Elections 2010 Uchaguzi mkuu 2010 kuvurugika

KakaNanii

JF-Expert Member
Sep 28, 2008
325
52
Yaani huwezi amini. Zikiwa zimebaki siku 5 tu kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika WASIMAMIZI WA VIYUO VYA KUPIGIA KURA bado hawajafahamika mpaka sasa.

Mimi nipo katika mkoa wa Dar es salaam. Na nimefuatilia kwa karibu zoezi hili la kuchagua wasimamizi wa vituo vya kupigia kura. Lakini nimeona kuna ujanja mkubwa unafanywa ili kuingiza wasimamizi ambao kwa namna moja au nyingine watapendelea chama tawala.

Ukienda kwa mkurugenzi wa manispaa iwe ya Temeke, Kinondoni hata Ilala. Ukaulizia majina ya Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura atakwambia , majina hayo yameshapelekwa katika Kata husika. Ukienda kwenye kata yako nao wanakwambia hatujaletewa bado hayo majina ya Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura kutoka kwa mkurugenzi .

Lakini katika pita pita zangu mitaani nimepata taarifa kwamba tayari hayo majina yameshatoka na watu sasa hivi wapo kwenye semina za namna ya kusimamia vituo vya kupigia kura na namna ya kuiba kura.

Kama unabisha nenda sasa kwa ama mkurugenzi wa manispaaa husika au kwenye kata yako waulizie hayo majina wameyabandika wapi uone kama watakupa.

Huku viongozi wetu wa siasa wakiwa wamejikita katika kufanya kampeni tu, wakifikiri ndo watashinda , lakini hiyo ni kama kujaza maji kwenye tenga. Maana wenzenu chama tawala mkwaka huu wa 2010 watatumia wasimamizi wa vituo vya kupigia kura katika KUCHAKACHUA matokeo ya uchaguzi. Hivyo vyama vya upinzani kalaga baho na kubobea katika kupiga kampeni tu, wakati mchakato mzima wa kuwapata Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura uanafanywa katika misingi ya KUCHAKACHUA matokeo !!!!

Mwisho ningependa kusema kwamba oezi zima la kuwapata WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA mwaka huu katika jiji la Dar es salaam limejaa mamluki watupu wa chama tawala !!!

MUNGU IBARIKI DAR ES SALAAM !!!
 
Wajitakia wenyewe waliianzisha mgogoro na waalimu wanawaogopa sasa wanashikizia shikizia shikizia tuu,watapatikana tuu hata iweje
 
Wasimamizi lazima wawe kati ya wale 315000 walionyimwa nyongeza ya mishahara na JK kwa madai serikali haina uwezo.Tume hawana ujanja.
 
Unajua mabadiliko ya namna hii ni mapambano (ingawa damu isimwagike!). Si sisi tu, sehemu nyingine walikofanya mabadiliko wamepitia shida hizi hizi. Wote tunaotaka mabadikiko inabidi tushirikiane na kuwajibika kila mmoja wetu kufanya analoweza. Ni vizuri umeleta hii info. Vile vile, kumbuka kuna watu (wengine nawafahamu) wanaosaidia chama tawala kwa kulinda maslahi yao au kupata posho lakini siku ya kupiga kura hawatawapigia CCM. Hawa wako wengi kwenye jeshi, polisi na pengine hata hao wasimamizi wa uchaguzi!
 
Sometimes Uhuru, haki na usawa hupatikana kwa kutumia nguvu. Kama itabidi basi wananchi hawatasita kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom