EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
Huko Chato, katika Mkoa mpya wa Geita, CHADEMA kimepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa wenyeviti wa serikali za vijiji baada ya kuibwaga CCM kwa kupata vijiji vinane kati ya 11 vilivyokuwa vikishindaniwa.
Uchaguzi huo mdogo wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi na baadhi ya viongozi waliokuwepo awali jimboni humo kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vifo ambao ulifanyika hivi karibuni uliwafanya baadhi ya Wana CCM kujiunga na CHADEMA mara baada ya matokoeo kutangazwa akiwamo aliyekuwa mgombea wa CCM wa Kijiji cha Minkoto.
Nafasi zilizogombewa zilikuwa zikishikiliwa na viongozi wa CCM kabla ya baadhi yao kujiuzulu, kuhamia vyama pinzani na wengine kuhama makazi yao na kwenda maeneo mengine.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo, Sodio Nyuga alisema CHADEMA kimefanikiwa kutwaa nafasi 8 za vijiji dhidi ya tatu zilizonyakuliwa na CCM.