Mabibi na mabwana heshima kwenu.
Uchaguzi ndiyo hivyo unajongea kampeni nazo zinaendelea. Kila mtu na kila chama na lake.
Wakati wa teuzi palikuwa na fomu yenye kanuni za maadili ya uchaguzi. Nini contents za fomu hii?
Ilikuwa vyema kilichomo kikafahamika kwetu wapiga kura pia. Ili tuweze kuwapima wagombea na hata kuitathimini tume.
Pana mambo mengi ambayo kweli - ni mambo valu valu ya Dr. Remmy (rip).
Pana wagombea wanaongea kutumia lugha za makabila ya kwao. Pana nyimbo zinaimbwa kutumia lugha za makabila ya wagombea kama zilizo rasmi katika kampeni hizi.
Pana upendeleo wa wazi katika matumizi ya radio na tvs zote za binafsi na taifa. Pana kupendelea baadhi ya vyama kutokana na shinikizo la wagombea na vyama fulani fulani.
Pana matamko ya utekelezwaji yanayotolewa kiserikali katika kampeni. Ni ziara za ufuatiliaji za serikali au ni rushwa badala ya kampeni? Ni vipi ufumbuzi wa kiserikali unaweza kutolewa na mgombea yeyote kwenye jukwaa la kampeni?
Pana hata vitisho vya waziwazi kwa wapiga kura vinavyotolewa katika majukwaa ya kampeni. Tume wapo kimya tu.
Hatua zipi tume inaweza kuchukua ili tujiridhishe kuwa haki inatendeka na kuwa hata tutegemee pia kuwa haki itaendelea kutendeka hadi mwisho?
Tume mna wajibu mkubwa katika kulinda haki ili amani iendelee kuwapo.
Taratibu kwa kufumbia macho maovu mengi ya wazi, hii nchi mnaipeleka kusiko.