
 
Abuu Islam
...

Pia, ikumbukwe kuwa makundi yote hayo matatu yana mategemeo makubwa kwake katika kusuluhisha mikwamo yao. Wazanzibari kwa miaka wanalalamika kuwa hawajatendewa haki na serikali ya Muungano, Waswahili (zaidi Waislamu) wamepitia mengi magumu awamu iliyopita na wanawake ndio usiseme - wana malalamiko kibao.

...
... hiyo ndio theme ya maelezo yako; hayo mengine ni danganya toto! Ni yapi hayo ambayo kundi hilo limepitia ambayo makundi mengine (non-waswahili wanawake) hawajapitia awamu iliyopita? With due respect elaborate them.
 
Abuu Islam

View attachment 2074036

Utangulizi:

Baraza jipya la mawaziri alilolitangaza Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi, Januari 8, 2022 limeshtua wengi. Vigogo, wakiwemo walioibuka katika awamu ya awamu ya tano, Maprofesa Kitila Mkumbo na Palamagamba Kabudi wametupwa, sura mpya, kama Ridhwani Kikwete, zimeingia, wengine, kama Nape Nnauye wamerejea baada ya kuwekwa pembeni awamu iliyopita.

Mshtuko uliowakumba watu ni matokeo ya kumsoma vibaya Rais Samia. Tulivyomdhania sivyo alivyo, kama ambavyo nataka kuonesha katika makala hii.

Usuli:

Katika mkutano mmoja na wanawake, akiwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anaonekana akieleza mambo yalivyokuwa siku Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ilipomteua kuwa mgombea mwenza wa Rais John Magufuli.

Anasewa baada ya mgombea urais kupatikana, walienda kukaa Kamati Kuu, ambapo yeye naye alikuwa ni mjumbe. Kamati ndogo ya vingunge wa kamati kuu ikakaa kujadiliana na mgombea waliporudi wakaja na jina.

Samia anasema: “Rais Kikwete ambaye alikuwa mwenyekiti wakati ule, akaja. Kavuta tu kiti, pap. (akawatangazia) ‘Mgombea anasema atafanya kazi na Samia.’ Mie ‘Mama yangu, siwezi siwezi siwezi.’ Wakanambia, ‘Utaweza.’”

Kwa mujibu wa Samia, makamu wa Rais aliyekuwepo wakati ule Dkt Mohammad Gharib Bilal, alimfuata akamshika mkono, akamwambia: “Sister utaweza. Ntakusaidia. Utaweza.” Kwa kauli yake Samia anasema: “Ehh haya. Ujasiri ukanishinda nikaanza kupiga kilio.”

Kwa kauli yake hii, ni wazi kuwa Rais Samia hakutarajia wala hakutamani kushika wadhifa ule wa umakamu wa rais bali aling’ang’anizwa. Watu walimuamini kuliko alivyojiamini yeye mwenyewe. Kwa sababu aliukataa umakamu wa rais mwanzo kabla ya kupewa moyo na kubadili mawazo, wengi tuliamini hata nafasi ya urais haitaki.

Labda ni kwa sababu ya mawazo hayo ndio maana baada ya kubainika kuwa Rais Magufuli alifariki, inasemekana kulikuwa na jitihada kubwa ya kufanya mapinduzi ya kikatiba kwa kutafuta namna ya kumuweka mtu mwingine. Bahati mbaya, watu wazito walisimama kidete kuhakikisha hilo halitokei.

Kwa dhana hiyo waliyokuwa nayo watu wengi, haistaajabishi kuona kuwa baada ya kuapishwa, wengi walimchukulia Rais Samia kirahisi, kama mtu aliyejikuta katika sehemu mbaya na katika muda mbaya na kulazimika kubeba mzigo usio wake. Baadhi wakamuita raisi wa bahati mbaya (accidental president), wengine wakasema ni wa mpito na hivyo wengi tukaanza kufikiria 2025 atakapopatikana mwenyewe.

Lakini kwa ushahidi wa matukio ya hivi karibuni, yaliyopelekea kujiuzulu kwa Spika Job Ndugai, ni wazi kuwa Samia si rais kishikizo bali bado yupo yupo sana tu na ana ajenda zake. Nani angedhani kuwa mwisho wa Ndugai ungekuwa wa aibu kiasi cha kulazimika kujiuzulu uspika Januari 6, katika uamuzi aliouita ni wa hiari uliozingatia maslahi ya taifa, Serikali na chama chake, CCM.

Licha ya kutaka tuamine hivyo, kila ishara zinaonesha kuwa haukuwa uamuzi wa hiari hata kidogo. Maji yalishazidi unga na alikosa mtetezi ndani ya CCM.

Kauli za Ndugai alizozitoa Desemba 26, 2021 kuhusu kiwango cha mikopo ya nchi na kutaja uwezekano wa serikali iliyopo madarakani kung’olewa katika uchaguzi mkuu wa 2025 ndiyo mambo mawili yanayotajwa kumuondoa katika nafasi yake. Kauli zake ambazo ni wazi zililenga kumkosa Rais Samia ziliudhi watu wengi na kusababisha akabiliwe na shinikizo la kujiuzulu.

Ndugai katika hotuba yake alizungumza kwa uchungu akikosoa mkopo wa shilingi trilioni 1.3 kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) wa kuwezesha mapambano dhidi ya Uviko-19, akidai kuwa mrundikano wa mikopo utapalekea nchi itapigwa mnada na kutaka fedha za tozo za miamala ya simu zitumike kugharamia miradi ya maendeleo.

Ndugai alinukuliwa akisema: “Juzi mama amekwenda kukopa Sh1.3 trilioni, deni na tuna majengo hivi sasa ya madarasa ya vituo vya afya ambayo yanajengwa kwa tozo. Hivi ipi bora, sisi Watanzania wa miaka 60 ya uhuru tuzidi kukopa hayo madeni au tubanane banane hapahapa tujenge wenyewe bila madeni haya makubwa makubwa?”

Kauli yake ilijibiwa haraka na Rais Samia, akisisitiza kwamba Serikali itaendelea kukopa ili kujenga miradi ya maendeleo. Ndugai akajiongeza na kuamua kuomba radhi, ingawa kimagumashi, maana hakukubali kosa bali alidai alinukuliwa vibaya.

Katika hatua ambayo haikutarajiwa, na hapa ndio inadhihirika kuwa watu hatukumsoma vizuri na kumuelewa mama, Rais Samia aliukataa msamaha alioombwa, badala yake akamkosoa vibaya Ndugai. Akihutubia viongozi katika hafla ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa matumizi ya fedha tajwa Shilingi trilioni 1.3 alimtaja Ndugai kuwa kuwa ana ‘stress ya 2025’.

“...Kwa sababu huwezi kuamini kiongozi mliyemwamini, mshika mhimili aende akaseme yale aliyoyasema.” alitupa kijembe Rais Samia hatua iliyoonesha kuwa Samia huyu sio yule wa 2015 aliyelia akiukataa umakamu wa rais.

Samia wa sasa

Samia wa sasa sio tu anautaka urais, lakini ana ajenda yake. Nini kimebadilika? Majibu yanaweza kuwa katika maeneo kadhaa.

Kwanza, baada ya kupitia kipindi kigumu cha miaka mitano, akiwa makamu, Rais Samia ameona na anajua mengi. Huenda Rais Samia sasa anahisi anao wajibu wa kurekebisha mengi ambayo hayakwenda sawa katika kipindi kile cha mtangulizi wake (2015 – 2021) ndio maana alipoingia tu madarakani alianza kuleta mabadiliko hapohapo ya kisiasa, kiuchumi, kidiplomasia na kadhalika.

Pili, Rais Samia bila shaka amegundua kuwa kushikilia nafasi hiyo ya urais si suala lake binafsi tu linagusa makundi ya watu anaoyawakilisha. Iwapo akiruhusu kushindwa, itajenga taswira mbaya juu ya uwezo wa makundi hayo kupewa nchi huko baadae. Rais Samia ni Mzanzibari, Mswahili na zaidii ni mwanamke. Kushindwa kwake kutakuwa ni kizuizi kwa mtu wa aina hiyo huko baadae.

Pia, ikumbukwe kuwa makundi yote hayo matatu yana mategemeo makubwa kwake katika kusuluhisha mikwamo yao. Wazanzibari kwa miaka wanalalamika kuwa hawajatendewa haki na serikali ya Muungano, Waswahili (zaidi Waislamu) wamepitia mengi magumu awamu iliyopita na wanawake ndio usiseme - wana malalamiko kibao.

Sio siri kuwa makundi hayo yote yamefaidika kutokana na urais wake. Tukiaanza na kundi la Wazanzibari, sio siri kuwa mgao wa Zanzibar kwenye mikopo na misaada kutoka nje imepanda umeongezeka, ushahidi ukiwa ni mgao ilioupata kutoka katika fedha za mkopo wa Shirika Fedha Duniani (IMF) wa shilingi bilioni 230 kati ya shilingi trilioni 1.3 zilizopatikana kwa ajili ya nchi nzima kwa ajili ya kukabiliana na janga la corona. Fedha hizo ni sawa na zaidi kidogo ya asilimia 17.

Mwanzoni tu mwa utawala wake, Rais Samia akawatoa jela Masheikh wa Jumuiya ya Uamsho zaidi ya 30, wengi wao wakina na asili ya Zanzibar. Kutoka kwao hakuna maana kuwa hakukuwa na wengine waliokuwa na mashtaka kama hayo na ambao wamekaa ndani muda mrefu, lakini wale walikuwa ni Wazanzibari. Kisu kimegusa mfupa. Damu nzito kuliko maji.

Kundi jingine ni la wanawake, ambao sio siri kuwa nao wamefaidika mno katika ngazi zote. Kwa mara ya kwanza, Rais kateua mawaziri wanawake katika wizara ambazo hawakuwahi kuzishikilia huko nyuma, zikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Ulinzi.

Tayari Rais Samia pia kashaamua kutenganisha Wizara ya Afya mbali na Jinsia, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto, uamuzi ambao aliutangaza Desemba 16 mwaka jana. Bila shaka uamuzi huo utanyanyua hadhi ajenda ya mwanamke. Katika hatua nyingine, Rais Samia alifuta amri ya mtangulizi wake ya kuzuia wasichana waliopata mimba kurejea shule!

Katika baraza lake jipya alilolitangaza Januari 8, 2022 Samia amemteua Dkt Ashatu Kijaji kuwa Waziri wa wizara nyingine nyeti ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara. Pia, amempa Ummy Mwalimu nafasi katika Wizara ya Afya, huku akiendelea pia na Profesa Joyce Ndalichako katika wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu huku Dorothy Gwajima akipewa Wizara mpya ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Watoto na Makundi Maalum bila kumsahau Jenista Mhagama alipelekwa Utumishi.

Rais alinukuliwa akisema: “Maamuzi yangu ni kuitenga Wizara itakayoshughulikia Jinsia Maendeleo ya Wanawake kutoka kwenye kuchanganywa na Wizara ya Afya kwa sababu tukiweka Wizara ya Afya na mambo mengine na hali tuliyonayo sasa hivi duniani Sekta ya Afya peke yake inachukua sura kubwa."

Waswahili (Waislamu) nao ni kundi jingine ambalo Rais Samia analisimamia maslahi yake baada ya kupitia kipindi kigumu katika utawala wa awamu ya tano, hasa katika masuala ya uteuzi. Ilikuwa ni kawaida kwa Rais kuteua kundi la watu kwenye nyadhifa mbalimbali, bila kuwepo mswahili hata mmoja.

Katika baraza jipya alilolitangaza tunaona mawaziri pamoja na manaibu watano kutoka mkoa wa Pwani pekee wakiwemo Dkt Suleiman Jaffo, Mohammed Mchengerwa, Abdallah Ulega, Ridhwani Kikwete na Omar Kipanga. Bado kuna mkoa kama wa Tanga ambapo kwa uchache kuna mawaziri kama watatu. Zanzibar nayo haijasahauliwa, husausan kwenye wizara za muungano.

Kwa haya yanayoendelea, ni wazi kuwa tulimsoma vibaya mama. Kule kuangusha kilio baada ya kuteuliwa Umakamu Rais, hakukumaanisha udhaifu, kukosa ajenda, kukosa kujiamini au vyovyote bali ulikuwa ni mshtuko tu. Lakini huenda pia miaka mitano aliyohudumu kama Makamu Rais imemfundisha kuwa imara na kumempatia ajenda.

Kasema sahihi mwenyewe katika hotuba ambayo aliitumia kukataa msamaha alioombwa na aliyekuwa Spika, Ndugai na ‘kumchamba’. Rais Samia alisema: “Don't judge the book kwa 'cover' yake. Wamenitazama nilivyo wakasema wanijaribu. Wamekosea, hapa sipo."
well narated
 
SAMIA ni chuma Cha pua,

Sukuma Gang wote chalii, chama na nchi vimerudi kwa wenyewe Sasa, alhamdulilah,

Mungu ampe Samia na team yake umri mrefu na kujiamini
 
Huyu mama sifa na uwezo wa kua rais hana. Tusubiri miaka 2 ijayo hadi uchaguzi ndio tutajua huyu mama uwezo hana.
 
Ni wakati wenu Waswahili
 
You know tunataka maendeleo, kama rais atakuwa haleti matokeo mazuri ya ukuaji wa uchumi wa Tz, basi kiuhalisia kazi itakuwa imemshinda na sioni sababu ya kujipanga kuendelea mwaka 2025, yeye awe focus na kuleta maendeleo, sisi wananchi tutamjudge kama anafaa kuendelea au hafai, ila mpaka sasa maneno ni mengi kuliko vitendo na hii inakatisha sana tamaa
 
Back
Top Bottom