Kuna habari kuwa uchaguzi mkuu wa oktoba mwaka huu huenda usifanyike endapo serikali itaendelea na msimamo wake wa kutoruhusu mgombea binafsi inasemekana kuwa mawakili mbalimbali wakishirikiana na Mwenyekiti wa DP Mchg. Christopher Mtikila na vyama vingine wamejipanga vilivyo kwenda mahakamani mara hukumu itakapotolewa kuruhusu mgombea binafsi ili kusisitiza hukumu hiyo itekelezwe
Tetesi kutoka kwa mawakili zinapendekeza kuwa endapo kama serikali itaona muda uliobaki hautoshi kuandaa mgombea binafsi basi uchaguzi uahirishwe hadi Februari mwaka ujao au hadi serikali itakapokuwa tayari, hukumu hiyo imepangwa kusikilizwa tena April 8 ingawa serikali iliomba muda wa miezi minne kujiandaa iliyopingwa na Mahakama ya rufaa
Je tetesi hizi ni za kweli?
Haya aliyasemea Bungeni hana wa kumshtaki. Baba wa watu kasema yaliyo moyoni mwake na kwa kuzingatia "hali halisi" kama lilivyo jina lako.Tanzania ni nchi ya pekee ndio maana Mahakama tena Jaji Mkuu akiwamo, inatoa tamko anatokea Waziri kama Marmo anasema "Hakuna".... sasa kama anajua watashinda kesi anawezaje kutoa tamko tena bungeni, kwani hiyo pekee ni kuingilia mahakama na ni kosa la jinai ambalo anaweza kushitakiwa na kuhukumiwa. Wanasheria nisaidieni.
Haya aliyasemea Bungeni hana wa kumshtaki. Baba wa watu kasema yaliyo moyoni mwake na kwa kuzingatia "hali halisi" kama lilivyo jina lako.
Kama ulimsikiliza vizuri alikuwa anaongelea muda. Ni swala ambalo litahitaji kubadili KATIBA. Linahitaji mchakato mrefu kidogo. Hukumu ya mahakama haibadili katiba automatically.well kama Marmo kasemea bungeni hawezi kushitakiwa mbona kuna wabunge wengine huzuiwa kuzungumuza bungeni mambo yaliyo mahakamani wakati mwingine hukalishwa chini au kupewa karipio na Spika huoni hiyo ni double standard?
CCM watakapoona mahakama imewabana kisawasawa walitalisukuma suala hili kwenye kura ya maoni. Wana mbinu na njia nyingi za kutokea. Kwa kifupi ni kwamba wasichotaka CCM kifanyike nchi hii hakitafanyika.
Haki ya Watanzania "shouldn't be raped for whatever means by the so called rulers" What is a problem wakirihusu hiyo? Waruhusu tu. watakaoshinda kwa mwelekeo huo ni wachache sana na sana sana sio kwa nafasi ya rais. JK will win and that has no doubt!! Whowever says no, he is blinding himself. He will win not necessarily on performance but on the background that we used to have whereby more youths do not want to come out and vote or they don't go campaign meetings/rallies so that they can make informed decisions. People are still not educated well about haki zao na wanadhani vitu wanavyopata kama vipo ni kwa hisani ya serikali ya CCM. Na ndiyo hata maana DC wa Tarime amediriki kusema mapambano ya kikabila ni kwa sababu wamechagua Chadema...huyu nadhani ni mvivu wa kusoma historia na ni mwongo kwani hata kabla ya vyama vingi huko tarime bado walikuwa wanapigana, je huko rorya, nayo Chadema imeshinda??? ndiyo viongozi tulionao, wanawapotosha wananchi!Yaleyale kama Zanzibar. Kuna kuchaguana basi nchi hii? Mgombea binafsi wa nini wakati huu? Hata kutafuta mchumba tu hauwi mgombea binafsi! Mnataka akina RA, EL, Mzee Mengi, Manji, Mtume na Nabii Mwigira, Kakobe, Sheikh Ponda, Prof Majimarefu, Dr Remmy Ongara, .....wagombee Urais?
Kama ulimsikiliza vizuri alikuwa anaongelea muda. Ni swala ambalo litahitaji kubadili KATIBA. Linahitaji mchakato mrefu kidogo. Hukumu ya mahakama haibadili katiba automatically.
Soma KATIBA yetu ibara ya 39(1)(c). ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;Ndugu WC
nafikiri hapa suala si kubadili katiba hukumu iliyoko ni utata wa katiba yenyewe sehemu moja inaruhusu nyingine hairuhusu Mtikila anachosema ni katiba iheshimiwe kwa hiyo kama atashinda kesi katiba haitabadilishwa kwa sababu imeshasema wazi kila mtu ana haki ya kupiga na kupigiwa kura kinachotakiwa kubadilika ni sheria tu za uchaguzi na si katiba.
Yaleyale kama Zanzibar. Kuna kuchaguana basi nchi hii? Mgombea binafsi wa nini wakati huu? Hata kutafuta mchumba tu hauwi mgombea binafsi! Mnataka akina RA, EL, Mzee Mengi, Manji, Mtume na Nabii Mwigira, Kakobe, Sheikh Ponda, Prof Majimarefu, Dr Remmy Ongara, .....wagombee Urais?
Soma KATIBA yetu ibara ya 39(1)(c). ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;