Uchaguzi uvccm vurugu tupu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi uvccm vurugu tupu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Aug 5, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Ally Salum Hapi[​IMG] (mgombea nafasi ya makam mwenyekiti taifa) TANURU LA FIKRA


  Ndugu vijana wenzangu, na watanzania wote kwa ujumla. Tangu nitangaze hatua yangu ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Makamu mkt UVCCM,nimepata pongezi nyingi kupitia simu yangu,email,mtandao wa facebook n.k toka kwa jamaa,marafiki na wana CCM wanaonifahamu ama kwa kunisikia au kufanya kazi nami. Lakini sambamba na hilo, wametokea watu wachache wenye nia mbaya ambao wao wameamua kupotosha jamii kuh... usu mimi ni nani kwa maslahi yao binafsi. Watu hawa wamekuwa wakieleza ndani ya mitandao kama Facebook kuwa mimi nimeamdaliwa na mtoto wa Rais bwana Ridhwan ili niwe Makamu mkt. Na kwamba yeye ndiye aliyenituma kuchukua fomu ya nafasi hii na kwamba nimesoma nae na nafanya kazi na mtoto huyo mkubwa wa rais Kikwete.Ningependa kusema yafuatayo kwenu :

  1. Uvumi huo ni uongo mkubwa unaolenga kunichafua, na hivyo wana CCM na watanzania wote naomba waupuuze na kuwapuuza wanaoeneza huo upotoshaji.
  2. Mimi sijaandaliwa na Ridhwani, Beno wala Hussein Bashe. Hivyo mimi si wa mtu fulani, mimi ni wa CCM na CCM ndiyo iliyonipika na kunijenga.
  3. Kama mwana CCM, naweza kuongea na yeyote ambae ni mwana CCM au kiongozi akiwemo Ridhwani Kikwete,au yeyote,kupata ushauri, au kujifunza jambo lolote.Kwa kufanya hivi hakunifanyi niwe mali ya mtu huyo wala kuvunja katiba ya CCM .
  4. Mimi sijasoma na sifanyi kazi ofisi moja na mtoto huyo wa Rais.
  5. Mimi sitoki pwani, nyumbani kwetu ni Nzega,Tabora.
  6. Sijatumwa na yeyote kuchukua fomu, ni utashi na haki yangu.
  7. Mimi si wa Ridhiwani, Bashe, Beno Malisa wala yeyote awaye, na sijawahi kutumiwa, situmiwi na sitatumiwa na yeyote kati yao, bali nitaitumikia CCM na jumuiya zake.

  Siwezi na sitakuwa kibaraka wa mtu au kikundi cha watu, siwezi kuwa mtumwa wa yeyote, awe Ridhwani au yeyote, maana kufanya hivyo ni usaliti mkubwa kwa wana CCM na watanzania wote. Mimi sihongeki, sina bei na sitakuwa nayo daima.Wala sizihitaji pesa chafu.

  Naomba muwapuuze hao wanaoeneza hayo, kwani wanahofu kubwa nami kwakua wanajua sina bei, wanajua uadilifu wangu na kuwa siwezi kuwa kibaraka wao. Nawashauri, kama wana wagombea wao waliowaandaa, wasubiri vikao vya chama vitujadili hatimaye tupimwe. Kunichafua hakutawasaidia, maana vijana wa CCM wanajua nani anawafaa,hawahitaji kusemewa. Binafsi sitawatukana wala kuwajibu hovyo, nimewapuuza. Njia ya haki ni nyoofu, na wale wanyoofu pekee ndio wataipita...
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Kazi mnayo...ngoja nijifue na fani nyingine. Siasa hizi mhhh!
   
 3. t

  thatha JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Mbio za uchaguzi UVCCM zaanza kushika kasi [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Thursday, 02 August 2012 21:02 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]digg

  Geofrey Nyang'oro
  UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umeanza kuwasha moto tena baada ya mbio za kuwania nafasi za juu za jumuiya hiyo kuanza kwa mbwembwe na tambo za aina mbalimbali.

  Wakati jana wanachama wa UVCCM walianza kuchukua fomu, mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Sango Kasera ametangaza kwamba akifanikiwa ataondoa mtindo wa watoto wa vigogo kutaka kuongoza umoja huo.

  Sango alisema anatambua kwamba UVCCM katika siku za karibuni umeweza kuwa taasisi inayoongozwa na baadhi ya watoto wa vigogo.

  Alisema akifanikiwa kushinda atahakikisha anaondoa mfumo uliojengeka na kuurejesha umoja huo katika zama zile za TANU Youth League(TYL) ambao ulikuwa ni wa watoto wa watu wote bila kujali matabaka.

  Hadi jana, majina ya wanachama waliokuwa wamechukua fomu kwa nafasi ya unyekiti ni pamoja na Thabit Jecha Kombo, Sadifa Juma Khamis na Rashid Simai Msaraka.

  Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti mbali ya Sango wengine ni Ally salum Hapi na Augustino Matefu, wakati wa Halmashauri Kuu (Nec) ni Theresia Mtewele, Halima Bulembo, Olivia Sanare, Ahmed Nyang'ani na Sango tena.

  Wengine ni Vaileth Sambilwa, Faidha Salim na Augustino Simwiya, huku kwa upande wa Baraza Kuu Taifa wagombea wakiwa ni Mteweke, Bulembo, Ester Mambali, Sanare, David Mwakiposa, Vaileth Sambilwa na Augustino Simwiya. ​
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 4. t

  thatha JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  watatoana roho wakigombania madaraka
   
 5. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,896
  Trophy Points: 280
  Kumbe ukiwa rafiki wa Ridhiwani hupati kura!!
   
 6. t

  thatha JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  ndio kawaida ya uchaguzi kuwa na patashika nguo kuraruka,kinachotakiwa ni kwamba baada ya uchaguzi walioshindwa wakubali matokeo
   
 7. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kumbe kuhusishwa na riz ni kashfa,kweli waswahili husema lisemwalo lipo.
  tutasikia mengi mpaka watu wakimkimbia mwenyekiti wao.
   
 8. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Nilifikiri Utafurahia kuwa umetumwa na Mtoto JK iwe sifa leo unakana hata mtoto wa Mwenyekiti wako wa chama basi tena kama hata Mtoto wa mwenyekiti wenu mnamkataa.
  Kumbe Baba Riz na Riz si wasafi ndio maana hutaki kuambiwa umetumwa nao? ...................Nashangaa kufiwa mikonono na ccm yenu.
   
 9. dogojanja 87

  dogojanja 87 JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 885
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Salum sio kiongozi ni mchumia tumbo,mnafiki na mwenye tamaa ya madaraka na fedha historia yake ndani ya DARUSO inadhihirisha haya yote,mbaya zaidi huwa hana msimamo na hashauliki(baba haambiliki)..UVCCM mkimchagua imekula kwenu..
   
 10. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Mtumeeeeeeee! Yaani unamkataa MTOTO WA RAIS? Kwani tatizo la Riz Kikwete ni lipo hadi umkatae wewe ambaye unagombea nafasi kwenye chama kinachoongozwa na baba yake?
   
 11. m

  malaka JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ngumi za makaburini.
   
 12. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,834
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Wewe SANGO KASERA ni sambuli ya akina Aden Rage, wanafiki wababaishaji ambao mipango huishia kama ile ya pwagu na pwaguzi tu, huna jipya . Ili maendeleo inchi yapatikane CCM inatakiwa ife izikwe kabisa.
   
 13. m

  majebere JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,521
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Ukitaka kujua CCM ni ya dini zote basi tazama hayo majina ya wagombeaji. Kweli hakuna chama zaidi ya CCM.
   
 14. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Poop on the head!
   
Loading...