Ndugu zangu,
Kuna mtangazaji wa redio kule Arusha amenihoji mchana huu. Ametaka kujua tafsiri yangu kwa kilichotokea jana.
Nilimwambia, kuwa tafsiri moja kubwa ya kilichotokea ni kuwa Edward Lowassa sio kwamba yuko njiani kurudi CCM, bali ameshafika nyumbani alikotokea, CCM. Lowassa amerudi kundini. Mwenda kwao si mtoro, walisema Wahenga.
Kwamba kwa Chadema kuanza kumshambulia Lowassa sasa ni kumpigia penalti mikononi. Lowassa ni mwanasiasa mzoefu, hatahangaika kulumbana na aliowaacha alikotoka, atawaacha wengine wafanye kazi hiyo. Upinzani bado una mtaji wa kupambana na CCM kwa hoja.
Na wala haijajulikana, Lowassa na Magufuli wameongea nini wakiwa wawili. Hata hivyo, kwa lugha ya picha, inaonyesha kuna mazuri wamekubaliana.
Kwa wakati huu utakuwa ni mkakati wa kimakosa, kuwaandama wanaondoka upinzani, watu wa aina ya Lowassa. Badala yake, kuna haja pia hata kimya kimya, kwa upinzani kumshukuru mwanasiasa kama Lowassa ambaye kura milioni sita alizovuna kwenye uchaguzi uliopita ilikuwa na tafsiri ya kusaidia upinzani kupata viti zaidi bungeni ( Lowassa Effect).
Nilimwambia mtangazaji yule kijana, kuwa yawezekana kabisa kuwa John Magufuli ndiye mwenye furaha zaidi kwa sasa kwa kufanikiwa kuisambaratisha CCM ' B' ambayo, kwa sasa, ni hatari zaidi kwake kuliko vyama vyote vya upinzani kwa pamoja.
Naam, Afrika mvua hainyeshi ghafla. Mzee Ali Hassan Mwinyi ni mmoja wa viongozi wa nchi hii ninaowaheshimu sana. Naamini pia, Rais Mstaafu Mwinyi anayeheshimika na wengi.
Nilikuwepo viwanja vya Jangwani siku CCM ilipofanya uzinduzi wa kampeni zake uchaguzi uliopita. Nilimwona na kumsikia kwa masikio yangu Mzee Mwinyi akisema , kuwa kuna CCM ' A' na CCM ' B'. Na kwamba kama CCM ' A' ipo kwanini mchague CCM ' B'.
Kwa kuangalia kampeni za UKAWA, ndipo maneno ya Mzee Mwinyi yalipodhihiri. Kampeni za mgombea Urais wa Ukawa kimsingi zilitawaliwa na Wana- CCM wa zamani.
Ni viongozi wa zamani wa CCM aina ya Edward Lowassa, Sumaye, Guninita, Mgeja, Masha, Kingunge na baadhi wengine. Kuna wakati ilikuwa mtu anahangaika kuitafuta safu ya upinzani ya wapiganaji aina ya John Mnyika, Godbless Lema, Tundu Lissu, Halima Mdee na wengine. Ilitoa tafsiri pia, kuwa upinzani, hadi miezi mitatu kabla ya uchaguzi, ulikuwa haujajiandaa kuunda Serikali kwa kutegemea safu yake.
Duniani hapa dalili ya mvua ni mawingu. Afrika mvua hainyeshi ghafla. Mwenye kutamka kuwa mvua imenyesha ghafla, huyo hajajisumbua kuangalia juu mawinguni. Afrika hata kusanyiko la mawingu ya mvua lina dalili zake. Wazee wetu wa zamani walikuwa na maarifa ya kuona dalili za kusanyiko la mawingu ya mvua. Ninachotaka kusema hapa ni hiki; kila jambo ni wakati na dalili.
Na tunapokumbushana umuhimu wa kusoma ishara za nyakati hatuna maana ya kuziangalia saa zetu za mikononi au ukutani. Ni kuyaangalia matendo yetu ya sasa na hivyo basi umuhimu wa kuzisoma ishara za mambo yatakayotokea.
Kwa kutafakari kauli ya Mzee Mwinyi nimepata kuandika hapa kuwa moja ya changamoto ya Serikali John Magufuli ni namna ya kuishi maisha ya kisiasa na kufanya kazi huku kukiwa na upinzani unaotoka kwa wapinzani asilia, na wale wa kutoka CCM' B'.
Naziona ishara za mwanzo wa mwisho wa CCM ' B'.
Maggid,