Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,151
- 44,081
Wakati wa kampeni sasa unewadia, kila kitu kiko wazi na kitaendelea kuwa wazi. Hapa ni uchambuzi mfupi sana kuelezea namna mahesabu ya CCM yalivyokwenda kombo mpaka kufikia sasa.
Kifupi hesabu zilizopigwa na CCM hapo kabla hazisomeki kabisa. Kwa mfano.
1/ MCHAKATO WA KUTEUA MGOMBEA URAIS.
Mpango wa CCM ulikuwa ni kumpata mgombea wake wa urais na hapo hapo wote watakaoshindwa wabaki ndani ya CCM ili kuleta ushindi.
Pasipo kutegemea kabisa, Edward Lowassa akiwa ndiye mgombea mwenye nguvu, ushawishi na watu wengi zaidi ndani ya CCM aliamua kuhamia CHADEMA na sasa ndiye mgombea urais wa CHADEMA.
Hili ni pigo zito sana kwa CCM kimahesabu.
2/ KUSAMBARATIKA KWA UKAWA.
CCM ilipanga na kujizatiti kabisa kuhakikisha UKAWA inavunjika kabla ya kampeni kuanza, mahesabu ya CCM yalionyesha kuwa ni rahisi sana kushinda kama wapinzani hawatakuwa pamoja. Bahati mbaya sana kwa CCM hilo halijatokea na UKAWA wako pamoja, tena imara zaidi. Hili ni pigo kubwa sana kwa CCM kimahesabu.
3/ MGOMBEA MWENZA MWANAMKE.
CCM kwa makusudi kabisa kiliteua mgombea Mwenza mwanamke(Samia Suluhu) kwa lengo la kutafuta kura za wanawake, ikitegemea kuwa ni rahisi sana kuingia kwenye kampeni kwa hoja ya kuwa CCM inawajali sana wanawake.
Bahati mbaya sana kwa CCM, tayari chama cha ACT kimemteua mwanamke(Anna Nghwira) kuwa mgombea wake wa urais ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama hicho, hivyo kuua kabisa agenda ya CCM ya kutaka kutumia uanamke kama kigezo cha kupata kura kwa wanawake wasiokuwa na upeo mkubwa.
Bahati mbaya kabisa kwa CCM ni kuwa mgombea wake mwenza(Samia Suluhu) sio mwanasiasa maarufu au mwenye ushawishi, hakubaliki kabisa kwa wazanzibar na anafahamika zaidi Tanzania bara kama mtu aliyetumika kuharibu maoni ya watanzania katika mapendekezo ya rasimu ya katiba, wakati wa bunge maalum la Katiba.