Uchaguzi wa Serikali za mitaa kufanyika Disemba 14, 2014

Uchaguzi wa Serikali za mitaa kufanyika Disemba 14, 2014

Mungi

JF Gold Member
Joined
Sep 23, 2010
Posts
16,975
Reaction score
9,580
Serikali kupitia ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI imetangaza kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika tarehe 14 Desemba 2014, na kampeni zinaanza Novemba 30, 2014.

Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI ya Septemba 13, 2014 imeeleza kuwa taratibu zaidi zitatolewa kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi huo.

Hatimaye Serikali imetangaza kuwa Desemba 14 itakuwa siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Tangazo hilo lililotolewa jana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, linasema kuwa maandalizi ya uchaguzi huo yalikuwa yakitegemea matokeo ya mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya.

"Katika hatua iliyofikiwa hadi sasa, shughuli za Uchaguzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa hazitaathiriwa na matokeo ya mwisho ya mchakato wa Katiba," linasema tangazo hilo.

Tangazo hilo limekuja siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kukutana na Vyama vya Siasa vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na kuafikiana kuahirishwa kwa Bunge Maalumu Oktoba 4 mwaka huu.

Kwa kujibu wa tangazo lililotolewa, uchaguzi utafanyika katika ngazi za mtaa, kijiji na kitongoji Tanzania Bara kwa ajili ya kuwachagua wenyeviti na wajumbe wa Serikali za vijiji na kamati za mitaa.

Pia, linaeleza kuwa uchaguzi huo utafanyika kwa kuzingatia masharti ya Sheria za Serikali za Mitaa na Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambazo zimetungwa baada ya kuwashirikisha wadau mbalimbali vikiwamo vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, Azaki na wadau mbalimbali.

Ratiba ya uchaguzi inaonyesha kuwa Waziri ataanza kwa kutoa tangazo la uchaguzi, lililoandaliwa kwa ajili ya kuwasilishwa kwa waziri mhusika mwenye dhamana na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Msimamizi wa uchaguzi atatangaza mipaka ya mitaa, vijiji na vitongoji siku 50 kabla ya siku ya uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni ya (6) ya Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za mitaa, vijiji, vitongoji za mwaka 2014.

Itafuatiwa na wasimamizi wa uchaguzi kuteua majina ya wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi mara baada ya kusambazwa kwa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Kisha wasimamizi wa uchaguzi watatoa maelekezo ya uchaguzi siku zisizopungua 28 kabla ya siku ya uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni ya 7(1), 8(1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, ngazi ya vijiji, vitongoji na mitaa za mwaka 2014.

Mwisho, Msimamizi wa Uchaguzi atateua Ofisa wa Umma mwenye sifa na uadilifu ambaye ataandikisha na kuandaa orodha ya wapigakura siku 21 kabla ya siku ya uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni ya 8 na 9 ya Kanuni za Uchaguzi wa viongozi wa mamlaka za Serikali za Mitaa za mwaka 2014.

Chanzo:
Mwananchi
 
Kikosi cha CCM kipo tayari kwa uchaguzi hata tukiamshwa saa 8 usiku, mtachezea sana za mbavu Ufipa
 
Wakuu
Serikali imetangaza uchaguzi wa serikali za mitaa ni 14/12/2014.Hii ni fursa kwa viongozi wote wapya #Chadema na kampeni zinaanza tarehe 01/12/2014.

Naomba sana hili zoezi lisiwe tu kwa viongozi bali kwa kila Mwana Chadema, maana hili ndio kaburi la maccm let's go
field.

KIPENGA cha kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa, kinatarajiwa kupulizwa Novemba 30 mwaka huu na uchaguzi kufanyika Desemba 14 chini ya sheria zilizopo.

Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), iliyotumwa katika vyombo vya habari jana, ilifafanua kuwa uchaguzi huo utafanyika kwa kuzingatia masharti ya sheria za serikali za mitaa na kanuni za uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, sheria hizo zimetungwa na ofisi yake, baada ya kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, asasi za kiraia na wadau mbalimbali.

Kwa uamuzi huo, wagombea wa nafasi zinazowaniwa za mwenyekiti wa mtaa, kijiji na kitongoji na nafasi za ujumbe wa serikali za vijiji na kamati za mitaa, wametakiwa wawe wanachama na wadhaminiwe na chama cha siasa chenye usajili wa kudumu.

Ratiba

Katika ratiba iliyotolewa sambamba na taarifa hiyo, wasimamizi wa uchaguzi wameelekezwa kutoa tangazo la majina na mipaka ya mitaa, vijiji na vitongoji, siku 50 kabla ya siku ya uchaguzi kwa kuzingatia Kanuni ya 6 ya Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, ngazi ya vijiji, vitongoji na mitaa ya mwaka 2014.

Baada ya hatua hiyo, wasimamizi hao wa uchaguzi watateua majina ya wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi mara baada ya kusambazwa kwa kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa.

Katika eneo lake, msimamizi wa uchaguzi atatoa maelekezo ya uchaguzi siku zisizopungua 28 kabla ya siku ya uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni ya 7(1), 8(1) ya kanuni za uchaguzi wa viongozi wa mamlaka za serikali za mitaa, ngazi ya vijiji, vitongoji na mitaa za mwaka 2014.

Aidha msimamizi wa uchaguzi atateua ofisa wa umma mwenye sifa na uadilifu, atakayeandikisha na kuandaa orodha ya wapiga kura siku 21 kabla ya siku ya uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni 8 na 9 ya Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa za mwaka 2014.

Uteuzi wagombea Baada ya hatua zote hizo za awali kufanyika, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi atabandika orodha ya wapiga kura mahali pa matangazo ya uchaguzi na kutunza kumbukumbu zake, baada ya kusambazwa kwa kanuni za uchaguzi na kufanya uteuzi wa wagombea siku zisizopungua 20 kabla ya siku ya uchaguzi.

Ratiba iliyotolewa pia inaonesha kwamba Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, katika muda wa siku mbili tangu siku ya uteuzi kufanyika, atasikiliza na kutoa uamuzi katika muda usiozidi siku mbili kwa mapingamizi mbalimbali, kuanzia siku ya kupokea pingamizi husika.

Aidha kutakuwepo na Kamati ya Rufaa, ambayo wajumbe wake watateuliwa na Katibu Tawala wa Mkoa na katika uteuzi wake, Katibu Tawala atazingatia hali halisi ya watumishi wa umma walioko katika wilaya husika.

Kamati hiyo ya Rufaa, itateuliwa siku saba kabla ya siku za uteuzi wa wagombea kwa mujibu wa Kanuni ya 16(4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa za mwaka 2014.

Kampeni

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, kampeni za uchaguzi zitafanyika wiki mbili za mwisho kabla ya siku ya uchaguzi na zitafanyika kwa muda wa siku 14 na zitamalizika siku moja kabla ya siku ya uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za mwaka 2014.

Ili kufanikisha uchaguzi huo, wananchi wametakiwa kujiandikisha katika Rejista ya Wapigakura, itakayoandaliwa siku ishirini na moja kabla ya siku ya uchaguzi; na uchaguzi utafanywa kwa kutumia karatasi maalumu za kupigia kura.

Aidha kura zitapigwa na kutumbukizwa kwenye masanduku ya kupigia kura na kama kawaida, uchaguzi utafanyika katika ngazi ya kitongoji na mitaa katika sehemu ya faragha na hakutakuwa na mikutano ya uchaguzi katika ngazi za vijiji.

Uchaguzi uliopita Katika uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa, CCM kilipata ushindi wa kishindo wa zaidi ya asilimia 90 ya kura zote zilizopigwa, hatua iliyochukuliwa na wachambuzi wengi kuwa ni dalili kuwa chama hicho kilikuwa kinakwenda kushinda Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Uchaguzi wa mwaka huu, mbali na kuendelea kutumika kutoa ishara za uchaguzi mkuu ujao, pia utakuwa na umuhimu wa ziada katika kupima uimara wa makubaliano ya vyama vikubwa vya siasa, vilivyounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakati wa mchakato wa Katiba mpya na kukubalika kwao kwa wananchi.

Tayari viongozi wa vyama hivyo, Chadema, CUF na NCCRMageuzi, walishatoa kauli ya kuhoji kwa nini uchaguzi huo unachelewa, wakihofia kuwepo wanachoita mchezo mchafu wa kuwashitukiza.

Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe, alinukuliwa akidai Serikali imeshindwa kutangaza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo, lakini pamoja na hitilafu hiyo, chama hicho kimeshatoa taarifa kwa wanachama wake kujiandaa kugombea.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya, alinukuliwa akidai kwa kuwa uchaguzi huo hufanyika Septemba kila mara na kwa kuwa mwaka huu kuna Bunge Maalumu la Katiba linalomalizika Oktoba, Serikali ilitakiwa kulitambua hilo na kutoa ratiba mapema.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Chadema, John Mnyika alisema kutokana na mchakato wa kupata Katiba mpya kusuasua, vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi vinatakiwa kushirikiana ili kushinda viti vingi.

Chanzo: Habari leo
 
Serikali hii kiziwi ya Chama dhaifu cha Mapinduzi, imetangaza Tarehe 14/12/2014 kuwa yawezekana ndio itakayokuwa Tarehe rasmi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa hapa Nchini.

Pia wamesema Kampeni zitaanza rasmi Tarehe 01/12/2014, hivyo basi;

Ninakwenda Jimboni kwetu
rasmi kama Katibu wa BAVICHA ngazi ya Wilaya, ili kusaidiana na viongozi wenzangu katika harakati za ukombozi wa pili wa Taifa letu kupitia chaguzi hizi, kwa sababu naamini ushindi wa leo 2014 ndani ya chaguzi hizi za Serikali za mitaa, ndio utakaoakisi matokeo ya Uchaguzi Mkuu ujao wa 2014.

Ninakwenda Katani kwetu
rasmi kama Katibu Mwenezi wa Chama ngazi ya Kata yetu, ili kuhakikisha kwamba jukumu la kuufanikisha ushindi wa kishindo linakwenda vizuri kama litakavyopangwa.

Ninakwenda Kijijini kwetu
rasmi kama Mlezi wa Tawi letu la Nyumbani, ili kuhakikisha kwamba, nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji na Vitongoji vyote vitatu, vinaongozwa na CHADEMA, hata kama CCM na vibaraka wao hawapendi iwe hivyo.

Natoa rai kwa vijana wenzangu na makamanda wote tuliopo mbali na maeneo yetu ya Nyumbani, hususani kwetu sisi tuliotokea maeneo ya kule vijijini ambako CCM na vibaraka wao wanaamini kuna mtaji wao wa kuendelea kuitawala Nchi hii kibabe na kidikteta kama wafanyavyo leo.

Twendeni huko makwetu tukawaamshe Ndugu, Jamaa na marafiki zetu ili watusaidie kuliua hili Joka liitwalo CCM 2014/2015.

Na;
Francis Boniface Marwa

Ahsanteni sana!!!
 
Back
Top Bottom