Siku hizi kila uchaguzi ni burudani tu! kwa ufisadi ndani ya serikali hii ni majambazi tu ndo wanaweza kukaa kwa amani ndani ya chama cha magamba.Huko Chato, katika Mkoa mpya wa Geita, CHADEMA kimepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa wenyeviti wa serikali za vijiji baada ya kuibwaga CCM kwa kupata vijiji vinane kati ya 11 vilivyokuwa vikishindaniwa.
Uchaguzi huo mdogo wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi na baadhi ya viongozi waliokuwepo awali jimboni humo kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vifo ambao ulifanyika hivi karibuni uliwafanya baadhi ya Wana CCM kujiunga na CHADEMA mara baada ya matokoeo kutangazwa akiwamo aliyekuwa mgombea wa CCM wa Kijiji cha Minkoto.
Nafasi zilizogombewa zilikuwa zikishikiliwa na viongozi wa CCM kabla ya baadhi yao kujiuzulu, kuhamia vyama pinzani na wengine kuhama makazi yao na kwenda maeneo mengine.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo, Sodio Nyuga alisema CHADEMA kimefanikiwa kutwaa nafasi 8 za vijiji dhidi ya tatu zilizonyakuliwa na CCM.
What do u mean!I cant wait to see......the day for liberation
Ushindi wa namna hii CCM wanauita KIMBUNGA.
Siku hizi kila uchaguzi ni burudani tu! kwa ufisadi ndani ya serikali hii ni majambazi tu ndo wanaweza kukaa kwa amani ndani ya chama cha magamba.
Rejao mwambie mjomba afanye haraka amvue Lissu ubunge ili akasaidiane na Lema kuimarisha M4C na kuzidi kuandaa mazingira ya 2014 na baadae 2015 kwa maana vitenge na khanga siku hiz si ki2 tena,tulizoeshwa kura za vijijini CCM inaelekea kushinda nafasi flani sasa ajabu naona vijijini nako pamegeuka mjini ...hakika nchi imetakata!
Hivi bado hamujaweza kusoma alama za vidole?hata kama alama za nyakati zimewashinda mngejitahidi kusoma kule Mwanza kisiwani walikoamua kumchagua mwenyekiti kwa kusimama msitarini na kuhesabiwa
Kwa dhuluma hizi mnazidi kuukoleza moto na kamwe hamwezi kuliokoa jahazi na abiria wenu ni lazima wafe maji...Sugu aliwaambia huu si upepo na kamwe haupiti,hii ni tufani na ni lazima paa liondoke na nyumba yake
Wasalimie magogoni,tell them CDM's mission is half done measured at a very shocking speed.