Uchaguzi mkuu Bavicha: Ni mpambano wa Alphonce Lusako na Mdude Nyagali

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Ni mpambano mkali. Ndivyo tunavyoweza kusema ukitizama watia nia wanaogombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bavicha Taifa.

Baraza la Vijana Chadema BAVICHA ndicho chombo kikuu kinachowasemea vijana si ndani ya chama tu bali Taifa kwa ujumla.

Pia Baraza hili limekuwa likiwapika vijana kuwa viongozi bora wa baadaye. Mfano mzuri viongozi kadhaa maarufu ndani na nje ya Chadema wamepikwa na Baraza hili wakiwemo John Mnyika, John Heche, David Silinde, Zitto Kabwe, Halima Mdee na wengineo wengi.

Katika uchaguzi mkuu wa Bavicha mwaka huu unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni yapo majina mawili makubwa yamejitokeza. Alphonce Lusako na Mdude Nyagali.

Vijana hawa wawili wana historia tofauti na uaminifu wao ndani ya chama. Alphonce Lusako ni mwanaharakati wa muda mrefu aliyefukuzwa mara kadhaa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kutoka na kuhusishwa na kuandaa migomo kadhaa ya kutetea wanafunzi na mpaka sasa amekifungulia mashtaka Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa kumpora haki yake ya kusoma.

Pia ni alikuwa mratibu wa Chadema Students Organisation CHASO. Pia alikuwa mgombea nafasi ya Katibu Mkuu Bavicha kwenye uchaguzi wa 2014. Kwa sasa anafanya kazi na Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu Tanzania - LHRC

Mdude Nyagali yeye anafahamika kama mwanaharakati wa muda mrefu wa haki za binadamu ndani ya Chadema anayepigania maslahi ya watu wote.

Kutokana na uaminifu wake usiyoyumba ndani ya chama Mdude amewahi kukamatwa mara kadhaa na kuwekwa ndani kwa muda mrefu na kuachiwa huku akifunguliwa kesi kadhaa.

Pia Mdude ameshiriki kwa muda mrefu zoezi la Chadema ni msingi kanda ya Nyasa na kuingiza maelfu ya wanachama wapya.

Vyovyote itakavyokuwa lakini vijana hawa ni hazina kubwa ndani ya Chadema na yeyote atakayedhinda itakuwa ni manufaa makubwa kwa chama na vijana kwa ujumla.

Attachments

  • VID-20191130-WA0080.mp4
    13.3 MB
Tunahitaji Vijana wa namna hiyo wenye Uchungu na Nchi na si Uchungu na WanaChadema.
Tofauti ya Chadema na CcM ni Kuwa CCM inawatambua wanaCCM kana kwamba ndiyo wenye haki na Tanzania hali Chadema inatambua Watanzania Kuwa Wawe na Haki, Uhuru, Maendeleo na Demokrasia Kiujumla.
Big ub Vijana Wetu, tuko Pamoja.
 
mkuu..naomba cv ya mdude Nyagali.amesoma wapi,amewahi kushika nyadhifa gani ndani ya chadema etc..
 
Tunahitaji Vijana wa namna hiyo wenye Uchungu na Nchi na si Uchungu na WanaChadema.
Tofauti ya Chadema na CcM ni Kuwa CCM inawatambua wanaCCM kana kwamba ndiyo wenye haki na Tanzania hali Chadema inatambua Watanzania Kuwa Wawe na Haki, Uhuru, Maendeleo na Demokrasia Kiujumla.
Big ub Vijana Wetu, tuko Pamoja.
Kwa kweli hawa vijana wanatutia moyo kwamba Taifa letu bado linao vijana wa kujivunia
 
Ni mpambano mkali. Ndivyo tunavyoweza kusema ukitizama watia nia wanaogombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bavicha Taifa.

Baraza la Vijana Chadema BAVICHA ndicho chombo kikuu kinachowasemea vijana si ndani ya chama tu bali Taifa kwa ujumla.

Pia Baraza hili limekuwa likiwapika vijana kuwa viongozi bora wa baadaye. Mfano mzuri viongozi kadhaa maarufu ndani na nje ya Chadema wamepikwa na Baraza hili wakiwemo John Mnyika, John Heche, David Silinde, Zitto Kabwe, Halima Mdee na wengineo wengi.

Katika uchaguzi mkuu wa Bavicha mwaka huu unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni yapo majina mawili makubwa yamejitokeza. Alphonce Lusako na Mdude Nyagali.

Vijana hawa wawili wana historia tofauti na uaminifu wao ndani ya chama. Alphonce Lusako ni mwanaharakati wa muda mrefu aliyefukuzwa mara kadhaa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kutoka na kuhusishwa na kuandaa migomo kadhaa ya kutetea wanafunzi na mpaka sasa amekifungulia mashtaka Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa kumpora haki yake ya kusoma.

Pia ni alikuwa mratibu wa Chadema Students Organisation CHASO. Pia alikuwa mgombea nafasi ya Katibu Mkuu Bavicha kwenye uchaguzi wa 2014. Kwa sasa anafanya kazi na Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu Tanzania - LHRC

Mdude Nyagali yeye anafahamika kama mwanaharakati wa muda mrefu wa haki za binadamu ndani ya Chadema anayepigania maslahi ya watu wote.

Kutokana na uaminifu wake usiyoyumba ndani ya chama Mdude amewahi kukamatwa mara kadhaa na kuwekwa ndani kwa muda mrefu na kuachiwa huku akifunguliwa kesi kadhaa.

Pia Mdude ameshiriki kwa muda mrefu zoezi la Chadema ni msingi kanda ya Nyasa na kuingiza maelfu ya wanachama wapya.

Vyovyote itakavyokuwa lakini vijana hawa ni hazina kubwa ndani ya Chadema na yeyote atakayedhinda itakuwa ni manufaa makubwa kwa chama na vijana kwa ujumla.

View attachment 1276988
Huyu dogo anachekesha sana huwa anajirekodi kwenye mitandao akijiita mwanaharakati huru.Pathetic.
 
Naona kama mdude ni balaa zaidi we mtu anatekwa na shetani bado hakomi.
 
Back
Top Bottom