Juma Polle apigwa chini uchaguzi Masasi, vijana wamkataa, watuma ujumbe mkoa mzima wa mtwara. Makundi na roho mbaya vyatajwa kummaliza

the horse

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
652
441
Wiki iliyopita Jumanne Julai 26, 2022 kulifanyika uchaguzi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Mijelejele Wilayani Masasi ambako Juma Polle ni Diwani wa Kata hiyo ya Mijelejele. Juma Polle aliomba nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Mkoa kutokea Kata ya Mijelejele.

Kwenye nafasi hiyo walichukua fomu watu watatu na Juma Polle alifanya kila awezalo kufanya figisu na kurubuni wenzake wawili waliochukua fomu hiyo wajiondoe ili abaki pekee yake ili ajitengenezee mazingira ya kuwa Mjumbe wa Mkutano wa UVCCM Mkoa ili akajipigie kura kwenye uchaguzi wa Vijana Mkoa wa Mtwara ambao Juma Polle amechukua fomu ya kugombea Uenyekiti wa Vijana-Mkoa wa Mtwara.

Basi bwana, baada ya kuingia Ukumbini kufanya uchaguzi na kuonekana nafasi hiyo inagombewa na mgombea mmoja tu ambaye ni Juma Polle, iliamuliwa kupigwa kwa kura za Ndiyo au Hapana ili kumthibitisha Juma Polle kwenye nafasi hiyo na kama kura za Ndiyo zikiwa nyingi basi atashinda au kama kura za Hapana zitakuwa nyingi basi nafasi hiyo itakuwa wazi.

Vijana wa Kata ya Mijelejele kwenye Mkutano huo walipiga kura 13 za Hapana kumkataa Juma Polle kushika nafasi hiyo huku wakisema hawako tayali kuongozwa na Juma Polle ambaye anasifika Mkoa mzima wa Mtwara kwa siasa za makundi, unafiki, kuchafua watu, kuumiza watu kwa kupeleka maneno ya uongo kwa Viongozi ili wenzake waharibikiwe.

Vijana wa Kata hiyo wanasema kwa muda mfupi ambao Juma Polle amekuwa Diwani amekuwa mwiba kwa Vijana wa Masasi na Mtwara mzima hasa kwa kukata fursa za Vijana, kupiga fitina kwa Vijana wengi sana ikiwemo kwa Martin Mkanga, Mwenyekiti wa Vijana Wilaya ya Masasi ambaye alifukuzwa kazi kwenye Taasisi moja ya Masasi kwa fitina za Juma Polle na watu wake.

Vijana wa Mijelejele walimkataa Juma Polle huku wakisihi Vijana wa mkoa mzima wa Mtwara kumkataa Juma Polle kwani kwa aina ya siasa zake kama atapata nafasi ataumiza wengi na kiharibu kila kitu.

FB_IMG_1659360390262.jpg
 
Bwashee mbona umeandika kiudaku sana kwa kushangilia kushindwa kwake, ni mpinzani wako nini?
Leo kwake kesho kwako!
 
Huyu kwa macho tu mbona umri wa kugombea uongozi Uvccm ameshapita? Kugombea kwenye chama anaogopa nini?

Kamati ya siasa ya wilaya na halmashauri kuu ya wilaya wanafanyakazi gani?
 
Back
Top Bottom