Uchambuzi: Mzunguko wa hela, faida na hasara

neo1

JF-Expert Member
Sep 1, 2013
576
840
MAONI YANGU KUHUSU HALI YA UCHUMI WA NCHI KWA SASA.

By Malisa GJ,

Leo gazeti la Mtanzania limeripoti kufungwa kwa Hotel kadhaa za kifahari kutokana na sababu mbalimbali, lakini SABABU KUU iliyotajwa ni hatua ya serikali kuzuia mikutano yake kufanyika hotelini, badala yake ifanyike kwenye kumbi za serikali na kudaiwa kodi (Mtanzania, Julai 14, 2016, uk.3 na 4).

Nilitamani kufanya uchambuzi wa kina kuhusiana na hali hii lakini nizungumze kwa kifupi kwa sababu niko 'field' huku kwa wanyantuzu natafuta karo ya shule ya mwanangu.

Nionavyo uamuzi huu wa serikali una faida na hasara zake.

#FAIDA_KWA_KIFUPI;

#Mosi; Mzunguko wa fedha utapungua na hivyo kusaidia sana kucontrol inflation rate (mfumko wa bei, unaotokana na monetary factor sio production factor). Sifa mojawapo ya fedha ni isiwe holela. Pesa ikiwa holela inasababisha mfumuko wa bei (inflation by monetary factor). So pesa inatakiwa ipotee kidogo, iwe adimu lakini si adimu sana (money should be scarce but not very scarce).

Kwahiyo pesa ikipotea kdg hata bei ya bidhaa na huduma itashuka. Maana yake ni kwamba bidhaa zitakuwepo lakini pesa hamna kwa hiyo itabidi zishuke bei. Hii itawaumiza wafanyabiashara lakini itawasaidia sana walaji.

Na hii ni mbinu nzuri sana ya kudhibiti uchumi. Bidhaa na huduma vitapungua bei sana. Kwa mfano Hotel ambayo ulikua ukilala kwa 400,000/= kwa usiku mmoja, muda si mrefu utaanza kulala kwa 100,000/= na zile za 100,000/= zitashuka hadi 40,000/=. Mfuko wa Cement kama unanunua 15,000/= tegemea kununua 8,000/= muda si mrefu. Hii ni habari njema kwa walaji (Consumers) lakini habari mbaya kwa wazalishaji (Producers) na wafanyabiashara.

#Pili; Njia hii itasaidia sana kuleta "nidhamu ya kazi". Kwa kuwa mzunguko wa pesa utakuwa mdogo itawalazimu watu kufanya kazi kwa bidii ili kupata pesa. Enzi za kupata pesa kiulaini zimekufa. Enzi za kumuandikia Mkuu wa Idara "minutes" na kujifanya mlikua na kikao, halafu mkuu wa Idara anasaini mjilipe posho, enzi hizo zimekwisha rasmi. Sasa ni kazi tu.

Kama unataka pesa fanya kazi, kama hutaki utakula jeuri yako. Kwahiyo kuanzia sasa watu watafanya kazi kwa bidii na uchumi wa nchi utakua kwa kasi. Utashangaa kuuziwa mfuko wa Cement 7,000/= lakini utashangaa zaidi kwamba unafanya kazi siku mbili hiyo 7,000/= huipati. Kutakuwa hakuna namna nyingine zaidi ya kuongeza bidii.!

#Tatu; Njia hii itasaidia sana kuimarisha sarafu yetu. Moja ya mambo yaliyokua yakichangia kuporomoka kwa sarafu yetu ni inflation rate kuwa kubwa sana. Sasa kwa utaratibu huu wa JPM inflation itakuwa controled kwa hiyo pesa itapotea mitaani.

Na pesa ikipotea maana yake itatafutwa. Na ikitafutwa means demand yake inaongezeka. Na demand ikiongezeka means thamani yake pia inaongezeka. Kwahiyo pesa ikipotea means demand yake inakua kubwa. (Law of demand; price falls with increase of demands, and vice versa). Kwahiyo usishangae hadi kufika mwaka 2020 Dola 1 ya kimarekani ikauzwa Shilingi 1,000/= au chini ya hapo.

Pia kwa kuwa mzunguko wa pesa utakuwa mdogo watu hawatafanya tena shopping nje ya nchi, kwa hiyo watanunua zaidi bidhaa za ndani na hivyo kusaidia kuimarisha sarafu yetu.

#Nne; Njia hii itasaidia kuleta nidhamu ya matumizi. Yani mtu akipata hela ataitunza vizuri na kufanya saving maana hajui kama kesho atapata tena. Unajua watu hawakuwa na nidhamu kabisa ya matumizi. Ulikua unakuta mtu anaenda bar weekend moja anatumia Milioni moja inaisha.

Wiki inayofuata anaenda tena na milioni bar inateketea. Ananunulia watu pombe, anahonga kila mwanamke anayemrembulia, akienda "Live band" kila jina lake likitajwa anatoa laki moja. Lakini kuanzia sasa nidhamu itakuwepo. Hakuna mtu atakayekua na ujasiri wa kufanya mbwembwe za kijinga tena kama hizo. Nidhamu ya matumizi itaongezeka sana.

#Tano; itasaidia kupunguza ombwe (gap) kati ya wenye nacho na wasiokua nacho. Ngoja nikupe mifano michache. Kuna watumishi ambao mishahara yao haizidi milioni moja lakini walikua na uhakika wa kuingiza milioni 5 hadi 6 kila mwisho wa mwezi kwa "deals" mbalimbali. Mara vikao, mara safari, mara manunuzi (procurement wanakula 10%) etc.

Kwahiyo unakuta mtu ana kipato cha milioni 7 au 8 kwa mwezi, anajiona juu kuliko wewe ambaye kipato chako ni laki 8. Anafanya shoping Nakumat wewe shoping yako Mwenge. Lakini kuanzia sasa ngoma droo. Wote mnaenda kuhemea sokoni Buguruni malapa.

#Sita; Maskini wataanza kumiliki ardhi na bei ya ardhi na viwanja itaanza kuwa "affordable" katika maeneo mengi. Unajua ardhi ilikua inapandishwa na "wapiga dili". Mtu amepata hela zake bila jasho anaenda kununua ardhi kwa mamilioni na kusababisha ardhi ya eneo hilo kupanda thamani. Kama mnakumbuka ile skendo ya boss mmoja wa shirika moja la hifadhi ya jamii aliyenunua ardhi Arusha kwa milioni 5 halafu akaiuza kwa shirika analoliongoza kwa shilingi bilioni 1.

Sasa imagine ardhi imepanda thamani kutoka Milioni 5 hadi nilioni 1 ndani ya mwaka mmoja. Kwahiyo wenye ardhi jirani na hapo wakiona mwenzao kauza Bilioni 1 nao wanapandisha bei. Lakini kuanzia sasa "discipline" itakuwepo. Mfumuko wa bei katika ardhi hautakuwepo tena kwahiyo hata maskini watakuwa na uwezo wa kununua na kumiliki ardhi.

#HASARA_KWA_KIFUPI

#Mosi; watu wengi sana watapoteza ajira kutokana na sekta nyingi za uzalishaji kufungwa. Jiulize mahoteli yote yaliyofungwa wafanyakazi wanaenda wapi? Na sio kwenye mahoteli tu, viwanda vitafungwa, makampuni na mashirika yatapunguza wafanyakazi. Wote hao wataenda kulundikana mtaani na kugeuka kuwa tegemezi.

#Pili; Taasisi nyingi za fedha zitafilisika. Mabenki yaliyozoea kukopesha wafanyabiashara kwa riba kubwa sasa hivi yatakosa wateja, na hivyo "ku-run bankrupt". Kwahiyo tutegemee mabenki mengi kufa, na machache yatakayo-survive yatapunguza wafanyakazi pamoja na kufunga baadhi ya "branches" zake.

#Tatu; Sekta nyingi za uzalishaj na fursa za ujasiriamali zitadumaa. Hii ni kwa sababu hazitakuwa na mitaji na pia wananchi hawatakuwa na purschasing power ya kuweza kumudu gharama ya baadhi ya bidhaa.

Kwamfano mtu alikua anaweza kwenda bank akakopa milioni 500 akaanzisha duka la kuuza vitu vya ndani kama furniture, mafriji, TV set, na akapata wateja wengi ndani ya mwaka mmoja akarudisha mkopo wa benki akaanza kula faida.

Lakimi kuanzia sasa hivi wajasiriamali wengi hawatathubutu kukopa. Na wakikopa hawatakuwa nacuwezo wa kulipa. Kwa hiyo mfanyabiashara akinunua bidhaa za milioni 500 akaziweka dukani, halafu baada ya mwezi mauzo ni laki 6, lazima atafute sumu ya panya atangulie akhera madukani.!

#Nne; Kuyumba kwa bei katika soko la hisa kwa sababu baadhi ya wanahisa katika makampuni mengi wanaweza kuuza hisa zao kufidia mikopo yao benki. Na kwakuwa fedha itakuwa adimu (scarce) watalazimika kuuza hata kwa bei ya hasara hali itakayosababisha soko la hisa kuyumba.

#Tano; kuongezeka kwa vitendo vya kihalifu. Kwa kuwa watu wengi watapoteza kazi, wengine biashara zao, wengine watapoteza dili zao za kuwaingizia kipato, watalazimika kutafuta njia nyingine ya kuishi. Na njia Rahisi ni kujiingiza katika vitendo vya kihalifu. Ujambazi, Ukahaba, Utapeli, Wizi etc.

Kwahiyo tutegemee kusikia matukio mengi ya ujambazi na unyang'anyi wa kutumia silaha katoka maeneo kama benki, super markets, Bureau de change, na hata majumbani. Hakuna mtu atakayekua tayari kukuona unatoa milioni 1 ATM akakuacha hivihivi wakati yeye ana siku ya pili hajala.

#HITIMISHO:
Sisemi Rais aendelee kubana matumizi au aache. Nachotaka kusema ni kuwa apiime kati ya faida na hasara kisha afanye maamuzi kwa maslahi ya nchi. Zipo faida na hasara nyingi zaidi ya hizi. Hapa nimeeleza kwa kifupi tu, lakini najua Rais anao washauri wazuri wa masuala ya kiuchumi watamsaidia kumshauri vizuri kwa maslahi ya "Mama Tanzania"

Malisa G.J
 
Hata Marekani baadhi ya majimbo kama si yote Elimu wanatia bure. Lipa kodi mkuu itawezekana
 
Tunahitaji sasa kuzimantain hizo.faida na kuzitafutia ufumbuzi.hizo hasara....moderation is.important
 
Hapo kwenye inflation umeleta uchumi wa form six! Mfumuko wa bei unazuiwa kwa faida tu pale uzalishaji ubapoongezwa. Hii ya kupakuwa ela kwenye mzunguko pasipo kuongeza uzalishaji ati kuzuia mfumuko wa bei ni counterproductive na wachumi makini kamwe hawasahuri hili. Kama economic theories za form five na six ndio zinazoongoza uchumi wetu tuna kila sababu ya kusema uchumi wa nchi yetu uko mahututi.
 
Biashara zikipungua na vitu kushuka bei maana yake ni kodi ya mapato na hata VAT iliyokuwa inaingia serikali kutokana na mauzo ya bidhaa na huduma mbalimbali nayo itashuka.

Watu wakipoteza kazi hata PAYE nayo itapungua.
 
Great economical analysis
Ahsante nadhani sasa tuko kwenye right track
Kama mbinu za uchumi za awamu zilizopita hazikusaidia twende na hizi basi
Ahsante mkuu
 
Hapo kwenye inflation umeleta uchumi wa form six! Mfumuko wa bei unazuiwa kwa faida tu pale uzalishaji ubapoongezwa. Hii ya kupakuwa ela kwenye mzunguko pasipo kuongeza uzalishaji ati kuzuia mfumuko wa bei ni counterproductive na wachumi makini kamwe hawasahuri hili. Kama economic theories za form five na six ndio zinazoongoza uchumi wetu tuna kila sababu ya kusema uchumi wa nchi yetu uko mahututi.
Ni kweli supply ikiwa kubwa demand ya bidhaa itashuka na bei itashuka,ila demand ikiwa kubwa na supply ikiwa ndogo lazima bidhaa ipande bei.
 
MAONI YANGU KUHUSU HALI YA UCHUMI WA NCHI KWA SASA.By Malisa GJ,...Nilitamani kufanya uchambuzi wa kina kuhusiana na hali hii lakini nizungumze kwa kifupi kwa sababu niko 'field' huku kwa wanyantuzu natafuta karo ya shule ya mwanangu.

Nionavyo uamuzi huu wa serikali una faida na hasara zake....#Sita; Maskini wataanza kumiliki ardhi na bei ya ardhi na viwanja itaanza kuwa "affordable" katika maeneo mengi. Unajua ardhi ilikua inapandishwa na "wapiga dili". Lakini kuanzia sasa "discipline" itakuwepo. Mfumuko wa bei katika ardhi hautakuwepo tena kwahiyo hata maskini watakuwa na uwezo wa kununua na kumiliki ardhi.
Huyu mwandishi wa hizi hasara na faida amenifurahisha sana. Inawezekana alikuwa anatania au ameamua kuwapandisha watu hasira.

Zisome hasara alizoziorodhesha, ukishazifahamu soma hayo niliyoweka wino mwekundu. Maskini ambaye hana pesa ya kununulia sukari ya bei elekezi vipi atakuwa na uwezo wa kununua ardhi?

Kwa nini anatafuta karo ya shule wakati (Chairman Mau?) Chairman mteule Magu anatoa elimu bure?
Hiyo karo si aitumie kununulia ardhi?

Hivi kweli kuna mdanganyika anayeamini maisha yatakuwa rahisi au nafuu chini ya uongozi wa Mtumbua Majipu? Ninavyowasikia wananunung'unika huku mtaani ni kwamba kila mmoja anasaga meno. Wadanganyika zote zinasikia maumivu ya kutumbuliwa majipu na kukamuliwa maziwa bila kupewa majani(malisho).
 
Mkuu katika vitu vyote izo ni issue ndogo!!!
Je tuendelee kufunga mkanda???,
Je huu ndo mfumo rasmi au kila Rais atakuja na mfumo wake!!!
Kuna weza kuwa na nia njema ila kwa kiasi kikubwa waathirika ni kada ya kati na chini!!,
Je mfumo wetu Kama nchi ni upi,je sera yetu ya uchumi ni ipi???
 
Mfumo wetu ni ujamaa , kugawiana umasikini na kutegemea wafadhili.
Sera yetu ya uchumi ni hapakodi tu na kutumbuana.
Mfumo wa maisha ni kuishi kama malaika, kuombeana kwa Mungu na kumpatia Kaizari vilivyo vyake.
 
Serikali ya kugawa umaskini kwa Watanzania walio wengi na kugawa utajiri kwa wachache watwnda maovu wakiwemo mafisadi, wezi wa mali ya umma, wapokea rushwa, wakwapuzi wa mashirika ya umma, wakwapuzi wa nyumba za Serikali, majangili na wauza unga. CCM oyee CCM oyee.
 
Back
Top Bottom