Uchaguzi Serikali za mtaa, CHADEMA waambulia mtaa mmoja

Uchaguzi Serikali za mtaa, CHADEMA waambulia mtaa mmoja

Jana Jumapili Jijini Dar es Salaam kulikuwa na uchaguzi wa wenyeviti wa mitaa katika mitaa mipya na ile ya zamani iliyotakiwa kujazwa nafasi, Kampeni zilikuwa kali zikijumuisha viongozi wa vyama vyote, hasa Chadema waliowatuma wabunge wao wote kugawana mitaa ili kuhakikisha ushindi mnono wa chama chao.

Taarifa kamili za matokeo zinaonyesha Chadema pamoja na nguvu kubwa waliotumia jijini Dar es Salaam, wameambulia mtaa mmoja wa Jogoo -Mbezi na mitaa mingine yote zaidi ya 9 ikiwa imechukuliwa na CCM.

Hii ni ishara ya nini kwa Matokeo haya hapo mwaka 2014?

Kichwa cha Habari ilitakiwa kiwe CCM yapoteza kiti serikali ya mtaa wa Jogoo.
 
walianza chadema ni ya wachaga (kilimanjaro tu), sasa wanasema arusha tu, wanasahau kwamba kagera ndio mkoa uliopigia kura kwa chadema kwa asilimia kubwa kuliko mikoa yote nchini mwaka 2010. Sio ajabu ukasikia wakija kusema chadema ni kagera tu, na baadae mwanza tu mwisho ni tanzania tu !

bukoba mjini 2010!
Slaa=16,000+
kikwete=14,000+
 
Mtaa wa Jogoo Mbezi Beach wananchi tulilinda kura zetu pale kisawa sawa maana ccm walileta wapiga kura feki kutoka kawe....Red Brigade walikuwa makini sana kwani zaidi ya mapandikizi 15 yalibainika......
 
CDM haijawa na mapana ya CCM kwa maana ya mtandao ... ikumbukwe fedha na michango ya watanzania kwa miaka mingi ilitumika kujenga na kuunda mifumo ya chama ( yaani CCM) mifumo hii ilihuishwa kwa maagizo ya Serikali hivyo mahusiano ya Serikali na Chama (CCM) yalipozaliwa .... CDM ni chama kinachoundwa kwa nguvu ya Wananchi wenyewe.... Hakitegemei matamko ya serikali kwani serikali "haiwezi kuwa CHAMA" ..... Serikali inapojushusha kuwa CHAMA nchi haitawaliki kwani kunakuwepo na Raia wa aina mbili Wanachama wa Chama tawala na Wengine, wanaofaidika ni Wanachama dhidi ya wananchi wengine .... Serikali inajifunza kusimamia na kukitumikia chama tawala tu...

Chaguzi zote zinaratibiwa na serikali na sote tunajua serikali yetu imejishusha kuwa CCM...! hivyo basi ni dhahiri pale serikali inapoona inamaslahi laazima ushindi uwe wa CCM.... na sehemu serikali inaposhinwa kupata ushindi ni pale Wananchi wanapokataa udhalimu wa serikali yao na kuizuia kuwa ngazi ya CCM .... mwamko huu wa Watu unatokana na kujiamini na kuyataka maendeleo.... Wanachi wa Dar bado hawana wanachokiamini na siyo wataka maendeleo zaidi ya kuyataka maisha ya raia wa kwanza ya U-CCM ili wajidekeze kupewa upendeleo bila kufanya kazi ... Ndio maana ktk biashara zote za serikali kuu hufanywa na wananchi wa Dar peke yao
 
Back
Top Bottom