Unajua Mwanakiji Kuna Watu Tunao Humu Jf Lkn Akili Zao Zimeshikwa Na Mafisadi,sasa Nyie Mnaona Raha Gani Ccm Kushinda?halafu Miongoni Mwa Hao Wanaoshangilia Huo Ushindi Hata Kadi Ya Ccm Hana Sasa Si Aibu Hh,au Ndio Mnafikiri Wote Walio Hapa Jf Ni Wapinzani Wa Ccm?tuliowengi Si Wana Ccm Wala Wa Pinzani Wa Ccm,ss Tunataka Kuona Maendeleo Yanapatikana Huko Bongo.kwa Maana Nyingine Tunataka Habari Zinazowachomoa Mafisadi Katika Mashimo Yao .
Chadema wanapaswa kuondokana na upuuzi wa kudhani kuwaonyesha wananchi 'helikopta' ndio mvuto mkubwa wananchi wawape kura. If anything, this in itself should be reason enough to vote against them.
Nakubaliana na mawazo ya Mkjj. Kila uchaguzi unategemea umejipanga vipi, na ni mikakati ipi umeiweka kufanikisha azma yako ya uchaguzi. Je, unawajua vizuri wapiga kura wako? Unayajua vizuri mahitaji yao?
Huwezi kwenda tu kuomba kura kwa kelele za jukwaani. Mgombea wa Chadema alishagalagazwa mara kadhaa katika jimbo hilo hilo. Je, kabla ya kumteua tena kugombea mara nyingine, walijiuliza ni sababu zipi zilizokuwa zinamfanya ashindwe; na kama walizijua, ni yapi waliyokuwa wameyafanya safari hii ili aweze kukubalika zaidi!
Chadema, kama chama inawabidi pia wakae chini ili wajitazame upya. Their top leadership may not be inspiring enough to the wananchi.
kuna kitu ambacho hukielewi katika siasa. Tatizo la watanzania wengi wanachagua chama wala si sera. Sisemi kama wapinzani ni bora, au CCM ni bora zaidi bali ni jambo la kujiuliza huo ushindi wa CCM kiteto hutaleta maendeleo gani? Je naweza pata jibu (quantify jibu lako). Nafikiri kabla ya kushangilia huo ushindi basi vinjari wilaya ya kiteto, kisha kwa dhati kabisa usimame kushangilia huo ushindi.
Yapata 40,000 awakupiga kura! wote wamepoteza kadi hati zao kupigia kura!
Ushindi wa ccm ulitegemwa maana wanaweza kuwanunua Wtz masikini hata kwa pair moja ya kanga. naweza kuwa mzito wa kuelewa, lakini nikiona gharama za kampeni za uchaguzi ni kubwa sana. Sijui kwa nini hiyo pesa hawa CCM wetu wasifanye kweli kwa kutoa huduma kwa hawa wapiga kura wasiojua hata kura zao zinawagharimu kiasi gani.
Bado napata shida sana kuamini kama ni kweli na kwa dhati kabisa hawa ndugu zetu wa kiteto wameichagua sisiem kwa sababu wameridhika na yale inayowafanyia,na kwa hiyo wako tayari kuendelea kuvuna yale yale ambayo wamekuwa wakiyapata. Shuda yangu inapata nguvu zaidi hasa baada ya kusikia(sijathibitisha) kuwa chadema waliongoza katika maeneo ya mijini zaidi tofauti an wenzao ccm waliowekeza zaidi bush. Kama ndivyo ilivyo, basi picha inayojitokeza hapa ni kuwa aidha ccm wamekuwa wakitoa upendeleo kwa watu wa vijiji zaidi kuliko kwa wale wa town katika kuwahudumia au hawa ndugu zangu wa town ambao nadhani hawahitaji helkopta ili kuhamasika,wana chuki binafsi na ccm.
Kama kawaida yenu mmeshaanza kuchonga na lawama kibao....Dae Es Salaam watch your language.Hukatazwi kushangalia CCM lakini hapa si mahala pa kufanya mambo ya muhimu kama mpira wa miguu.Siasa hizi zinagusa maisha ya watu kabisa na si kuleta kejeli za JK kuwaita wapinzani watani wa jadi .This I find it always low .Siasa si kama mnavyo taka tuelewe.Tuongee issue hii bila kuonyesha kwamba jambo la mzaha tu.Hakuna mzaha hapa maana wana siasa ndiyo wanao amaua Watanzania wa Kiteto na kwingineko waishi vipi kwa hali .Kushindwa kupo na kushinda kupo.Lakini ningalikuwa wewe nisingaliweza kushangalia ushindi ambao hata damu za watu zimemwagika , Serikali na polisi wameingilia ka ku force ushindi .Mkuu wa Mkoa Shekifu alikuwa huko muda na yule mwingine toka Iringa nk .Tunajua CCM walitaka hili jambo to foos us kwamba wanakubalika .Kama wanakubalika basi wabadilishe vipengele vya katiba na hatimaye Tume ya Uchaguzi iwe na watu wote maana wa serikali wameshindwa kuwa wakweli bali kuibeba CCM sawa na Polisi na wengine wote .
Komba kafanya vurugu za wazi kabisa hajachukuliwa hatua hata moja lakini angalifanya Slaa ama Zitto ungalisikia matangazo na kipigo na kesi Mahakamani.Bado una akili timamu unataka kuleta suhabiki ? You can do this lakini nenda kule Tazama, IPP Media, Rai nk .
Tunakubalia Chadema kushindwa lakini isiwe ushabiki wa kijinga na kutufanya kjuongea kama sisi wote ni wapuuzi no .
Ukimuona mjanja anaipenda CCM jua yuko highly connected na UFISADI .
Ama kweli mwanakijiji leo kachanganyikiwa amefikia kutoa Thanks na lile jina lake la "mwafrika wa kike" ambapo mjadala huu halijachangia kitu. teh teh teh teh
Unajua wapinzani hawana sera hichi kibano wakizoee mpaka siku ile watakapobadirika na sera zao.
watu hatuoni kwanini wapewe CHADEMA/CUF/NCCR ambao hawafahamiki namna ya uendeshaji wao.
Maana kimantiki wapinzani hawatofautiani na CCM sasa basi kwanini ufanye majaribio ???
Mie naona udhaifu wa wapinzani ni huu mtindo wao eti kuibua uozo wa mwazako na kuufanya SERA,kuibua uozo ni vyema lakini kuufanya ndio mgongo wa kupandia ni makosa makubwa ,hii naifananisha kama mtu yule anayemtaka mwanamke kwa gia za kumuambia maovu ya mwanaume aliyenaye.Mwanaumme aliyenaye anaweza akawa muovu sana lakini wewe kupitia mgongo huo ili ufanikishe adhima yako na kama mwanamke huyo ni makini hakika hutompata.
Wapinzani kama wapo tofauti na CCM hawakuhitaji kuruka na ndege angani kupoteza fedha nyingi kwa kutangaza sera za maneno ,bali sera zao zingejitangaza zenyewe kwa kufanya hivi-
Wapinzani nendeni huko kijijini mnakoruka na madege wakati tu wa uchaguzi kafanyeni harambee/tafuteni wadhamini wapelekeni huduma ya maji,umeme.
wapinzani nendeni huko mkahamasishe watu muwaelimishe jinsi ya kufanya kilimo cha kipande kidogo na kuvuna mavuno yenye tija.
wapinzani kahamasisheni huko vijijini kwa miharambee/wadhamini watu wapate muamko wa kilimo cha kutumia matrekta.
wapinzani hamasisheni wananchi/wadhamini kujengea vyuo vikuu vingi nchini ili wananchi wapate kuelimika.
Hakika mkijitahidi hata kwa nusu ya hayo mtapata kura nyingi za tsunami ambazo hata wezi wa kura wataona aibu yenyewe na mtazipata bila jitihada zozote za kuruka na ndege angani .
Mnavyofanya saizi hamna tofauti na CCM ndio maana hatuna sababu ya kuwapa kura.
anyway wewe endelea kuchonga maana naona baada ya juhudi za kushindwa kuizima JF sasa kuna new memberz kibao wamejiunga hapa JF!
Niliwaambia mapema mtaangukia pua! pwaaa!!!!!!!!!!
..washakataa si wageni! check the pattern!
Nashindwa kuwaelewa watu ambao bado wanaipigia kura CCM.
Baada ya maskendo yote haya,je hawa watu hawaoni?
Je ni kitu gani CCM imewafanyia?
Nimechanganyikiwa !
wapinzani nendeni huko mkahamasishe watu muwaelimishe jinsi ya kufanya kilimo cha kipande kidogo na kuvuna mavuno yenye tija..