UCHAGUZI NDANI YA VYAMA, GOP & DEM
Kinachoendelea sasa hivi ni uchaguzi ndani ya vyama kupata mgombea
Marekani, mgombea hupatikana kwa kura za wananchi na si viongozi
Hili limelenga kupata wapiga kura wa chama husika kwa kuwashirikisha kuanzia mwanzo
Kwa maana nyingine, wanachukua 'uhodhi' wa madaraka ya viongozi kupata viongozi
Chaguzi ndani ya vyama zinalenga kupata wajumbe watakaokwenda mkutano mkuu
Mkutano mkuu iwe Republican(RNC) au Dem(DNC) ndiyo unapitisha jina la mgombea
Hivyo, uchaguzi unaoendelea ni kupata wajumbe wa mkutano mkuu
Hapa ieleweke, wajumbe hupatikana katika njia tofauti miongoni mwa vyama
Inapotokea hakuna mjumbe aliyepata idadi ya wajumbe wa kutosha, mkutano mkuu huingia katika kuchagua kiongozi (Brokered convention) au contested convention
Ndilo linaloweza kutokea kama hali ya GOP kuhusiana na 'the establishment' itaendelea
Tutafafanua mbele ya safari
Kwasasa uchaguzi ni primaries, kwamba watu wa majimbo wa vyama husika kuchagua wajumbe wa mkutano mkuu. Mfano, Michigan wanachagua wananchi wote wa kila chama
Yapo majimbo uchaguzi hufanywa na wajumbe wa chama wa jimbo husika(Caucus).
Tueleze wa mifano rahisi. Kwa mfano, CCM inatafuta wajumbe na kila mkoa utapiga kura za kupata idadi ya wajumbe kwenda mkutano mkuu(primairies)
Lakini pia kuna uwezekano mikoa mingine, wajumbe wa CCM wa vitongoji , miji, manispaa au majiji wakakutana na kuchagua wajumbe(Caucus)
Hata pale Dodoma, wabunge wa CCM walipokutana kupitisha jina la Spika, ile inaitwa caucus. Kwamba, ni wajumbe fulani tu wanaopiga kura
Taratibu huu upo kwa vyama vyote. Tofauti ni jinsi vyama vinavyogawana wajumbe
Kwa baadhi ya mjimbo, GOP -atakayeshinda kwa kura anachukua wajumbe wote.
Mfano, Florida, ina wajumbe 50, mshindi atachukua wote bila kujali nani alishinda kitongoji au mji gani
Kwa upande wa Dem, wajumbe wanagawanya kwa uwiano kutokana na ushindi
Mfano, Jimbo la Iowa Hillary na Bernie walipata asilimia 49.. wakipishana point tu.
Hii ina maana kama kuna wajumbe 30, wote watawagawana sawa
Hata hivyo, wapo wajumbe wanaokwenda mkutano mkuu kwa hadhi zao ndani ya vyama
Ndio maana utasikia non committed delegates , super delegate n.k
Ikitokea hakuna mjumbe aliyefikisha idadi inayotakiwa, ngoma inakwenda mkutan mkuu ambako kura zitapigwa kwa wagombea waliobaki(Brokered convention)
Utaratibu ni mpana sana unaohakikisha demokrasi inafanya kazi.
Tunajaribu kueleza katika lugha nyepesi na kuchukua muhimu ili tuwe pamoja
Kwa majimbo yaliyofanya uchaguzi,Trump anaongoza kwa GOP, na Clinton kwa Dem
Kwa upande wa Dem, uwiano wa wajumbe hufanya mchakato kuwa mrefu
Kwa GOP, mshindi anachukua wote, inaleta tatizo sana hasa kwa wasiomtaka Trump
Hivyo, jitihada zinazoendelea ni kuhakikisha Trump hafikishi idadi ya wajumbe wanaotakiwa mchezo uhamie mkutano mkuu ambako ndiko 'machinjio' yanapowezekana
Si rahisi kwa kuangalia hali ya uchaguzi mkuu!!Wajumbe wa Trump wanatokana na wananchi. Je, ni vema kumchinja akiwa na wafuasi?
GOP wanaogopa mkutano mkuu,historia inaonyesha huvunja umoja wa chama'makovu'
Republican wamefikaje hapo walipo? Nini kinamzuia Hillary Clinton hadi sasa?
Tutajadili