Uchaguzi Igunga: Ni lini Upinzani utajifunza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi Igunga: Ni lini Upinzani utajifunza?

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Mo-TOWN, Oct 2, 2011.

 1. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 160
  Natumia neno upinzani nikimaanisha kuwa upinzani unatarajiwa au walau unapashwa kuwa na united front...after all wanapingana na timu moja-chama tawala.

  Swali kuwa lini upinzani utajifunza linatokana na matokeo ya uchaguzi wa Igunga hii leo. Ukweli ni kwamba CCM watashida (kihalali au kiwizi) kwa kupata 20% ya kura wakati Upinzani collectively watagawana 80% (vyama 7).

  Ushindi wa CCM Igunga God forbid...uwe wa kihalali au kwa wizi kutatokana na exposure kwa wapinzani kwa kukosa umoja miongoni mwao. Watch this space
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Toa upupu wako hapa.Magamba mkubwa wewe
   
 3. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Hata ww haujajifunza bado,SWALI KWAKO;kama upinzani hauwezi kushinda ilikuwaje asilimia 80% ya CCM ikashuka hadi 61%,na (b),ilikuwaje CDM kikashinda majimbo 21 kwa kishindo na (c),kama CDM haikushinda ilikuwaje CCM wakachakachua mpaka leo hii Makame anastaafu NEC haijawahi kutoa data za matokeo kama taharifa rasmi?

  NB: Majibu yako ni muhimu mkuu.
   
 4. G

  GUN B Member

  #4
  Oct 2, 2011
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Matokeo hayajatanganzwa,isitoshe sasa hivi bado watu wanapiga kura, wewe unasema ccm wanashinda kwa 20%.una matatizo wewe
   
 5. WOWOWO

  WOWOWO JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2011
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Fikra zako ni mgando sana.Kwani ni lazima tuwe na chama kimoja cha upinzani?Kwa jinsi CDM ilivyo na nguvu inahitaji kusaka kuungwa mkono na CUF?Kwa lipi hasa wakati CUF ni CCM B kwa sasa?Kama umefuatilia kampeni za Igunga unawezaje krahisirahisi kuwapa Magamba ushindi wakati mchuano unaonekana ni mkali?Badilika mkuu.
   
 6. d

  dotto JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwani CCM sio chama cha upinzani Igunga? Mtazamo wako ukoje!
   
 7. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Sioni ni wapi MoTown amekosea, yuko sahii kwa wazo alilokuja nalo: ushirikiano kwa vyama upinzani ili kuin'goa CCM ni muhimu sasa, hivi vyama vyetu vya upinzani unakuta vinapingana vyenyewe kwa vyenyewe ni hatari na itatuchukua muda kufanya kama watu wa Zambia.

  we just imagine endapo CCM kule Igunga ikipata 20% ya kula zote na zikabaki 80% zikagawanywa kwa vyama 7 ina maana kila chama kitapata 11.4% ambazo ni ndogo sana huyo ni mfano.

  Inabidi tufikilie kwa makini kama tunania ya kuachana na haya magamba kwa ujumla
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kwanza Chama kama Chadema waungane na chama gani ?
  Kuna vyama vilikuwa igunga muda wote nimevisikia leo navyo vya kuungana na Chadema .KUna vyama kama Bakwata, KAFU na CCM wao wameungana kwa maslahi ya matumbo yao si taifa .
   
 9. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160

  Ukitumia akili kidogo tu utagundua vyama vya upinzani haviwezi kuungana.
  Hivi kweli cdm ikiungana na cuf si ndio ccm wanafanya party? Hata mm nitahamia Zambia!
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  Oct 2, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Stori kama hizi mkuu ni zilipendwa. Unapoongelea upinzani unamaanisha nini hasa?, Katika uchaguzi wowote ule vyama vyote vinavyoshiriki ni pinzani. Kwa taarifa yako ni kwamba wananchi sasa wanaakili sana kuhusu elimu ya uchaguzi na vyama makini kuliko 1995, 2000, 2005 and 2010. Ni nani asiyejua kuwa kuna vyama vya siasa vimeanzishwa na CCM kwa siri strategically?. Under free and fair election CCM haina chake katika chaguzi za Tanzania ya leo. Napoongelea free and fair election nina maana kuwa
  1. Tume huru ya uchaguzi inayofanya kazi kama chombo kinachojitegemea na wafanyakazi wake hawatokani na hisani ya kupewa madaraka na serikali ya CCM
  2. Kila mtu mwenye sifa za kupiga kura anapiga kura bila ya kuangaishwa au kukuta jina lake halipo
  3. Matokeo ya vituoni yanakuwa ndiyo ya Mwisho na kila chama kilichoshiriki kinaondoka na kopi ya matokeo ya kituo na kuwa na kuyajumlisha, kama vile mwanafunzi anapopata matokeo yake ya mtihani na kujumlisha kujua amepata wastani wa ngapi
  4. Msimamizi wa uchaguzi hana ya haki ya mwisko ya kumtangaza mshindi bali ni kujumlisha kwa uwazi matokeo yote ya vituo, kata na jimbo kwa ajili ya official documentation na kuyasini baada ya kukubaliana na tallies za vyama vyote.
  5. Kama mtu hajaridhika na matokeo ya uchaguzi anapinga mahakamani na kwa kupinga huko Jimbo linakuwa wazi mpaka shauri likiamuliwa na mahakana inapewa miezi mitatu ya kuammua baada ya ushahidi kuwasilishwa mfululizo.
   
 11. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #11
  Oct 2, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Cha msingi CDM inabidi iendelee kukaza buti, ifanye mambo yake kwa uhakika bila kuteteleka huto tuvyama tudogotudogo na wapambe wao wataifuata tu; hata kama ushindi kwa leo usisopatikana CDM hatupaswi kukata tamaa.
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Oct 2, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  wewe ni masaburi kweli..nani amekwambia bakwata ni chama....acha udini na hufai kuwepo ktk great thinkers.
   
 13. p

  plawala JF-Expert Member

  #13
  Oct 2, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuungana ni hiari,na ni pale ambapo vyama vyenyewe vina sera na mikakati inayoendana na kuwa na maelewano yanayofahamika
   
 14. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #14
  Oct 2, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  How old are you?
   
 15. Criss

  Criss JF-Expert Member

  #15
  Oct 2, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 825
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi vyama vya upinzani unavyozungumzia ni vipi hivyo mkuu ?
  au nijamii ya vile vya akina Mutamwega hahahahaa

  Hivi inaleta tija gani kuungana na vyama dhaifu, ni uvivu tu wa kufikiri au ni uoga binafsi?

  Huvi hivyo vyama vingine vinavyoweza kugawana kura sawa na CDM kwa mtazamo wako?

  Tuache akili za kike kusindikizwa kicmani na mtoto mdogo eti tu kwa kua niwakiume.
   
 16. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #16
  Oct 2, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huwezi kujenga demokrasia kwa kuunganisha vyama kwenye chaguzi, vyama vitajifuta vyenyewe na imara vitahimili na kuishi, huwezi kulazimisha watu wenye itikadi na malengo tofauti waungane hilo litakuwa ni kuua demokrasia
   
 17. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #17
  Oct 2, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Hapa hakuna utitiri kama unavyodai. Ila kuna vyama makini vya upinzani na matawi ya ccm. Haya matawi yamepewa jina la upinzani ili kuwahadaa watu na kucheza na akili za watanganyika.


   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Oct 2, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kujifunza kwa upinzani sio lazima iwe kwa style hii unayotaka wewe. Uchaguzi mkuu uliopita hakuna mpinzani aliyemuachia mwenzake lakini bado walishinda baadhi ya majimbo.

  Hata pale ambapo baadhi ya vyama vya upinzani vilishindwa kusimamisha wagombea bado ccm ilishinda mfano mzuri ni igunga yenyewe.

  Kwahiyo observation yako haina mantiki kabisa.
   
 19. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #19
  Oct 2, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Ushirikiano wa vyama ni muhimu hata kama mnatofautiana kinachowaunganisha ni kumwondoa ccm madarakani baada ya hapo vyama ndio viangalie utofauti wa sera zao. Tofauti na hilo kama ni haya tunayoyaona Igunga; vyama kugombana wao kwa wao, mifano ya Kenya na Zambia haitatokea kwetu hapa!
   
 20. B

  Bandiho New Member

  #20
  Oct 2, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni muda wa watanzania kuchagua watu ambao wataisaidia nchi na si mpaka wapinzani waungane, suala ni nani anachaguliwa, hivyo wananchi wanatakiwa kugutuka na kuchagua 1. chama ambacho wanaona kitawasaidia 2. mtu ambae atakuwa msaada kwao , kwa kuzinga tia haya ccm kwao itakuwa mwisho.
   
Loading...