Uchaguzi UVCCM vurugu tupu Arusha; Chatanda apigwa, ajificha chini ya meza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi UVCCM vurugu tupu Arusha; Chatanda apigwa, ajificha chini ya meza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by commited, Oct 11, 2012.

 1. commited

  commited JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, amenusurika kipigo baada ya kutuhumiwa kuvuruga uchaguzi wa mkoa wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) akidaiwa kutaka kumpitisha mmoja wa wagombea, Dk. Harold Adamson.

  Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa tisa alasiri wakati Chatanda ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo, alipoamuru zoezi la uchaguzi huo lirudiwe baada ya kuwa ulishafanyika, kwa madai kwamba idadi ya wajumbe kutoka wilaya za Monduli na Arumeru haikuwa sahihi.

  Hali hiyo ililazimu Jeshi la Polisi na maafisa Usalama wa Taifa kuingilia kati kuhakikisha amani inarejea ambapo polisi walioletwa kwenye gari aina ya Land Rover yenye namba za usajili PT 0746, waliamua kuwaamrisha waandishi kutoka nje ili wasione kilichokuwa kikiendelea ndani ya ukumbi huo.

  Mara baada ya hali kutulia uchaguzi huo ulirudiwa huku ulinzi ukiwa umeimarishwa na milango ya kuelekea eneo hilo ikiwa imefungwa.

  Hata hivyo vurugu hizo zinahusishwa na makundi hasimu ya urais 2015 ndani ya CCM kwani tokea chaguzi hizo zianze mkoani hapa kuanzia ngazi ya wilaya hali hiyo ilikuwa ikijidhihirisha wazi.
   
 2. m

  malaka JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Safi sana. Naona mungu kasikia kilio cha wengi.
   
 3. Simba mnyama

  Simba mnyama JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2012
  Joined: Jul 14, 2012
  Messages: 348
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tobaaaaaaaaaa! Siasa za makundi hizo.
   
 4. Z

  Zimamoto JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 464
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Waache KUNGURU WAJITAFUNE wenyewe. Wanapisha njia tupite.
   
 5. S

  SUPERXAVERY Member

  #5
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizo ni ishara kwamba chama bado imara, na watu wana uchu wa kushika madaraka katika chama.
   
 6. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,812
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  kumbe ndo maana jana niliwaona mitaa ya CCM mkoa na maeneo mengi ya mjini Arusha jana walikuwa walikuwa wanaonekana na minguo yao ya kijani. Watajiju.
   
 7. p

  propagandist Member

  #7
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kajificha chini ya meza kama wenje? wenje staili wataiiga wengi.
   
 8. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,812
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  hapo kuna uimara gani wa chama wakati watu wanagawanyika na kutaka kurithishana madaraka? We utakuwa umelewa magamba,nakushauri uyavue na uvae magwanda.
   
 9. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Siku hizi chaguzi za magamba unatakiwa uwe unapasha vuma na kuna wa mbio.. anyway Tendwa ni kipi chama chenye vurugu?
   
 10. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  watamalizana mwaka huu, alafu dhaifu anasema magamba itadumu daima kweli kuna watu wana2mia vichwa kufuga nywele!
   
 11. J

  John W. Mlacha Verified User

  #11
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  tendwwa toa tamko
   
 12. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Hivi huyo LOWASSA na mwenzie MEMBE nani kawaambia tunawataka wachukue URAIS.
   
 13. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Sasa kama walipigana na mapanga na marungu ndani ya ukumbi.Walikwenda kuwinda ama kuchagua?
   
 14. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Safi sana
   
 15. E

  EMMANUEL NSAMBI JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 402
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapo tendwa atasema ni changamoto za kisiasa.
   
 16. naninibaraka

  naninibaraka JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Huyu mama alishawahi kusema uhisiano wake na rais unaenda beyond kazi za chama na serikali,yeye,mkuu wa mkoa waliletwa kwa kazi maalumu lkn cha kushangaza mkoa wa Arusha umekuwa ngome ya kubwa ya CDM,kavuruga chaguz ili mtu anayetakiwa na Ritz 1 ashinde pamoja na kumwaga hela zote hizo bado mipango yao imekwama....
   
 17. 2hery

  2hery JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,532
  Likes Received: 2,054
  Trophy Points: 280
  wale wazee WAKISHILI bado wapo? nafikiri watamsaidia Tendwa kutoa tamko la hli
   
 18. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  CCM ndicho chama cha siasa kinachoongoza kwa vurugu kwa sasa hapa Tanzania.
   
 19. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,900
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Yale yale yaliotekea Mara ya kupeana kichapo cha mbwa mwizi tena anayeiba kuku.
   
 20. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Chitanda ni katibu mkuu wa CDM Arusha, chama ambacho ni cha vurugu, alienda kufanya nini ktk uchaguzi wa CCM?
  Mh Nape bado haujarudi toka shopping na kuishitaki CDM kwa kuleta vurugu ktk chaguzi zenu?
   
Loading...