Nimekupata.
Ila, kwenye political spectrum ya Marekani kumbuka kuwa GOP wengi wa NYC ni centrists/ moderates.
Kwa mfano, hao uliowataja [Giuliani na Bloomberg; na hata George Pataki] wote ni pro--choice ikija kwenye suala la abortion ingawa Pataki nadhani ana vi-exceptions vyake na pia ni pro gay rights.
Na ndo maana walishinda chaguzi kwenye hilo jimbo. Huyo Bloomberg mwenyewe alikuwa Democract hadi mwaka 2001 alipobadili vyama na kuwa Republican. Mwaka 2007 akaondoka GOP na kuwa independent!
Hata Trump mwenyewe siyo conservative kivile.
La sivyo, conservatives kama Jeff Sessions, Tom Coburn, Nathan Deal, na wengineo, kushinda NY state na NYC ni ndoto.
Katika swing states NY haipo kabisa maana yenyewe ni solid blue state.
Angalia hata uone hata electoral college ratings za Centerforpolitics.org uone NY ilipo.
Ni 'safe' Democratic state.
The Crystal Ball‘s 2016 Electoral College ratings (for Hillary Clinton vs. Donald Trump)
NY ile conservative ya 'evangelica'l ni ngumu. Inabidi wawe centrist
Kama ulivyosema, uzalendo ulimshinda Bloomberg mara 3.
Hata hivyo, alipokuwa independent bado alishinda kuonyesha NY ilivyo na utata
Hii ramani inaonyesha namna viti 270 vinavyopatikana uchaguzi mkuu
Utaona kwa wakati huo hakukuwa na ' toss up' states. Hizi hutokea kutokana na ngvu za wagiombea
Kuna nayakati majimbo yanakuwa hayana 'majority' katika kuunga mkono vyama ni ngumu kujua jimbo linaenda wapi bila kujadili huegemea upande gani
Lakini pia ramani inaeleza kwanini popular vote pekee haiwezi kumpa ushindi mhusika
Mfano, Utah ina wajumbe 4 , Washington state 12 , Idaho 4 kwa jumla ya wajumbe 20
Majimbo haya kwa upande wa uchaguzi wa ndani unaonedelea Sanders kashinda yote
Florida, lina wajumbe 29 peke yake, Illinoi 20 peke yake.
Ikifika wakati wa kujenga hoja wajumbe wataangalia hoja kwa mitazamo hii
Sanders: Kwa mfano wa wiki moja iliyopita alishinda majimbo 3, Utah, Idaho, Washington
Utah na Idaho ni majibo ya Republican tena yenye viti 8. Ushindi huo umeeleza nini ktk uchaguzi mkuu? Je, independents kutoka maeneo hayo wapo likely kubadilisha rangi ya jimbo?
Hoja ya Sanders itakuwa, ameshinda jimbo la Washington lenye viti 12 likiwa ni 'safe' kwa Dem
Hii ni pamoja na Michigan na NH inayoegemea Dem, kwamba ana uwezo wa kuyalinda
Hoja ya Bi. Clinton ni kuwa ameshinda Florida, ataweza kuitetea ikiwa na viti 29.
Ameshinda Illinoi anaweza kuitetea ikiwa na viti 20
Mifano hiyo ni kuonyesha jinsi gani super delegates wanavyoangalia wagombea na kufanya ''projections'' nini kitatokea siku za mbeleni kabla ya kuwaunga mkono.
Kwa upande wa Republican, hali ikoje?
.....inaendelea