Uchaguzi wa Serikali za mitaa hoi

Ulimbo

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
3,767
4,035
Pamoja na viongozi wa serikali na vyombo vya habari kuhimiza wananchi wakajiandikishe kwa ajili ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, wanachi wengi hawakujitokeza kufanya hivyo, sijui ni kwamba hawajui humuhimu wa kupiga kura au wameshagudua kuwa matokeo/viongozi wameshapangwa na hatakama watapiga kura yule aliyepangwa ndiye atapita hata kama ajachaguliwa. Naombeni mwenye datas jamaini.
 
Mkuu Ulimbo,

Hii wala haihitaji data. Watanzania walio wengi wamekata tamaa, ni ni ishara ya kuwa mambo mengi hayaendi kama walivyotarajia hivyo wengi hata umuhimu wa kura kwa sasa hawauoni. Viongozi wa dini wanapotoa nyaraka kuhamasisha watanzania waone umuhimu wa kupiga kura na watofautishe vipi matapeli wa kisiasa na wazalendo wa kisiasa wanapigwa mikwara kwani wanaonekana kuziba mianya ya rushwa na ubadhirifu wa wachache wanaojiona wana haki ya kuiendesha nchi hii wanavyotaka...

Nchi imetekwa, watanzania wanajua lakini naamini muda si mrefu, hauzidi 10yrs toka sasa itakombolewa tu! Tutawashughulikia mmoja baada ya mwingine...
 
Wewe Invisible ulivyosema kipindi cha ukombozi hakizidi miaka 10 umenifanya nikate tamaa zaidi... ningelipenda iwe ndani ya miaka 6 ijayo!!
 
Wewe Invisible ulivyosema kipindi cha ukombozi hakizidi miaka 10 umenifanya nikate tamaa zaidi... ningelipenda iwe ndani ya miaka 6 ijayo!!
Bado unamaanisha kile nilichosema... Kipindi hicho hakizidi miaka 10! Tutafanikiwa, tushaumia, tunaumia na tutaumia lakini kuna siku maumivu yatapata dawa. Siku si nyingi!
 
Sasa jamani kama wananchi ndo wenye kura, na wamekataa kujitokeza pamoja na kwamba JK alipigia dembe kujiandikisha, serekali inabidi ijichunguze kulikoni na si tu kuwaburuza watu, itafika siku hata kura za madiwani, wabunge na rais wananchi hawatajiandukisha. Pembe najua ni wachache sana watachagua serikali ya CCM, najaribu kufikiri watu wa kipawa na Loliondo watafanyaje kwani Serikali hii haiwadhamini kabisaaaaaaaaa!!!!!!
 
'...Tanzania is like a new-land, a jungle; no one is in there to take control of that wilderness. Even those who were considered survivors of the disaster, are no longer seen! What a tragedy! However, I still have hope; soon it will be discovered and recovered back. very soon'-Sanga, J.S (2009)
 
Mbona mnatuchanganya? si mlituambia hapa matokeo ya chaguzi za Kiteto, Tarime, Busanda na Biharamulo yanaonyesha watanzania wameamka na sasa wapo tayari kwa mabadiliko, iweje leo mnatuambia watanzania hao hao wamekata tamaa?

Mimi nadhani wananchi wameshastukia komedi za Chadema na genge ala "wapiganaji" na sasa wanafungamana na chama dume. kilichobaki msubiri kipigo kitakatifu tu. So far almost 10% ya wagombea wa CCM hawana mpinzania katika ngazi mbalimbali za chaguzi za mitaa na vitongoji.

Na bado mtalalama sana mwaka huu
 
Huu ni ule msumari wa Mzee Yusufu
 
Ndo kusema kutojiandikisha ni mbinu ya CCM kuwafanya watu wasijitokeze, na kama ndivyo, basi hatuna viongozi.
 
mimi nina interests na kata za Kariakoo ndio muhimu kwangu huko kwingine wacha mafisadi wagombee
 
Wananchi wanaona viongozi wao ni wasanii tu ndio maana wamekata tamaa hawaoni faida ya kujiandikisha kupiga kura wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa;serikali inawahadaa wananchi kwa kupinga kuwa na wagombea binafsi hata pale mahakama iliporuhusu kwa hiyo wananchi wanaona kuwa serikali hii haithamini matakwa ya wananchi wake na hivyo basi hakuna maana ya kujiandikisha wala kupiga kura!
 
Mbona mnatuchanganya? si mlituambia hapa matokeo ya chaguzi za Kiteto, Tarime, Busanda na Biharamulo yanaonyesha watanzania wameamka na sasa wapo tayari kwa mabadiliko, iweje leo mnatuambia watanzania hao hao wamekata tamaa?

Mimi nadhani wananchi wameshastukia komedi za Chadema na genge ala "wapiganaji" na sasa wanafungamana na chama dume. kilichobaki msubiri kipigo kitakatifu tu. So far almost 10% ya wagombea wa CCM hawana mpinzania katika ngazi mbalimbali za chaguzi za mitaa na vitongoji.

Na bado mtalalama sana mwaka huu

we kweli masatu..kama chadema ni komedi basi li CCM lenu na JK ni FUTUHI orojino
 
Tukubali kuwa elimu ya uraia Tanzania iko chini mno, ni watu wachache sana wanaojua ni kitu gani kinaendelea hivi sana. Hawajui umuhimu wa nafasi ambazo zinagombewa sasa hivi. Unaanza kuhamasisha watu wajiandikishe wakati muda wa kutaka kugombea unakaribia kwisha, sioni mantiki ya hilo.Nadhani wangeanza kuwaelimisha watu umuhimu wa kugombea nafasi hizo na baadaye kuwaambia watu wengine wajiandikishe kupiga kura na sio vinginevyo.
 
Back
Top Bottom