Uchaguzi wa vijana CHADEMA (BAVICHA) taifa ni mpambano mkali

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
Nafasi ya m/kiti had sasa waliotangaza nia ni Habibu Mchange,jonh heche,Grayson nyakarungu,Silinde(mp)na Mwampamba..je ni nan kat ya hawa atakuwa mwenyekit wa vijana taifa?Uvccm ipotee kabisa kutokea hapa
 
Tunahitaji kuona cv za hao jamaa ili tuweze kutoa maoni yetu kikamilifu otherwise tunaweza kuwa biased!
 
Habari haijakamilika na umeitoa kwa haraka bila kuifanyia kazi au kuiandaa. Kama ulitaka kureport uchaguzi wa Bavicha basi ungeweka taarifa kamili. Wagombea hujui hata majina yao kamili. Na uchaguzi ni wa Mwenyekiti peke yake? Kwa nini usiweke wagombea wa nafasi zote na cv zao au sifa zao? Kama huna waombe wenye kuhusika.

Huwezi ukapata mchango wowote wa kuridhisha kuhusu wagombea au uchaguzi huo kwa taarifa kama hii.

Nakushauri kama mwanachadema please revisit your thread and if you agree go back, put on a shirt before putting on a tie and come back.

Otherwise, any and all can win the elections.
 
Mie naweza sema kuwa kati ya wote hapo grayson anafaa kuwa mwenyekiti wa vijana wa CDM bavicha ,henche ni mhuni ndiyo yeye wakishirikiana na kafulila by then waliharibu uchaguzi uliopita kwa kuongeza idadi ya kura na kutaka kupigana hawatufai, grayson ni kijana msomi asiye na makundi ndani ya chama na ni kijana msomi mwenye taaluma ya udaktari.
Mbunge wa Mbozi bwana silinde yeye kwa sasa ningemshauri hizo nafasi awaachie vijana yeye ameshavuka hiyo level ajikite kuwatumikia wapiga kura wake na kujenga mtandao mkuu wa chama jimboni na mkoa mzima wa mbeya yeye kama mbunge awaachie maunderground wafanye hiyo kazi
 
Habari haijakamilika na umeitoa kwa haraka bila kuifanyia kazi au kuiandaa. Kama ulitaka kureport uchaguzi wa Bavicha basi ungeweka taarifa kamili. Wagombea hujui hata majina yao kamili. Na uchaguzi ni wa Mwenyekiti peke yake? Kwa nini usiweke wagombea wa nafasi zote na cv zao au sifa zao? Kama huna waombe wenye kuhusika.

Huwezi ukapata mchango wowote wa kuridhisha kuhusu wagombea au uchaguzi huo kwa taarifa kama hii.

Nakushauri kama mwanachadema please revisit your thread and if you agree go back, put on a shirt before putting on a tie and come back.

Otherwise, any and all can win the elections.
mgombea jamaa hajakutaja hapo wakati nawe ni mmoja wao
 
Sina background zao na niko familiar na majina mawili-john heche na silinde so no comments.
 
Kipipili, sigombei nafasi yoyote kamanda na siko kwenye timu ya mgombea yeyote. Miaka 32 ujana ushasogea! Hatua za mwishoni!
 
au ni moja ya mbinu za hao wagombea kuanzisha thread hii ili ajipigie campain??
 
Nadhani Grayson anafaa zaidi coz ni kijana asiye na makundi, msomi na mchapa kazi, kizuri zaidi atapata muda wa kutekeleza majukumu yake. Silinde ni mzuri zaidi bt kwa sasa angeachana na hyo nafasi na aongeze jitihada ktk kuleta maendeleo jimboni mwake, wananchi wanamhitaji zaidi yetu sisi vijana. Mchange Habibu yeye bado sana, ndio kwanza yupo chuo mwaka wa pili so huyu hajasettle ila ni kijana mdogo mwenye uelewa mkubwa wa siasa! All in all CDM watuletee KIONGOZI MAKINI NA MCHAPA KAZI.
 
Habari imekuja nusunusu kiasi kwamba ukichangia unaweza kujikuta umepoteza hebu nijuzeni uchaguzi huo utakuwa lini?
 
hii habari imekondeana haioneshi uhalisia wa uwepo wa huo uchaguzi

tushawishi ili tumwage comments za kutosha.
 
Ili kuvuruga udini,kura yangu kwa mchange,japo anayefaa kuliko wote ni clinde.Akichukua Mchange,ccm watabaki na sera gani?
 
Nafasi ya m/kiti had sasa waliotangaza nia ni Habibu Mchange,jonh heche,Grayson nyakarungu,Silinde(mp)na Mwampamba..je ni nan kat ya hawa atakuwa mwenyekit wa vijana taifa?Uvccm ipotee kabisa kutokea hapa

Huyo RED CV yake ikoje, Taarifa za kiinteligencia zikamiliswe. Tunahitaji CV za huyu.:juggle:
 
tunahitaji viongozi na sio watawala,tunahitaji viongozi watakao kuwa na uchu wa maendeleo na mabadiliko,tunahitaji kiongozi atakaye sikiliza matatizo ya wanachama na kujaribu kuyatafutia ufumbuzi,tunahitaji viongozi wasikivu,tunahitaji viongozi wasio ogopa kelele za makamba na chama chake na wasiopenda rushwa

tuna hitaji viongozi wataka tutoa hapa tulipo na kutupeleka pale

tunawataki chaguzi njema
 
mwanzisha thread. hujatuambia fomu za kujaza wanaotaka kugombea zilianza kutolewa lini?

this excersise is very serious. Tunavyozungumzia BAVICHA tunazungumzia kisima cha uongozi na dira ya taifa kwa sasa na miaka mingi ijayo.

isichukuliwe ki lelemama. high level scrunity is also a requirement! Bavicha ya sasa inahitaji mtu makini sana ambaye hata akiwkewa lundo la hela atabakia kuwa dhabiti kwa chama na nchi yake!

unless otherwise, tunashukuru kutukumbusha hili, ngoja na sie tuanze kuwahimiza vijana wetu kuwa alert kwani uchaguzi uko karibu sana.
 
Back
Top Bottom