Uchaguzi umekwisha, tujipange kufanya mabadiliko

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,650
Yafuatayo ndo mambo muhimu ya kufanya sasa, baada ya uchaguzi, ili kuwe na mabadiliko bora na siyo mabadiliko ya kuzungusha mikono kama wana sarakasi:

1) Tubadilike kifikra kutoka kulaumu tu bali kufanya kazi. Tanzania ya Magufuli ni #kazitu.

2) Kujituma na kuwajibika kikamilifu mahala pa kazi kwa kila mmoja wetu.

3) Kuondokana na tabia ya rushwa na ufisadi pasipo kusubiri mahakama ya mafisadi.

4) Makampuni yanayochezesha bahati nasibu na mashindano ya vijana, hususani sanaa, yajikite katika kushindanisha vijana katika stadi za maisha (ususi, useremala, upishi, kilimo, gereji, nk) ili kuongeza uzalishaji na huduma zenye tija na ajira kwa vijana. Wakati mashindano ya sanaa mshindi ni mmoja, mashindano ya stadi za maisha ni kundi la vijana.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
wewe subiri tu utakachokiona na kukishuhudia; nadhani wote wanaosema "Hapa Kazi Tu" aidha watakujashangaa na kujiona kumbe wao kwa mtu mmoja mmoja ndo malofa; na wengine watapoteza hata kile kidogo walicho nacho: Tusubiri tu ndugu yangu; sote ni watz jk aliingia kwa kishindo 2005 na gia ya "Ari mpya, Nguvu Mpya, na Kasi Mpya" watu wakashangilia "Maisha bora kwa kila mtanzania" watu wakasema neema imekuja: hebu sote tujiulize je nini kimetupata watz hii miaka ya ari mpya, nguvu mpya, na kasi mpya? tembo, twiga, gesi, umeme wa mgao- nyongeza yake udini kushamiri na kwa mara ya kwanza watz kuchinjana wao kwa wao-

Leo kila mtu hap tz anasema "Hapa Kazi Tu" mie kwa udhoefu nilionao hakuna cha kujivinia chchote chini ya utawala wa ccm haijalishi ni nani rais cha msingi tuungane na tukubaliane na matokea yaliyotangazwa na tume yetu ili nchi yetu iendelee kuwa na amani- pili na la faida kwetu sote bila kujali itikadi ya vyama na dini, ukabila au rangi ni hili: kwa umoja wetu na uzalendo wetu na utaifa wetu tuungane kudai rasmu ya katiba ya mzee Warioba ndo iwe katiba yetu. hata kama swala la muungano libaki lilivyo sasa lakini tutakuwa tumefanya uzalendo mkubwa wa kuwa na katiba bora kuliko zote Africa nzima, katiba inaayomwajibisha mwenye kutawala, katiba inayompunguzia mtawala mamlaka na kuwagawia watu wa chini mamlaka ya kumwajibisha mbunge wao, waziri wao, na hata rais wao pale ambapo ameenda kinyume kwa masilahi yake.

Lakini tukibakia kusema hapa kazi tu wakati katiba yetu inamruhusu waziri, rais kufungua account nchi za nga'ambo, tena inamruhusu kubadilisha matumizi ya ardhi mda wowote na popote pale anapojisikia, tena inampa mamlaka ya kuteua maafisa waandamizi kwa ngazi zote za kitaifa, kimkoa na hata kiwilaya, halafu tutegemee hapa kazi tuu" pengine ipo siku moja sisi sote tutakubalia kwa sauti kubwa kuwa "HAPA GIZA TUU"
 
ulisha ona bibi anabadilika, ccm ni ileile mbona huelewi, unataka uambiwe na nani? hakuna mabadiliko hapa labda ujinga kupanda juu.
 
Back
Top Bottom