Uchaguzi wa marudio Zanzibar February 29, 2016

Uchaguzi wa marudio Zanzibar February 29, 2016

Kinachoendelea huko Zanzibar ni serikali ya CCM kuendesha mambo yake kibabe.
Siku ambayo Jecha alitoa tamko lake la kuufuta huo uchaguzi katika ZBC tena kwa kutumia mkanda uliorikodiwa, mimi mwenyewe nilimsikiliza.
Hakuna hata sebemu moja ambapo ali-quote Ibara yoyote ya Katiba ya Zanzibar au ku-quote kifungu chochote cha Zanzibar Electoral Commission Act, zaidi sana alikuwa akirudia rudia kwa kusema kuwa anatoa tamko hilo kutokana na mamlaka aliyopewa kisheria bila kufafanua ni vifungu vipi hivyo vya kisheria vinavyompa mamlaka hayo.
Ni dhahiri basi kuwa mamlaka hayo aliyokuwa anadai anayo ni yale aliyopewa na 'kurubuniwa' na viongozi wahafidhina wa CCM ambao 'walimzuzua' kuwa mamlaka hayo anayo!
Na ndiyo maana tokea atoe tamko hilo ambalo hata viongozi hao wa CCM wanalijua kuwa ni batili, wamemkimbiza na kumficha mahali kusikojulikana 'Kivuitu' huyo wa Zanzibar.

wadanganyika wataendelea kuwa maskini milele.kama watakubali kutawaliwa na akili ndogo kama hizi za kukimbilia kufuta matokeo.hii inaonyesha uwezo mdogo wa viongozi kufikiri.kama kuwanyang'a CUF ushindi mbinu ziko nyingi lakini sio kufuta uchaguzi.hili ccm wamekosea sana
 
Sasa kama serikali yetu itaamua kutumia ubabe katika mambo ambayo wanajua wazi kuwa 'wameteleza' basi Taifa letu muda si mrefu litaorodheshwa kuwa miongoni ya nchi zinazoendesha utawala wake kidikteta.
Nchi yetu ni ya kidicteta toka mdamrefu mrefu sana
 
Hii habari inapingana na ile ya gazeti la serikali ya zanzibar kuwa uchaguzi utarejewa tar 13 Dec.


Sent from mTalk
 
Hao RAIA tanzania..bado wanaendeleza njaa zao,wasubili kidogo ukuu wa mikoa na wilaya au kurugenzi ya mawasiliano ikulu ipo wazi kea sasa.
 
Mikwara miiingi,wapiga kura ni wale wale sefu kama kashinda kihalali anaogopa mini kurudiwa uchaguzi?uchaguzi utarudiwa na hakuna yoyote wa kuleta machafuko.
Jecha kasema kafuta uchaguzi kwa vifungu na kavitaja,mnao hororoja tajeni vifungu vilivyokiukwa muende mahakamani mkafungue shauri la kikatiba badala ya kutishana mitandaoni

Hii inawezekana Tanzania tu. Mawakala wa chama kilichoshindwa uchaguzi (ccm) walisaini matokeo yote bila malalamiko lakini tume ndio inalalamika kwa niaba ya ccm na kudai kuwa uchaguzi haukuwa huru na wa haki. kwa upande wa bara chadema walipinga matokeo yasiendelee kutangazwa kwa kuwa yana kasoro lakini hakuna aliyesikiliza hoja yao. kama ushindi wa ccm bara ulikuwa halali wanaogopa nini kuchunguzwa kwa matokeo ya uchaguzi? mbona ccm mnang'ang'ania uchaguzi wa zanzibar urudiwe lakini hamtaki wa bara urudiwe? SASA IMEJIONESHA WAZI KUWA NEC NA ZEC NI WADAU WA CCM.
 
Inchi inayotawaliwa na mashetani na wachawi haya ndio matokeo yake. The soln is to take these devils down one by one, the nation will be healed.
 
Back
Top Bottom