Uchaguzi mwema CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi mwema CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pdidy, Aug 1, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,552
  Likes Received: 5,757
  Trophy Points: 280
  Mungu awaongoze mchague wale walio wa mungu na sio waliowapa vijisent mungu awabariki
   
 2. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2010
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hivi bila vijisenti inawezekana kweli?

  Hapa napata mgagaziko japo sijui labda lolote laweza kubadili upepo.

  Kila la kheri wana chama chao.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mhhhh haya...
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Itawezekana vipi wachague wasiowapa visenti wakati unasikia sasa hivi takukuru wako busy kila mahali.

  Umefika wakati watanzania tukae, tutafakari na kuwa wazi. Kama wamefanya hivyo ili kupata uteuzi na au udhamini kwenye chama watashindwaje kufanya hivyo kwenye uchaguzi mkuu. Kama uliwahi kucheza mpira wakati wa selection ya 1st eleven kwenye timu lazima ndani ya timu mnapigana viatu ili kupata kujenga uhalali wa kupata namba na ubabe uleule uliuotumia kwenye mazoezi utautumia kwenye mechi ukicheza na adui.

  Tujiulize na tupate majibu ya uhakika na uhalisia ni kwa nini ajenda ya wiki mbili zilizopita ni Rushwa, rushwa, rushwa, rushwa mpaka watanzania wote wanaccm na wasio wananuka rushwa. Lazima tuone kuwa kuna tatizo kubwa sana. Tunalitatuaje hilo tatizo kwa faida ya nchi? Majibu yaliyotolewa na viongozi waandamizi wa chama tawala mwishoni mwa juma hili hayatoi majibu ya kweli kwa tatizo lililopo mbele yetu. Kwa kawaida mtu ukituhumiwa basi inabidi uwekwe pembeni ili kupisha uchunguzi ufanyike lakini wenzetu wanasema ikithibikika ndo watachukua hatua.

  Tusiwe kama mbuni kuweka kichwa shimoni kujificha na adui wakati adui anamuona. Tatizo la Rushwa ni kubwa na lipo hatuwezi kulikimbia ila tunabidi tukabiliane nalo kwa njia yoyote iwayo ile.

  Kuna mbunge mmoja bunge lililopita aliuliza, ( na hakuna aliyejibu mpaka bunge linavunjwa) nani kati yetu alikuja hapa bila ya kutoa rushwa? Wote wakacheka na hakuna aliyebisha ikiwa na maana kuwa ni kawaida kabisa kufanya hivyo. Binafsi sioni ni jinsi gani tunaweza kupata ambao hawajoa vijisenti.

  Tutegemee rafu zaidi na rushwa zaidi kampeni zikianza.
   
Loading...