Uchaguzi wa marudio Zanzibar February 29, 2016

Uchaguzi wa marudio Zanzibar February 29, 2016

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,728
Reaction score
62,878
Gazeti la RAIA Tanzania limeripoti kuwa uchaguzi wa marudio Zanzibar umepangwa February 29 mwaka ujao.
 
Wao wametoa wapi habari hii? Kama source ya habari ya ni yamkini wafungiwe. Nadhani kwa ustaarabu wa Maalim Seif amekubali kufanya mazungumzo na kada mbalimbali ili kupata maridhiano. Kama mambo yatalazimishwa ina maana kwa yatakayotokea ni laana kwa ZEC
 
Gazeti la RAIA Tanzania limeripoti kuwa uchaguzi wa marudio Zanzibar umepangwa February 29 mwaka ujao.
Uchaguzi wa Zanzibar ulifanyika tarehe 25/10/2015 na hakuna chama chochote kilichotoa malalamiko yake kwenye chombo cha sheria cha mahakama kuu inayohusika kusikiliza malalamiko ya aina hiyo.
Kwa hiyo kitendo cha Mwenyekiti wa ZEC Jecha kuufuta uchaguzi huo tena hata bila ya kuwashirikisha makamishna wenziwe wa ZEC, ni uvunjaji wa dhahiri wa Katiba ya Zanzibar na sheria za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
Kwa hiyo solution pekee ya kutoka kwenye mkwamo huo wa kisiasa wa Zanzibar ni Tume hiyo ya Uchaguzi kuendelea kutangaza matokeo yaliyosalia na hatimaye kumtangaza mshindi wa kiti cha Urais wa Zanzibar.
Kitendo cha wahafidhina ndani ya CCM kulazimisha kutaka uchaguzi huo urejewe huku wakijuwa fika kuwa huo ni uvunjaji wa wazi wa Katiba ya Zanzibar waliyoapa kuilinda, kitaleta mtafaruku mkubwa wa kisiasa ambao haujawahi kutokea ndani ya nchi hii tokea tupate uhuru wetu toka kwa mkoloni zaidi ya miaka 50 iliyopita.
 
Kwa kadri mambo yanavyoendelea huko Zanzibar ambapo mshindi wa kiti cha Urais, watawala wa huko wameizuia ZEC isimtangaze, ni vyema tu hao watawala wetu wa CCM wakajitokeza hadharani na kuutangazia Umma wa watanzania na dunia kwa ujumla kuwa nchi hii ingawa imejitangaza kuwa inafuata mfumo wa vyama vingi, lakini PRACTICALLY 'wanaoruhusiwa' kupokezana vijiti vya Urais ni wanaccm peke yao!
 
CCM wanacheza na saikolojia ya muda ila ninauhakika Maalim Seif atatangazwa rais ni muda tu.
 
Huu uhuni unaofanywa na CCM haukubaliki na kila mwanadamu mstaarabu anaeamini ktk haki, yafaa CCM wakabidhi madaraka kwa mshindi halali
 
mmmh kama ni kweli aiseee dah tutaona itakuwaje, yangu macho tu, zanzibzr Mungu aibariki isipate machafuko,
 
Gazeti la RAIA Tanzania limeripoti kuwa uchaguzi wa marudio Zanzibar umepangwa February 29 mwaka ujao.

Naapa sina muda mchafu wa kupanga foleni na kupiga kura.yaani lijitu lijiamulie kufuta uchaguzi lisumbue na kuharibu ratiba za watu nyambaaaaaa......f....u
 
Kwa kifupi hatupo kwenye utawala wa kidemokrasia bali utawala wa mabavu chini ya viongozi wa ccm. Ccm haiwakilishi wananchi hata kidogo. Wazanzibar wanapaswa kudai haki ya kusikilizwa kama walivyofanya 1964. Viongozi wa ccm wakishtakiwa icc ndio tutapata tume huru na katiba mpya.
 
Ushauri mwingine kwa wabunge wa upinzani kwenye kikao kinachoanza Jumanne ya wiki ijayo huko Dodoma ni kuwa baada tu ya zoezi la kumpata Spika mpya, wasiruhusu suala lingine lijadidiliwe bungeni hapo zaidi ya mkwamo wa kisiasa huko Zanzibar.
Wasikubali hata kidogo ombi lao hilo la kujadiliwa suala hili la Zanzibar lipigwe kumbo na Spika mpya wa Bunge na wabunge wenzake wa CCM.
Wanapaswa wajifunze na makosa wliyoyafanya siku za nyuma 'wasilogwe' hata kidogo kususia kikao hicho na badala yake wakomae humo humo bungeni hadi dakika ya mwisho.
Hata kama watawala wetu wataamua kuyaleta magari ambayo ni brand new ya 'washawasha' ya polisi bado wabunge hao tuwasihi waendelee kukomaa bungeni humo hadi pale mshindi wa kiti cha Urais wa Zanzibar kwenye uchaguzi uliofanyika tarehe 25/10/2015 atangazwe.
 
Hawawezi kushindana na serikali na kama huamini subili utajionea wakiingiza hilo jambo subili utajionea nini kinafuata
 
Kwa maana hiyo kutakuwa na ratiba tofauti za uchaguzi maana Rais wa Zanzibar muda wake utaanza pale tu atakapoapishwa.Kwa jinsi hiyo kuna na uchaguzi wa JMT na kisha wa Tanzania visiwani
 
Sheria inasema kama uchaguzi umehairishwa ( tujaalie hiyo kufutwa, japokuwa hakuna kitu hicho) basi uchaguzi utarejewa ndani ya siku 90. Sasa wanaposema uchaguzi utarejewa Feb 29, hiyo kinyume ya sheria za uchaguzi na katiba. Siku ya kufa nyani...
 
Maalim ingia kwenye kinyang'anyilo cha uchaguzi usiope kitu kama watu wanakukubali basi bado wewe utakua mshindi usiogope kitu
 
Acha ccm wacheze makede makede na taarabu nyingii ila ni suala la muda tu,,Maalim Seif atatangazwa rais wa Zanzibar
 
Maalim ingia kwenye kinyang'anyilo cha uchaguzi usiope kitu kama watu wanakukubali basi bado wewe utakua mshindi usiogope kitu

Magamba wazee wa zisipotosha watatatosheleza maalim awezi shinda watafanya ujuma zao hii ni kwa sababu bara walibanwa na ukawa wakatosheleza huku bara wakasahau Zanzibar kuja kutaka kutosheleza maalim kashatangaza kura zake ndio jecha akafanya kazi
 
Mikwara miiingi,wapiga kura ni wale wale sefu kama kashinda kihalali anaogopa mini kurudiwa uchaguzi?uchaguzi utarudiwa na hakuna yoyote wa kuleta machafuko.
Jecha kasema kafuta uchaguzi kwa vifungu na kavitaja,mnao hororoja tajeni vifungu vilivyokiukwa muende mahakamani mkafungue shauri la kikatiba badala ya kutishana mitandaoni
 
Back
Top Bottom