Elections 2010 Uchambuzi, na Msimamo Wangu...!

Konakali

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
1,533
263
Wakuu hebu nisaidieni maana kila nikijaribu kuchambua sera na ahadi za CCM, na wagombea wake nayakuta yana sifa kuu tatu ambazo zinanipelekea kujiuliza maswali yasiyo na majibu...!

  1. Ahadi nyingi ni za kwenda kuomba au alizoahidiwa pengine:Utamsikia JK akisema, tumeingia mkataba na Marekani, Japan, China, etc. Au nimeahidiwa na Obama...! Sasa mimi najiuliza hii misaada inayotolewa na Marekani, China, Obama nk, wanatoa kwa Watanzania au kwa CCM/Kikwete? Kama wanatoa kwa Watanzania, je ndio kigezo cha sisi kumchagua Kikwete na CCM? Tukiwachagua wengine hawatatupa hiyo misaada tena? Kikwete mwenyewe alisema; "Ukitaka kula, lazima uliwe...!", na kweli wahenga walisema, "Ya bure ni ya ghali". Je, hii misaada inatupeleka wapi? Nadhani kuna haja ya kuwa masikini jeuri, vinignevyo, tutaliwa...!
  2. Ahadi nyingine ni vitu ambavyo pengine vipo kwenye mchakato au vimeshaanza na vipo katika hatua fulani: Kwa mfano akifika huko Rukwa utamsikia akisema, "Tunajenga barabara tatu kwa kiwango cha lami...!". Hivi tukiwachagua wengine hizi barabara hazitajengwa tena? Akienda kwenye shule za kata anaahidi kuweka maabara na kuleta waalimu...! Kwani wakati hizo shule zinajengwa, maabara na waalimu hazikuwepo kwenye mpango? Je, tukiwachagua wengine, waalimu hawatakuja na maabara hazitajengwa? Hivi wajibu wa serikali yeyote ile ni nini? Mbona wajibu yanafanywa kuwa ahadi?
  3. Ahadi zingine haziwezekani hata kwa akili za kimbayuwayu, yaani "IMPOSSIBLES": Utasikia akiahidi hospitali za rufaa kila mkoa, wakati hata zilizopo kwa sasa hazina madawa...! Hospitali imelazimishwa tu kuwa ya mkoa kwa kutokuwa na sifa, halafu unaahidi kuipa hadhi ya rufaa...! Ahadi ulizotoa miaka mitano iliyopita hazikukamilika kwa kiwango cha kuridhisha, je, ukiongeza na zingine ndio zitawezekana? CCM imeshindwa kuondoa UJINGA, UMASIKINI, na MARADHI kwa miaka 50 ya uongozi wake...! Je, pamoja na kuongezeka kwa RUSHWA, na UFISADI, ndio wataweza kwa miaka mitano tu?
CCM wanaomba ridhaa ya kuitawala nchi, na dola ili wapate kuleta MAPINDUZI ya kuipindua nchi mithili ya "Miguu juu, Kichwa chini". Lakini CHADEMA wanaomba kuiongoza nchi, na dola ili wapate kuleta "Demokrasia na Maendeleo ya Kweli". Hivyo, kamwe tusikubali KUTAWALIWA, bali KUONGOZWA...! Na hata kwa kushinda msituni, nipo tayari kupigania Demokrasia na Maendeleo, maana ndio hitaji langu, familia yangu, jamii yangu, na nchi yangu kwa ujumla...!
 
mhhh hayo ndo wananifanya mimi nikawachape hiyo tarehe 31 tena kwa hasira, TUSIFANYE MAKOSA JAMANI!
 
Back
Top Bottom