Uchaguzi mkuu Uganda

Primier

Member
Dec 16, 2015
86
14
07:45 Upigaji kura katika maeneo mengi umeanza, ingawa kwa kuchelewa. Hapa ni Kalangala watu wakipiga kura.

160218044920_uganda_kalangala_voting_624x351_bbc.jpg


07:44 Kuna ripoti kwamba baadhi ya watu wanaotumia simu kuingia mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook wanatatizika. Lakini WhatsApp inafanya kazi.

07:30 Upigaji kura ulifaa kuanza saa moja asubuhi lakini katika vituo vingi, licha ya wapiga kura kujitokeza, shughuli yenyewe haijaanza na wapiga kura wanalalamika. Katika kituo cha Kamwokya Central Market, vifaa vya kupigia kura vinaingizwa kituoni pole pole. Mwangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Madola Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo amekuwa katika kituo hicho.

160218044002_olusegun_obasanjo_uganda_640x360_bbc.jpg

Image caption Bw Obasanjo anaongoza waangalizi wa Jumuiya ya Madola
07:09 Tuangalie takwimu muhimu kuhusu uchaguzi wa Uganda unaofanyika leo.

Takwimu muhimu
Wagombea urais 8
Maeneo bunge 290
Vituo vya kupigia kura 28,010
Wapiga kura waliosajiliwa 15,277,196
07:00 Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa.

06:40 Wapiga kura wameanza kufika katika vituo vya kupigia kura. Hapa ni katika kituo cha Kalangala, katika kisiwa kilichoko katika Ziwa Victoria.

160218035408_uganda_kalangala_voters_640x360_bbc_nocredit.jpg


06:30 (Saa za Afrika Mashariki)


Hujambo! Twatumai umeamka salama. Karibu kwa habari za moja kwa moja kuhusu uchaguzi mkuu wa Uganda.

Wapiga kura 15 milioni nchini Uganda leo wanafika vituoni kupigia kura viongozi wao, kinyang'anyiro cha urais kikivutia wagombea wanane.

160211150458_uganda_elections_woman_640x360_electoralcommissionofuganda_nocredit.jpg

Image copyright Electoral Commission of Uganda

Vituo vya kura vitafunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa kumi alasiri.
 
Nimependa sana mtiririko wa Updates,

Uchaguzi ungekuwa huru na haki ingependeza sana. Hapa kila mmoja anajua tu kwamba kaende kupoteza muda (ni siku ya mapumziko) Maana kama ni mshindi wa Urais anajulikana tangu karatasi za kupigia kura zikiandaliwa..!!!

Hata upande wa Ubunge, Ili kuindanganya jumuiya za Kimataifa kwamba huko Uganda kunademokrasia, Wapinzani watapewa vita 30 kati ya hivyo 290 kisha mambo yataendelea kama kawa..!!

Africa suala la Demokrasia ni msamiati mgumu sana kwa Watawala especially Watawala Madikteta kama huyo Museveni. Poleni sana kina Besigye

BACK TANGANYIKA
 
Me npo hapa mjini kuna hali ya wacwac sana wanajeshi wametanda kila kona ya jiji jambo linalozindisha wacwac..na kuna taarifa ifikapo saa8 mchana kutakuwa hakuna mawacliano ya cm kabsa..watazania wengi waliopo huku hawajatoka ndani leo!
 
Wabunge 290 wapiga kura mil. 15 hiyo ni changamoto kubwa sana kwa nchi ndogo kama uganda
Hivi uganda inakitu gani cha maana hadi wawe na wabunge wote hao 290 wakati india ni nchi kubwa sana na ni ya pili kwa watu wengi duniani inawatu bilion 1.2 lakini inawabunge 400. Tu
Uganda ilitakiwa wapate kiongozi ambaye ataendana na kasi yao lakini hilo halitawezekana kwasababu viongozi wa afrika wanatamaa mno na madaraka na hapo tayari kunamtu ameisha jitangazia ushindi. Na hao upande wauraisi wasifikilie kwamba museveni atatoka madarakani wakomae na wabunge tu.
 
Upigaji kura wachelewa maeneo mengi Uganda(updated news)
Upigaji kura wachelewa maeneo mengi Uganda

160218080247_uganda_voting_640x360_bbc.jpg

Image caption Upigaji kura unafaa kuanza saa moja asubuhi kwa mujibu wa sheria
Wapiga kura nchini Uganda wanaendelea kupiga kura vituoni kuwachagua viongozi, ingawa katika baadhi ya vituo upigaji kura ulichelewa kuanza.


Hili lilitokana na vifaa na karatasi za kupigia kura kutofikishwa vituo kwa wakati katika baadhi ya maeneo.

Mjini Kampala, ambapo makao makuu ya Tume ya Uchaguzi yapo, bado kuna vituo ambavyo kufikia saa nne upigaji kura haukuwa umeanza.


Hata hivyo, tume hiyo kwenye ukurasa wake wa Twitter, imeandika: "Tunabaki kuwa na matumaini na tunawahikishia kwamba nyote mtaweza kupiga kura leo. Tunasikitika kutokana na kuchelewa huku. Asanteni.”

Kuhusu iwapo muda wa kupiga kura utaongezwa, tume hiyo kupitia mitandao ya kijamii imesema kwa mujibu wa sheria, ni sharti vituo vifungwe saa kumi alasiri.

Tume hiyo imeahidi kuhakikisha wapiga kura wote watakaojitokeza kufikia wakati huo wanapiga kura.

160218044002_olusegun_obasanjo_uganda_640x360_bbc.jpg

Image caption Mwangalizi mkuu wa Jumuiya ya Madola Olusegun Obasanjo (kushoto) akizungumza na baadhi ya wapiga kura Kampala
Raia katika maeneo mengi nchini humo pia wanalalamikia kutatizika wakiingia mitandao ya kijamii kama vile Twitter, Facebook na WhatsApp, sana kwa kutumia simu. Serikali haijaeleleza ni nini chanzo cha matatizo hayo.

Kuna wagombea saba wa urais wanaojaribu kuhitimisha uongozi wa Rais Yoweri Museveni ambaye ameongoza kwa miaka 30 sasa.

Wanaotoa ushindani mkubwa kwa Bw Museveni ni mgombea wa FDC Kizza Besigye na waziri mkuu wa zamani Amama Mbabazi.

Kuna jumla ya wapiga kura 15 milioni ambao wamejisajili kupiga kura nchini humo kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi.
 
I am following the Uganda election via their news media. I am not pleased of what NBS TV are doing. They're showing the previous general election statistics where NRM won. This is campaigning during the election day and it is prohibited by Uganda laws governing election issues.
 
Even Urban TV are doing the same., this time they are campaigning for Morieen Kyaala by beaming her vote live. She has voted for herself. I am not sure if they will do the same to other candidates. ...

Ooh No!!! They have not allowed Eng. Mabirrizi to show his vote. This is fraud, people may stand on this to nullify general election results.

I wish Uganda the peaceful general election. God bless Uganda and God bless East Africa Community. Amen
 
WBS TV has information that some candidate's agents have been chased out of polling station. The cause of that saga is unclear. Also they (WBS TV) have noted that there is unusual delay of starting election process in Kampala. Again there is information that some polling stations have recieved wrong election materials. ...!

Courtesy : WBS TV.
 
Shots have been heard in Machinge division polling station in Kampala. A man acting as an Oldman has fired shots to security forces. ....!Police are converging to the area.
.......
UP now some polling stations have not starting voting!
................
 
Delta TV are beaming live chaos where voters composed of large portion of youths are screaming while holding election gargets. ...the place is unspecified.
=========
IT seems some policemen are cornered by voters. ...and as they are extremely calm.
 
Police are are now allowed to leave the scene. Youths are chanting Besigye 's name. boxes are seen to be torn.
Courtesy by Delta TV
 
WBS TV have the information that all journalists are not allowed to enter Namboole before 4 pm .this where election Commission will be announcing election results. This rises the suspicious thoughts to observers.
 
Election commission members have switched off their phones as they can not be reached . Sources : WBS TV
 
You can make a follow up the update on Uganda general election events via most of the TVs websites which I have been fetching info.

Good day!
 
Wabunge 290 wapiga kura mil. 15 hiyo ni changamoto kubwa sana kwa nchi ndogo kama burundi.
Hivi burundi inakitu gani cha maana hadi wawe na wabunge wote hao 290 wakati india ni nchi kubwa sana na ni ya pili kwa watu wengi duniani inawatu bilion 1.2 lakini inawabunge 400. Tu
Burundi ilitakiwa wapate kiongozi ambaye ataendana na kasi yao lakini hilo halitawezekana kwasababu viongozi wa afrika wanatamaa mno na madaraka na hapo tayari kunamtu ameisha jitangazia ushindi. Na hao upande wauraisi wasifikilie kwamba museveni atatoka madarakani wakomae na wabunge tu.
Kazi ipo... Burundi imekujaje hapa?
 
One more info is that most of Uganda social media have been shutdown,!! Africa BBC as quoted by WBS TV.
There is a heavy fighting in Namubende between candidates camps.
 
Wabunge 290 tuseme ni 300 tu kwa nchi ndogo kama Uganda!!!!!!! Yaani Tanzania pamoja na ukubwa wote bado watu tungependa tuwe na wabunge wachache, sasa najiuliza Uganda ingekuwa kubwa walau kufikia robo ya Tanzania tu si ingekuwa na wabunge zaidi ya 1000.
 
Back
Top Bottom