Uchaguzi: Wenyeviti serikali za vijiji CHADEMA 8 CCM 3

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Huko Chato, katika Mkoa mpya wa Geita, CHADEMA kimepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa wenyeviti wa serikali za vijiji baada ya kuibwaga CCM kwa kupata vijiji vinane kati ya 11 vilivyokuwa vikishindaniwa.

Uchaguzi huo mdogo wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi na baadhi ya viongozi waliokuwepo awali jimboni humo kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vifo ambao ulifanyika hivi karibuni uliwafanya baadhi ya Wana CCM kujiunga na CHADEMA mara baada ya matokoeo kutangazwa akiwamo aliyekuwa mgombea wa CCM wa Kijiji cha Minkoto.

Nafasi zilizogombewa zilikuwa zikishikiliwa na viongozi wa CCM kabla ya baadhi yao kujiuzulu, kuhamia vyama pinzani na wengine kuhama makazi yao na kwenda maeneo mengine.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo, Sodio Nyuga alisema CHADEMA kimefanikiwa kutwaa nafasi 8 za vijiji dhidi ya tatu zilizonyakuliwa na CCM.
 
Kama taarifa hii ni sahihi,hiyo ni tahadhari kwa wana CCM wote ambao bado hawajafanya maamuzi sahihi kisiasa!
 
Huko Chato, katika Mkoa mpya wa Geita, CHADEMA kimepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa wenyeviti wa serikali za vijiji baada ya kuibwaga CCM kwa kupata vijiji vinane kati ya 11 vilivyokuwa vikishindaniwa.

Uchaguzi huo mdogo wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi na baadhi ya viongozi waliokuwepo awali jimboni humo kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vifo ambao ulifanyika hivi karibuni uliwafanya baadhi ya Wana CCM kujiunga na CHADEMA mara baada ya matokoeo kutangazwa akiwamo aliyekuwa mgombea wa CCM wa Kijiji cha Minkoto.

Nafasi zilizogombewa zilikuwa zikishikiliwa na viongozi wa CCM kabla ya baadhi yao kujiuzulu, kuhamia vyama pinzani na wengine kuhama makazi yao na kwenda maeneo mengine.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo, Sodio Nyuga alisema CHADEMA kimefanikiwa kutwaa nafasi 8 za vijiji dhidi ya tatu zilizonyakuliwa na CCM.
Siku hizi kila uchaguzi ni burudani tu! kwa ufisadi ndani ya serikali hii ni majambazi tu ndo wanaweza kukaa kwa amani ndani ya chama cha magamba.
 
ni upepo tu huu utapita, watakapotaamaki kumbe kilikuwa ni kimbunga.............
 
Kama matokeo ndiyo hayo, hakika mtikisiko kwa CCM ni mkubwa sana, na bila kufanya tathmini na kuchukua hatua hakika CCM kitakuwa chama cha ubinzani si muda mrefu kuazia sasa
 
Hivi bado wanatuita sisi 'wanachama wa chama cha msimu...'

Serikali huanzia shinani...

M4C reloaded, with no apology!!
 
Mi nimeipenda. Kama na mwaka 2015 wanakijiji wengi watakuwa wameelimika kama hawa(vijiji vya Geita),basi mabadiliko ya kweli yatapatikana.
 
Rejao mwambie mjomba afanye haraka amvue Lissu ubunge ili akasaidiane na Lema kuimarisha M4C na kuzidi kuandaa mazingira ya 2014 na baadae 2015 kwa maana vitenge na khanga siku hiz si ki2 tena,tulizoeshwa kura za vijijini CCM inaelekea kushinda nafasi flani sasa ajabu naona vijijini nako pamegeuka mjini ...hakika nchi imetakata!

Hivi bado hamujaweza kusoma alama za vidole?hata kama alama za nyakati zimewashinda mngejitahidi kusoma kule Mwanza kisiwani walikoamua kumchagua mwenyekiti kwa kusimama msitarini na kuhesabiwa

Kwa dhuluma hizi mnazidi kuukoleza moto na kamwe hamwezi kuliokoa jahazi na abiria wenu ni lazima wafe maji...Sugu aliwaambia huu si upepo na kamwe haupiti,hii ni tufani na ni lazima paa liondoke na nyumba yake

Wasalimie magogoni,tell them CDM's mission is half done measured at a very shocking speed.
 
Siku hizi kila uchaguzi ni burudani tu! kwa ufisadi ndani ya serikali hii ni majambazi tu ndo wanaweza kukaa kwa amani ndani ya chama cha magamba.

siyo upepo huo ni kimbunga sasa, je utapita?
 
Rejao mwambie mjomba afanye haraka amvue Lissu ubunge ili akasaidiane na Lema kuimarisha M4C na kuzidi kuandaa mazingira ya 2014 na baadae 2015 kwa maana vitenge na khanga siku hiz si ki2 tena,tulizoeshwa kura za vijijini CCM inaelekea kushinda nafasi flani sasa ajabu naona vijijini nako pamegeuka mjini ...hakika nchi imetakata!

Hivi bado hamujaweza kusoma alama za vidole?hata kama alama za nyakati zimewashinda mngejitahidi kusoma kule Mwanza kisiwani walikoamua kumchagua mwenyekiti kwa kusimama msitarini na kuhesabiwa

Kwa dhuluma hizi mnazidi kuukoleza moto na kamwe hamwezi kuliokoa jahazi na abiria wenu ni lazima wafe maji...Sugu aliwaambia huu si upepo na kamwe haupiti,hii ni tufani na ni lazima paa liondoke na nyumba yake

Wasalimie magogoni,tell them CDM's mission is half done measured at a very shocking speed.

Mbona hatusikii tena matawi yao ya Marekani na Uingereza yakifunguliwa? Magamba this time yatavuliwa kwa maji ya moto.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom